Anajaribu kuua makundi ndani ya mfumo lakini ili afanikiwe aanzishe mjadala wa rasimu ya warioba,ndio itakayomaliza mzizi wote wa fitina na kuukatilia mbali kiasi kwamba mtu yeyote maadam ni mtanzania anaweza kuwa kiongozi bila kuathiri misingi ya utawala bora.
Vinginevyo siku akiondoka watakaoingia wataturudisha kule kule kwa vile atakuwa hajafanya mabadiliko ya kweli kikatiba.
Hamuhitaji katiba mpya, tunahitaji marekebisho makubwa ya katiba iliyopo. Katiba ya warioba inaitaka nchi iwe na katiba tatu tofauti badala ya kuwa na katiba moja yenye sehemu kuu tatu. Ukishakuwa na katiba tatu kila mamlaka itakuwa na uwezo wa kuchezea katiba yake vile ipendavyo. Na haya tunayaona sasa jinsi zanzibar inavyosubua kupitia katika yao. Katiba mama haina cha kufanya.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.