M
MegaPyne
Guest
WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, ametoboa siri nzito ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, jinsi alivyomteua mara mbili kuwa waziri mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kuwa waziri mkuu pekee aliyelitumikia taifa kwa mihula miwili mfululizo.
Sambamba na hilo, Sumaye alisema kwa jinsi mambo yanavyokwenda nchini, anamshukuru Mungu kwamba alishindwa katika Uchaguzi Mkuu wa rais wa Jamhuri ya Muungano.
Sumaye alisema hayo juzi katika mahojiano maalumu na kipindi cha Jicho Letu wiki hii, kinachorushwa hewani na kituo cha redio cha Clouds FM. Mahojiano hayo ya Sumaye, yanatarajiwa kurushwa na kipindi hicho Jumamosi ijayo.
Bila kufafanua kwa undani, Sumaye alisisitiza kuwa kwa jinsi hali ya mambo inavyokwenda kiuchumi, kisiasa na kijamii, hajutii kabisa kuikosa nafasi hiyo iliyokutanisha wagombea wengine 11 kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hatimaye Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kuibuka mshindi.
Katika mahojiano hayo, Sumaye alitoboa siri ya mshituko alioupata siku alipoitwa na Rais mstaafu Mkapa, na kujulishwa nia ya kutaka kumteua ili awe waziri mkuu.
Kusema ukweli, sikuwa na habari hadi saa 7:30 ya siku ya uteuzi, ndipo Rais Mkapa aliponidokeza nia yake ya kutaka niwe waziri mkuu. Sikutegemea wala sikuota kama naweza kuwa waziri mkuu na hakuna mtu yeyote aliyejua mpango huo, kwani hakuna habari zilizovuja kabla, anasema.
Alisema siku hiyo, akiwa nyumbani kwake amejipumzisha, alipata taarifa za kuitwa Ikulu na Rais Mkapa.
Wala sikutegemea habari ya kuwa waziri mkuu, maana hata Mkapa mwenyewe sikuwa nimezoeana naye, alisema.
Mwanzoni nilifikiri labda ni mambo hayo ya Baraza la Mawaziri, pengine anataka kuniambia nitakuwa au sitakuwa kwenye Baraza la Mawaziri. Nikaenda, nilipofika, akaniambia ameniteua, nilishtuka sana aliponiambia, nami nilimwambia kwamba, sidhani kama kazi hii naiweza, alisema.
Nilimwambia, kwanini usitafute mtu mwingine, lakini yeye aliniambia, ahaaa! hapa hakuna majadiliano tena, jina nimeshapeleka kwa Spika, wakati huo (Pius Msekwa) na saa 11 atakuita, nakupa taarifa tu ili ukajiandae na hakuna habari za kupatana hapa, tayari nimeshaamua, alisema.
Wakati ule alikuwa hapa Karimjee. Nilipata shida sana, nikaondoka, nikapita ofisini, sekretari aliponiona nimechanganyikiwa, akaniuliza kuna nini bosi, nikawa sisemi na mtu, nikaondoka, nikaenda nyumbani, alisema Sumaye.
Alipofika nyumbani na kukutana na mke wake, Sumaye alisema: Nilimwambia mke wangu, rais ameniteua kuwa waziri mkuu, na kitu cha kwanza akaniambia, usikute umekubali. Ugomvi ukanzia hapo, nikamwambia, nimejaribu kukataa, lakini ameningangania, alisema Sumaye, huku akicheka.
Kuhusu uteuzi wa awamu ya pili uliowahi kuzua gumzo nchini, Sumaye alisema kama ilivyokuwa mara ya kwanza, safari hii hakutarajia kabisa kuendelea na nafasi hiyo.
Alisema hakutarajia kwa sababu mara baada ya kumaliza muda wake wa miaka mitano, alikwenda kumuaga Rais Mkapa, kwani hakutaka kurejea tena kwenye nafasi hiyo, hasa kutokana na misukosuko mingi aliyokutana nayo katika kipindi cha miaka mitano ya muhula wa kwanza.
Alisema, lakini baada ya uchaguzi kufanyika, Rais Mkapa alimpigia tena simu na kumweleza nia yake ya kutaka aendelee na nafasi hiyo.
Safari hii nilikataa kwa nguvu zangu zote, kiasi cha kugombana naye, niligoma kweli kweli. Nilimwambia Rais Mkapa kuwa safari hii, sipendi kuendelea na nafasi hii, kwa vile nimegombana sana na wabunge, alisema.
Alisema alikorofishana na wabunge kwa sababu alikuwa akipinga hoja zao za kutaka kuongezewa mishahara na marupurupu.
Nikamwambia, ukipeleka jina wale wabunge watakaa kulipitisha, hivyo ni bora safari hii umchague mtu mwingine, alisema.
Kwa mujibu wa Sumaye, Mkapa alimlazimisha aende, na kama wabunge watamkataa, basi itajulikana hapo na atajua la kufanya.
Mkapa alikataa na kuniambia, kama watakutaa, basi tutajua la kufanya, lakini nionavyo, huwezi kukosa nusu ya kura za wabunge, alisema Sumaye.
Hata hivyo kwenye hatua ya kupitisha jina lake, Sumaye aliweza kupata kura nyingi, ni tatu tu ndizo zilizomkataa.
Kuhusu makundi yaliyochipuka wakati wa uchaguzi na kuendelea hadi sasa, Sumaye alisema yalishakufa na kuzikwa, lakini bado kuna makundi yanayofuata watu, huku yakitembea na matumaini ya urais mifukoni mwao.
Makundi ya uchaguzi yalishakufa, lakini bado kuna makundi yanayofuata watu kutokana na umaarufu wa nafasi zao. Hao bado wanauota urais, na bado wanatembea na urais mifukoni, alisema Sumaye.
Mbali ya kutoboa siri ya uteuzi wake, Sumaye pia alizungumzia uwezekano wa kuwania tena nafasi ya urais katika uchaguzi ujao, suala tata la utaifa wa Zanzibar na dawa ya kumaliza tatizo hilo. Sehemu hiyo ya mahojiano itaendelea kesho.