Sumaye atoa siri

M

MegaPyne

Guest
WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, ametoboa siri nzito ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, jinsi alivyomteua mara mbili kuwa waziri mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kuwa waziri mkuu pekee aliyelitumikia taifa kwa mihula miwili mfululizo.

Sambamba na hilo, Sumaye alisema kwa jinsi mambo yanavyokwenda nchini, anamshukuru Mungu kwamba alishindwa katika Uchaguzi Mkuu wa rais wa Jamhuri ya Muungano.

Sumaye alisema hayo juzi katika mahojiano maalumu na kipindi cha ‘Jicho Letu’ wiki hii, kinachorushwa hewani na kituo cha redio cha Clouds FM. Mahojiano hayo ya Sumaye, yanatarajiwa kurushwa na kipindi hicho Jumamosi ijayo.
Bila kufafanua kwa undani, Sumaye alisisitiza kuwa kwa jinsi hali ya mambo inavyokwenda kiuchumi, kisiasa na kijamii, hajutii kabisa kuikosa nafasi hiyo iliyokutanisha wagombea wengine 11 kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hatimaye Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kuibuka mshindi.

Katika mahojiano hayo, Sumaye alitoboa siri ya mshituko alioupata siku alipoitwa na Rais mstaafu Mkapa, na kujulishwa nia ya kutaka kumteua ili awe waziri mkuu.

‘‘Kusema ukweli, sikuwa na habari hadi saa 7:30 ya siku ya uteuzi, ndipo Rais Mkapa aliponidokeza nia yake ya kutaka niwe waziri mkuu. Sikutegemea wala sikuota kama naweza kuwa waziri mkuu na hakuna mtu yeyote aliyejua mpango huo, kwani hakuna habari zilizovuja kabla,” anasema.

Alisema siku hiyo, akiwa nyumbani kwake amejipumzisha, alipata taarifa za kuitwa Ikulu na Rais Mkapa.

‘‘Wala sikutegemea habari ya kuwa waziri mkuu, maana hata Mkapa mwenyewe sikuwa nimezoeana naye,” alisema.

‘‘Mwanzoni nilifikiri labda ni mambo hayo ya Baraza la Mawaziri, pengine anataka kuniambia nitakuwa au sitakuwa kwenye Baraza la Mawaziri. Nikaenda, nilipofika, akaniambia ameniteua, nilishtuka sana aliponiambia, nami nilimwambia kwamba, sidhani kama kazi hii naiweza,” alisema.

‘‘Nilimwambia, kwanini usitafute mtu mwingine, lakini yeye aliniambia, ahaaa! hapa hakuna majadiliano tena, jina nimeshapeleka kwa Spika, wakati huo (Pius Msekwa) na saa 11 atakuita, nakupa taarifa tu ili ukajiandae na hakuna habari za kupatana hapa, tayari nimeshaamua,” alisema.

‘‘Wakati ule alikuwa hapa Karimjee. Nilipata shida sana, nikaondoka, nikapita ofisini, sekretari aliponiona nimechanganyikiwa, akaniuliza kuna nini bosi, nikawa sisemi na mtu, nikaondoka, nikaenda nyumbani,” alisema Sumaye.

Alipofika nyumbani na kukutana na mke wake, Sumaye alisema: ‘‘Nilimwambia mke wangu, rais ameniteua kuwa waziri mkuu, na kitu cha kwanza akaniambia, usikute umekubali. Ugomvi ukanzia hapo, nikamwambia, nimejaribu kukataa, lakini amening’ang’ania,” alisema Sumaye, huku akicheka.

Kuhusu uteuzi wa awamu ya pili uliowahi kuzua gumzo nchini, Sumaye alisema kama ilivyokuwa mara ya kwanza, safari hii hakutarajia kabisa kuendelea na nafasi hiyo.

Alisema hakutarajia kwa sababu mara baada ya kumaliza muda wake wa miaka mitano, alikwenda kumuaga Rais Mkapa, kwani hakutaka kurejea tena kwenye nafasi hiyo, hasa kutokana na misukosuko mingi aliyokutana nayo katika kipindi cha miaka mitano ya muhula wa kwanza.

Alisema, lakini baada ya uchaguzi kufanyika, Rais Mkapa alimpigia tena simu na kumweleza nia yake ya kutaka aendelee na nafasi hiyo.

‘‘Safari hii nilikataa kwa nguvu zangu zote, kiasi cha kugombana naye, niligoma kweli kweli. Nilimwambia Rais Mkapa kuwa safari hii, sipendi kuendelea na nafasi hii, kwa vile nimegombana sana na wabunge,” alisema.
Alisema alikorofishana na wabunge kwa sababu alikuwa akipinga hoja zao za kutaka kuongezewa mishahara na marupurupu.

‘‘Nikamwambia, ukipeleka jina wale wabunge watakaa kulipitisha, hivyo ni bora safari hii umchague mtu mwingine,” alisema.

Kwa mujibu wa Sumaye, Mkapa alimlazimisha aende, na kama wabunge watamkataa, basi itajulikana hapo na atajua la kufanya.

‘‘Mkapa alikataa na kuniambia, kama watakutaa, basi tutajua la kufanya, lakini nionavyo, huwezi kukosa nusu ya kura za wabunge,” alisema Sumaye.

Hata hivyo kwenye hatua ya kupitisha jina lake, Sumaye aliweza kupata kura nyingi, ni tatu tu ndizo zilizomkataa.

Kuhusu makundi yaliyochipuka wakati wa uchaguzi na kuendelea hadi sasa, Sumaye alisema yalishakufa na kuzikwa, lakini bado kuna makundi yanayofuata watu, huku yakitembea na matumaini ya urais mifukoni mwao.

“Makundi ya uchaguzi yalishakufa, lakini bado kuna makundi yanayofuata watu kutokana na umaarufu wa nafasi zao. Hao bado wanauota urais, na bado wanatembea na urais mifukoni,” alisema Sumaye.

Mbali ya kutoboa siri ya uteuzi wake, Sumaye pia alizungumzia uwezekano wa kuwania tena nafasi ya urais katika uchaguzi ujao, suala tata la utaifa wa Zanzibar na dawa ya kumaliza tatizo hilo. Sehemu hiyo ya mahojiano itaendelea kesho.
 
Very ironical siri gani hapa?
Anajifanya alikataa ama ndiyo alishangilia kupata hiyo nafasi?Kumbe analijua kwamba alikuwa hapendwi ndio maana alishikwa na wasiwasi hatapitishwa na wabunge.
Hawa viongozi wanafurahisha sana na wewe unayeiita hii siri go find a better secret kuhusu huyu mtu ndio uite siri.I suggest ungesema 'Sumaye Atema Porojo Zake.'
 
WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, ametoboa siri nzito ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, jinsi alivyomteua mara mbili kuwa waziri mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kuwa waziri mkuu pekee aliyelitumikia taifa kwa mihula miwili mfululizo.

Sambamba na hilo, Sumaye alisema kwa jinsi mambo yanavyokwenda nchini, anamshukuru Mungu kwamba alishindwa katika Uchaguzi Mkuu wa rais wa Jamhuri ya Muungano.

Sumaye alisema hayo juzi katika mahojiano maalumu na kipindi cha ‘Jicho Letu’ wiki hii, kinachorushwa hewani na kituo cha redio cha Clouds FM. Mahojiano hayo ya Sumaye, yanatarajiwa kurushwa na kipindi hicho Jumamosi ijayo.
Bila kufafanua kwa undani, Sumaye alisisitiza kuwa kwa jinsi hali ya mambo inavyokwenda kiuchumi, kisiasa na kijamii, hajutii kabisa kuikosa nafasi hiyo iliyokutanisha wagombea wengine 11 kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hatimaye Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kuibuka mshindi.

Katika mahojiano hayo, Sumaye alitoboa siri ya mshituko alioupata siku alipoitwa na Rais mstaafu Mkapa, na kujulishwa nia ya kutaka kumteua ili awe waziri mkuu.

‘‘Kusema ukweli, sikuwa na habari hadi saa 7:30 ya siku ya uteuzi, ndipo Rais Mkapa aliponidokeza nia yake ya kutaka niwe waziri mkuu. Sikutegemea wala sikuota kama naweza kuwa waziri mkuu na hakuna mtu yeyote aliyejua mpango huo, kwani hakuna habari zilizovuja kabla,” anasema.

Alisema siku hiyo, akiwa nyumbani kwake amejipumzisha, alipata taarifa za kuitwa Ikulu na Rais Mkapa.

‘‘Wala sikutegemea habari ya kuwa waziri mkuu, maana hata Mkapa mwenyewe sikuwa nimezoeana naye,” alisema.

‘‘Mwanzoni nilifikiri labda ni mambo hayo ya Baraza la Mawaziri, pengine anataka kuniambia nitakuwa au sitakuwa kwenye Baraza la Mawaziri. Nikaenda, nilipofika, akaniambia ameniteua, nilishtuka sana aliponiambia, nami nilimwambia kwamba, sidhani kama kazi hii naiweza,” alisema.

‘‘Nilimwambia, kwanini usitafute mtu mwingine, lakini yeye aliniambia, ahaaa! hapa hakuna majadiliano tena, jina nimeshapeleka kwa Spika, wakati huo (Pius Msekwa) na saa 11 atakuita, nakupa taarifa tu ili ukajiandae na hakuna habari za kupatana hapa, tayari nimeshaamua,” alisema.

‘‘Wakati ule alikuwa hapa Karimjee. Nilipata shida sana, nikaondoka, nikapita ofisini, sekretari aliponiona nimechanganyikiwa, akaniuliza kuna nini bosi, nikawa sisemi na mtu, nikaondoka, nikaenda nyumbani,” alisema Sumaye.

Alipofika nyumbani na kukutana na mke wake, Sumaye alisema: ‘‘Nilimwambia mke wangu, rais ameniteua kuwa waziri mkuu, na kitu cha kwanza akaniambia, usikute umekubali. Ugomvi ukanzia hapo, nikamwambia, nimejaribu kukataa, lakini amening’ang’ania,” alisema Sumaye, huku akicheka.

Kuhusu uteuzi wa awamu ya pili uliowahi kuzua gumzo nchini, Sumaye alisema kama ilivyokuwa mara ya kwanza, safari hii hakutarajia kabisa kuendelea na nafasi hiyo.

Alisema hakutarajia kwa sababu mara baada ya kumaliza muda wake wa miaka mitano, alikwenda kumuaga Rais Mkapa, kwani hakutaka kurejea tena kwenye nafasi hiyo, hasa kutokana na misukosuko mingi aliyokutana nayo katika kipindi cha miaka mitano ya muhula wa kwanza.

Alisema, lakini baada ya uchaguzi kufanyika, Rais Mkapa alimpigia tena simu na kumweleza nia yake ya kutaka aendelee na nafasi hiyo.

‘‘Safari hii nilikataa kwa nguvu zangu zote, kiasi cha kugombana naye, niligoma kweli kweli. Nilimwambia Rais Mkapa kuwa safari hii, sipendi kuendelea na nafasi hii, kwa vile nimegombana sana na wabunge,” alisema.
Alisema alikorofishana na wabunge kwa sababu alikuwa akipinga hoja zao za kutaka kuongezewa mishahara na marupurupu.

‘‘Nikamwambia, ukipeleka jina wale wabunge watakaa kulipitisha, hivyo ni bora safari hii umchague mtu mwingine,” alisema.

Kwa mujibu wa Sumaye, Mkapa alimlazimisha aende, na kama wabunge watamkataa, basi itajulikana hapo na atajua la kufanya.

‘‘Mkapa alikataa na kuniambia, kama watakutaa, basi tutajua la kufanya, lakini nionavyo, huwezi kukosa nusu ya kura za wabunge,” alisema Sumaye.

Hata hivyo kwenye hatua ya kupitisha jina lake, Sumaye aliweza kupata kura nyingi, ni tatu tu ndizo zilizomkataa.

Kuhusu makundi yaliyochipuka wakati wa uchaguzi na kuendelea hadi sasa, Sumaye alisema yalishakufa na kuzikwa, lakini bado kuna makundi yanayofuata watu, huku yakitembea na matumaini ya urais mifukoni mwao.

“Makundi ya uchaguzi yalishakufa, lakini bado kuna makundi yanayofuata watu kutokana na umaarufu wa nafasi zao. Hao bado wanauota urais, na bado wanatembea na urais mifukoni,” alisema Sumaye.

Mbali ya kutoboa siri ya uteuzi wake, Sumaye pia alizungumzia uwezekano wa kuwania tena nafasi ya urais katika uchaguzi ujao, suala tata la utaifa wa Zanzibar na dawa ya kumaliza tatizo hilo. Sehemu hiyo ya mahojiano itaendelea kesho.Nimesoma word to word and between lines, nashangaa sijaona siri!
 
Ni nondo znuri sana kujua hata huwa inakuwaje kuteuliwa na kujadiliana na mkuu wa kaya hadi kufikia uamuzii...nasi tunapata pich na kujijenga...kisaikolojia...ni nzurii,......ila kwa upande mwingine kujua kwa nini alisema hawezii au kwa nini alikataa second term hayo ndio ya kuyajadili kwa kina na kutoa sababu muafaka ...........pia kuangalia kwa nini alimchagua yeye???
 
Nimesoma word to word and between lines, nashangaa sijaona siri!
Kungururu na kevo nini maana ya siri?

Ulikuwa unafahamu kama aliitwa na Rais Muda wa saa Saba,na kwa taarifa yako hakuna aliyejua uteuzi wa PM kipindi cha Mkapa.

Je ulikuwa unajua kama yeye alikataa kuchaguliwa kuwa PM second Time?
 
Sumaye...is a spent force.Hana mpya ila anataka kujisafisha.He was a nobody,and like his colleague he is now a billionear.
 
Jamaa ana siri hebu tumsikie. kwanza hatukujua aliwahi kukataa hiyo nafasi wakati wa uteuzi mara mbili!!!!!! halafu hisia zake kwa siasa za wakati huu ni muhimu tuzijuee...kwa nini anafurahia kuukosa uraisi kipindi hichi kwa jinsi mambo yanavyokwendaaaa!??? ATUPATIE NJIA..
tofauti ni kwamba uteuzi wake ulikuwa siri sana kuliko huuu wa jamaa wa majuzi...EL..
ni muhimu mkuu wa kaya kuwa na siri kwenye uteuzi wa nafasi nyeti za uongozi wa umma???TUJADILI.
 
Nyauba,
Hivi una amini ni kweli kama alikataa au la?Huyu ni mwongo anataka kutuonyesha kuwa alikuwa hana haja sana na hii nafasi ila ni mroho mno.Unadhani sasa hivi akitaka kupewa hii nafasi ya Uwaziri Mkuu atakataa?
Changa la Macho hilo!
 
Hivi ndivyo Tanzania inavyopata Waziri Mkuu waungwana!!
Kweli mabadiliko ya Katiba hayaepukiki!

.
 
Kungururu na kevo nini maana ya siri?

Ulikuwa unafahamu kama aliitwa na Rais Muda wa saa Saba,na kwa taarifa yako hakuna aliyejua uteuzi wa PM kipindi cha Mkapa.

Je ulikuwa unajua kama yeye alikataa kuchaguliwa kuwa PM second Time?
Gembe, ukweli ni kuwa hizi si porojo za Sumaye, nakubaliana nawe kuwa kuna mengi ambayo wengi hatukujua. Tena nadhani akipata mtu wa kuhojiana naye kwa kina zaidi huyu Sumaye anaweza kutoa zaidi ya haya. Mwanakijiji can you do us this favor?

Mac
 
Kweli mkapa alikuwa mgumu!!
kumteua mtu ambaye hana mazoea naye!!
Manake ccm lazima ujulikane ndio upewe nafasi,
au kama si ugumu wa mkapa, basi sumaye alikuwa hana ishu yoyote ambayo ni threat kwa chama chetu cha mapinduzi, hakuwa na agenda yoyote alikuwepo tu, ready for the PICK!!
kwa maana hiyo hawezi kuwa rais, hana agenda,
 
Mimi namuelewa Sumaye alichosema. Sawa! kama alikuwa anajua kuwakuna misuko suko mingi katika siasa kiasi kwamba mara mbili alikataa kata kata uteuzi wa u PM je, alikuwaje akawania Urais ambao ni post ngumu zaidi? Sawa naweza kumuelewa kwa ile mara ya kwanza lakini hata kwa mara ya pili na hata kuwania urais?
Hapo simuelewi.
Alipokataa mara ya kwanza alishaonja utamu wa ikulu na akatamani naye aende huko akachume kama fisadi BWM, maana aligundua ikulu ni mahala pa kuchuma.
 
Ukweli ni kuwa hawa wanapofungua vinywa kidogo inatakiwa kuwachangamkia kabla hawajabadili mawazo na kuvifunga. BWM alipofungua kinywa kidogo angepata mtu wa kuendelea kumchokonoa ingekuwa deal kweli
 
Hivi kwa nini huyu bwana mkubwa hatajwi kwenye masakata yote haya yanayoendelea sasa. Nadhani kuna staili nyingine ya ufisadi ambayo hatujaigundua ambayo yeye na wengine waliitumia kutajirika kwa kiwango hicho walipo. Ni ipi hiyo?
 
Ni nondo znuri sana kujua hata huwa inakuwaje kuteuliwa na kujadiliana na mkuu wa kaya hadi kufikia uamuzii...nasi tunapata pich na kujijenga...kisaikolojia...ni nzurii,......ila kwa upande mwingine kujua kwa nini alisema hawezii au kwa nini alikataa second term hayo ndio ya kuyajadili kwa kina na kutoa sababu muafaka ...........pia kuangalia kwa nini alimchagua yeye???

Mkuu, hapa naspeculate tu kwamba labda Mkapa alimuona Sumaye hana makundi ndani ya Chama na hiyo ndiyo sababu kubwa za kumchagua pia inawezekana alimuona Sumaye hawezi kukataa chochote kile ambacho Mkapa angeamua kifanywe anavyotaka yeye.
 
Back
Top Bottom