Sumaye akutana na waandishi wa habari; afafanua msimamo wake

Tunakosa muda wa kujielekeza katika mambo ya msingi tunaanza siasa za kupakana matope - Sumaye
 
Na bado mnamsikiliza? kweli tz waandishi wa habari hakuna ni majungu tu y don't you walk out?

angalau kesho magazeti yatgaibuka na habari tofauti. tumechoka na babari-crap za mradi wa lowawsa wa loliondo
 
Nategemea nimeeleweka, sitarajii kuibua malumbano na sitarajii kurejea kuongea na waandishi juu ya hili. Mimi ni mwana CCM na sipo chama chochote cha siasa zaidi ya hiki.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
 
Nawaomba watanzania, yeyote atakayejaribu kutumia njia za udanganyifu kwa RUSHWA, KUTENGANISHA WATU, tumkatae kwa nguvu zote

Hapa Sumaye anamaanisha nini? Ina maana ndani ya chama chake kuna watu wameshapeana rushwa kuanza kuchafuana? Mh! sisi yetu macho, vita vya Panzi Furaha ya Kunguru.
 
Anasema LENGO ni kuwajibu UVCCM, anatumia njia wanayotaka.

Anasema yeye hayupo CCM kwa maslahi yake binafsi, amekereka sana na kauli za UVCCM na inamshangaza kuona wanafumbiwa macho na ana wasiwasi na hatma ya CCM
Ok, nimekupata mkuu!!
 
FT hana jipya kumbe. Makamba alikuwepo kikao kile. Aulizwe kama anayaunga mkono maazimio ya kikao kile.
 
Nategemea nimeeleweka, sitarajii kuibua malumbano na sitarajii kurejea kuongea na waandishi juu ya hili. Mimi ni mwana CCM na sipo chama chochote cha siasa zaidi ya hiki.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika

Movie ilikuwa fupi hivyo................... Duh aturudishie pesa zetu!!!
 
Kwaheri CCM kapumzike mahala pabaya kuzimuni!! Go Freddy, ila na wewe usilete majungu ishia kwenye point tu, leo usimtaje yule aliewatuma UVCCM
 
Nategemea nimeeleweka, sitarajii kuibua malumbano na sitarajii kurejea kuongea na waandishi juu ya hili. Mimi ni mwana CCM na sipo chama chochote cha siasa zaidi ya hiki.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
Amemaliza?
 
Serikali yoyote iliyochaguliwa kidemokrasia LAZIMA itasemwa na kukebehiwa. Kiongozi yeyote na chama chochote kilichochaguliwa kidemokrasia, kitasemwa na watu watakikebehi. Si ajabu
Dah kumbe shule nzuri bwana, tangu amalize MBA yake siku hizi Sumaye anaongea point, nimeshitushwa kidogo maana nilizoea kumsikia akitoa point zilizokuwa tata sana enzi za uwaziri mkuu wake.

Hongera Sumaye
 
Sasa hivi mtu yeyote akiongea ndani ya CCM ataambiwa anautaka urais, hii inaweza kuwaziba wengi midomo

Utamaduni huu wa kuongea hivi hawakuwa nao. Na aliyejaribu kuongea hivi aliitwa Dodoma. FT akijaza fomu 2015 hili litamwandama sana na huenda asivuke ile hatua ya CC kwenda NEC.
 
Back
Top Bottom