Uchaguzi 2020 Sumaye aichokonoa CHADEMA. Asema Vyama vya Upinzani haviwezi kuongoza nchi kwa sababu hawana sera

Akafie mbali hukoooo

Ni baba mpumbavu pekee kama stone anayeweza kusifiwa kwa kumnunulia mkewe Iphone X lakini aliacha mwanae akafa kwa kukosa laki moja ya matibabu. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 8[1](a) inasema "Lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa (wananchi) WATU sio ustawi wa VITU. Asomaye na afahamu.!
 
Kama aliemteua PM miaka 10 alimtusi hadharani kuwa ni Lofa sasa sisi tusemeje ? Huruma tu zero brain huyooo
Zaidi ya yote Kama,hawana Sera alifuata Nini kwao?Na pia aliondoka bila kulazimishwa Kama amarudi aliko sema nyumbani ni vyema.Ila asitamani kurudi siku moja.
 
Kama ni zero brain, wale aliokuwanao kwenye Kamati Kuu ya Chadema unawaitaje?
Hata wewe mgeni wako, unamkaribisha kwa ukarimu Kama mwenyeji,ila matendo take yatafanya ukarimu wako kwake ubadilike ,kulingana na tabia yake.
 
Muulizeni alikuwa wapi kabla hajarudia uanachama wake wa mapinduzi?

Kutanga tanga ni dalili ya kupungukiwa imani na kutokuwa hakika mahala ulipo

Hata matarajio ya kesho hawezi kufunuliwa yeye aliye mzururaji
 
Kusema rais kachukua heka laki mbili kagera nayo ni sera? Tafuteni sera semeni chadema itafanya nini kama ikipewa mamlaka ya uongozi na sio kuongelea personals.
 
Mentally freshman ameshindwa kutengeneza legacy akiwa kwa wakati wake amebaki kurukaruka kama maharage ya Mbeya ambayo hayaivi mpaka yasuguliwe.
 
Huyu alienda upinzani kama jasusi alitumwa na kama mnakumbuka siku waliyoitwa wastaafu wote ikulu akaropoka sasa sijui alijisahau kuwa yeye kuwa upinzani ni kwa manufaa ya CCM baada ya hapo jamaa wakamshutukia ndio maana wakamdhalilisha katika uchaguzi wa Pwani wakamuacha kuingia bila mpinzani lakini akapigiwa No vote kushindwa na kivuli chake pale ikawa mzee kaumbuka vibaya sana ikawa hana budi arudi nyumbani maana ujasusi kashindwa na hataweza kupeleka info zozote kule. Chadema intelligence yao inakuwa ndani ya chama na nje miaka ya nyuma walikuwa wanaenda na hamasa tu wanabeba tu wamekuwa makini ndio maana mwaka huu tunaona wanatoa upinzani.
 
Na John Walter - Hydom, Mbulu

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Frederick Sumaye amesema vyama vya Upinzani nchini haviwezi kuongoza nchi kwa sababu hawana sera.

Ameyasema hayo Leo Septemba 30,2020 akizungumza na wananchi wa Jimbo la Mbulu Vijijini katika mkutano wa Mgombea mwenza Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kunadi Sera za Chama cha Mapinduzi katika viwanja Vya Haydom.
Sumaye amesema Chama alichotoka CHADEMA, ni Chama cha Uanaharakati na hakina sera zozote za kuwasaidia wananchi.
"CHADEMA wanafikiri kuwa nchi ya Tanzania bado ipo mikononi mwa Wakoloni, wanapiga kelele utafikiri bado tunatawaliwa" alisema Sumaye

"Nilienda kule lakini baada ya kugundua hawana chochote nikaamua kurejea nyumbani" alisisitiza Sumaye. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Manyara Simon Lulu amesema Chama hicho kinajiandaa kwa ushindi wa kishindo kwa sababu kimefanya maendeleo kwa wananchi.

Amemweleza Mgombea Mwenza kiti cha Urais Tanzania Samia Suluhu Hassan kwamba katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu, Upinzani mkoani hapo hawataambulia hata kiti cha Udiwani.

My take:
Huyu mzee atakuwa amepitwa na wakati hivi wanazotangaza CHADEMA kwenye mikutano yao siyo sera hizo? Kama yeye zero brain ukiweza kukaa ofisi ya waziri mkuu kwa miaka 10 kwa nini CHADEMA washindwe kuongoza nchi? Ndiyo maana mzee wa Lupaso alimwita "Lofa na Mpumbavu"
Kuonzwa na sumaye kwa miaka 10, nimeamini tanzania tunaweza kuongozwa na CHAUMA kwa miaka 40.
 
Back
Top Bottom