Sumaye agoma kumchafua Dk Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sumaye agoma kumchafua Dk Slaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Oct 13, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Sumaye agoma kumchafua Slaa

  Na Ezekiel Kamwaga

  Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ameingia katika kampeni za mgombea urais wa chama chake kwa sharti la kutomchafua Dr Willbrod Slaa.

  Taarifa zilizofikia gazeti hili kutoka Moshi zinamnukuu Sumaye akisema, hatamchafua mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa vile kufanya hivyo kutamvunjia hadhi.

  Sumaye ameingia kwenye kampeni kufuatia mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete, kuwaomba msaada viongozi wastaafu wanaodaiwa “kukacha” kampeni zake.

  “Naweza kukuthibitishia pasipo shaka kwamba, Kikwete amewaangukia baadhi ya wazee wetu kumsaidia katika mikoa ambako CCM ina “hali mbaya,” ameeleza mtoa taarifa.

  Chanzo hicho cha habari kimesema awali ilionekana Kikwete angeweza kushinda bila msaada wa wastaafu, lakini sasa ameona upepo umegeuka.

  Taarifa zinasema Kikwete alimwomba Sumaye kumsaidia hasa katika mikoa ya kanda ya Kaskazini ambako imeelezwa kuna upinzani mkubwa.

  “Awali, Sumaye alisita kukubali ombi hilo la rais, lakini baadayeakakubali kwa kutoa masharti ya mahala hasa anapoweza kwenda,” kimeeleza chanzo chetu cha habari.

  Hata hivyo, alimwambia kikwete kwamba atakwenda tu katika maeneo ambayo anadhani anaweza kuroa msaada mzuri,” kimeeleza chanzo hicho.

  Ofisa mmoja wa ofisi ndogo ya makao makuu, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam ameliambia gazeti hili kuwa awali Sumaye alielekezwa kwenda majimbo ya Moshi Mjini, Hai, Rombo, Moshi Vijijini na Vunjo.

  MwanaHALISI lina taarifa kuwa Sumaye amekataa kufanya kampeni katika majimbo hayo, kwa maelezo kwamba anaamini wagombea ubunge wa Chadema huko “hawana matatizo.”

  Haikufafanuliwa iwapo kwa “hawana matatizo” Sumaye alikuwa na maana ya kusema hawashikiki au wana uwezo wa kuwakilisha majimbo yao…………..

  ……..Kuna taarifa kwama ilibidi Sumaye awasiliane na Kikwete moja kwa moja kumweleza uamuzi wake huo. Imeripotiwa kuwa Kikwete amekubalkiana naye.

  Taarifa zilizopatikana juzi Jumatatau zimesema Sumaye amekubali kufanya kampeni katika majimbo ya Vunjo na Hanang.

  Aidha, imefahamika kuwa Sumaye amekubali kuingia katika kampeni kwa sharti la kutoshiriki katika kumkashifu mgombea wa urais wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, jambo ambalo amenukuliwa akisema linaweza kumuondolea hadhi.

  Taarifa zaidi zinasema Sumaye amegoma kumfanyia kampeni mgombea ubunge wa jimbo la Rombo kupitia CCM, Basil Mramba, kwa vile ana wasiwasi ataonekana ni mtetetezi wa watuhumiwa wa ufisadi na anaweza kuanza kuandamwa baadaye…….

  Habari zaidi katika MwanaHALISI ya leo.
   
 2. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,508
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Si Makamba alishasema kuwa JK anapendwa zaidi ya CCM, sasa msaada wa nini tena???
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nimejaribu sana kutafuta na kupata tuhuma za ufisadi za huyu Bwana, lakini sijafanikiwa. Hakuguswa na kashfa ya EPA, Meremeta, Twin Toweres, Deep Green etc -- inakuwaje? Inaonekana ni msafi ama sivyo saa hizi angekuwa anaogelea katika dimbwi la tuhuma.

  Hata mwaka 2005 alipojaribu kugombea urais, sikusikia kashfa yoyote ya ufisadi dhidi yake.

  Naamini ni kiongozi safi, na ndiyo maana hataki kumkashifu mtu msafi (Slaa) na kumtetea mtu mchafu (Mramba).
   
 4. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Muda wa kuomba msaada na kusaidiana umekwisha tusubiri tuone ni nini watanzania wataamua
   
 5. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Ukiona paka kakubali kulala chali....
   
 6. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Sumaye kama hataki kutetea ufisadi kule Rombo, basi afanye kampeni kwa ajili ya Dr. Slaa.
   
 7. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Sumaye hakutakiwa kuomba msaada, hadi Kikwete na wanamtandao woote wamwombe radhi kwa kumchafua.......
   
 8. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  CCM ndio limekwishameguka hivyo!
   
 9. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Sumaye ana akili sasa baada ya kutoka Harvard
   
 10. u

  urasa JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sumaye mzee wangu,kipi bora kwako?tz au ccm?fanya maamuzi magumu
   
 11. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Wanapoteza muda tu. Sumaye anaushawishi gani? Mkapa akitokea tu watu watapiga yowe. Ruksa ndo amekwisha kwani kila kitu kwake ni mzaa. Wangekuwa ni wanachama wa ccm ndo wanaoamua hatima ya tanzania ingewezekana kubadili upepo lakini hadi sasa decide group iko kwa slaa. nani hamtambui slaa, hata ccm wenyewe naimani slaa anaweza kuondoka na 30% ya vote zao.

  TUMESEMWA SANA TUMETUKANA SANA NA MANENO YA TAARABU TOKA KWA JK SAA YAKE YA KUBWABWAJA IMEFIKIA UKINGO. kwani wako wapi akini ridhiwani na wengine alowaamini zaidi?
   
 12. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Umeniwahi nilitaka kusema hivyo hivyo.
   
 13. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hukusikia wakati JK alitumia magazeti kama kawida yake kumchafua yeye pamoja na Dk Salim, hata hivyo tuhuma haziwa nzito kwani alikuja akatoa tamko kwamba atakae andika tuhuma za uongo zidi yake na kushindwa kuzibitisha atampeleka mahakamani na kumdai fidia ya Bil 1, tangu hapo sikusikia tena magazeti ya JK kuandika tuhuma hizo na inasemekana alikuwa na kinyongo sana na serikali ya JK lakini kwakuwa siasa sazingine ni unafiki siajabu kweli kuanza kumkampenia JK.....Alikuwa akidaiwa anaakaunti nje ya nchi yenye pesa zaidi ya bil 3.....ngoja watu wenye data zake watakuja kuzimwanga
   
 14. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Safi sana!Unaona elimu inavyoweza kumbadisha mtu!jamaa sasa yuko juu,anajua madhara ya siasa za maji taka,kwa sasa ni mtu makini kupita maelezo!
   
 15. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ujue Kilio kinafata....
   
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  Huko Vunjo ni kwa mashemeji au kuna nini? Tunajua Hanang ni nyumbani ambako Dr. Slaa atalamba kura zote na hata Sumaye anawajua wa-Irak wenzie jinsi walivyo na msimamo.
   
 17. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  walikuwa wamemweka kando labda kaahidiwa sehemu nyeti aachane na ufugaji ili kumaliza so lake na JK
   
 18. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #18
  Oct 14, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Na ya kwake yaja. Kila mtu ataumbuka kwa kombola lake, hakuna kujichagulia. Kama Sumaye anategemea kombola lake kuwa kwenye mashamba, asubiri akishaanza kampeni ndo watampa vitu vyake.
   
 19. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #19
  Oct 14, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  mbona nilikwisha sikia alilazimishwa akopeshwe pesa toka PPF ili hali yy si mwanachama na akakopeshwa milion 500! kwani km ni kweli si kashfa hiyo!?
   
 20. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #20
  Oct 14, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Juzi juzi nilisikia watu wakisema Sumaye aliwashauri wazee wa Hanang kuwa mwaka huu hakuna kukosea tena, akiwaambia wamchague Dr Slaa. Alifanya hivyo kwa siri.
   
Loading...