Uchaguzi 2020 Sumaye aichokonoa CHADEMA. Asema Vyama vya Upinzani haviwezi kuongoza nchi kwa sababu hawana sera

Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
8,110
2,000
Na John Walter - Hydom, Mbulu

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Frederick Sumaye amesema vyama vya Upinzani nchini haviwezi kuongoza nchi kwa sababu hawana sera.

Ameyasema hayo Leo Septemba 30,2020 akizungumza na wananchi wa Jimbo la Mbulu Vijijini katika mkutano wa Mgombea mwenza Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kunadi Sera za Chama cha Mapinduzi katika viwanja Vya Haydom.
Sumaye amesema Chama alichotoka CHADEMA, ni Chama cha Uanaharakati na hakina sera zozote za kuwasaidia wananchi.
"CHADEMA wanafikiri kuwa nchi ya Tanzania bado ipo mikononi mwa Wakoloni, wanapiga kelele utafikiri bado tunatawaliwa" alisema Sumaye

"Nilienda kule lakini baada ya kugundua hawana chochote nikaamua kurejea nyumbani" alisisitiza Sumaye. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Manyara Simon Lulu amesema Chama hicho kinajiandaa kwa ushindi wa kishindo kwa sababu kimefanya maendeleo kwa wananchi.

Amemweleza Mgombea Mwenza kiti cha Urais Tanzania Samia Suluhu Hassan kwamba katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu, Upinzani mkoani hapo hawataambulia hata kiti cha Udiwani.

My take:
Huyu mzee atakuwa amepitwa na wakati hivi wanazotangaza CHADEMA kwenye mikutano yao siyo sera hizo? Kama yeye zero brain ukiweza kukaa ofisi ya waziri mkuu kwa miaka 10 kwa nini CHADEMA washindwe kuongoza nchi? Ndiyo maana mzee wa Lupaso alimwita "Lofa na Mpumbavu"
 

Interested Observer

JF-Expert Member
Mar 27, 2006
2,132
2,000
Alikuwa waziri mkuu akiwa na Diploma ya Agro, baada ya kwenda Boston kusoma MBA akasema “baada ya kupata MBA nimeelewa mengi ambayo nilikuwa siyajui” Hawa ndiyo makapi ya CCM

we are going with Lisu - intelligent, bombastic, flamboyant, agile, young, absorbent, charismatic and inspirer!!!!!
 

Date20210317

JF-Expert Member
Nov 7, 2018
3,862
2,000
NJE YA MADA KIDOGO.

Nilimuona mtu wa ajabu kidogo (not negativelly) huyu mzee sumaye na nikafikiria sana kuhusu influence ya viongozi hawa wanapotoka madarakani.

Kitu kilichonifanya nimuone tofauti ni baada ya kifo cha mzee mkapa.Kwenye mahojiano na tv station flan, I think ni TBC, nikamskia anaongelea kupokea taarifa ya mzee Mkapa kupitia vi clip vya watsap.Halaf akaenda mbali kidogo akasema " nilivyoona ile video sikuamin, nikampigia mtu flan kumuuliza eti mzee mkpa kwel kafariki?"" Na blah blah zingine kibao.

Nikajiuliza hiv mtu mzito kama huyu aliyekua wazir mkuu wa utawala wa mkapa anakosaje info nyeti kama hiz directly on spot? Hana connection au influence kwenye system kutaarifiwa mambo ya msingi kama yale?

Anyway, sio issue ila nikamdharau kwa kuwa less informed kiasi kile na mtu kama huyu una kila sababu ya kutomuamin directly.
 

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
4,552
2,000
Mimi Sumaye hata sijamuelewa ila cha muhimu nawakumbusha bado siku 27 mpige kura na Membe bado hajaanza kampeni

EjIsClXX0AEf3ya.jpeg
 

Sir_Mimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2013
7,141
2,000
Ana tabia za kimalaya malaya....refer hotuba ya Mwalimu Nyerere miaka ya 60s,haelewi kama anataka kuolewa au alishaachika (staafu).
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom