Sumaye afunguka suala la familia yake kunyang'anywa mashamba mawili!

Tumeacha mambo ya msingi aliyosema na kumsakama mtu. Ameeleza hatua kwa hatua ya kilichotokea na pia suala la utawala bora. Hatugusi issues zilizomo tuna attack personalities what kind of people! Ule msemo wa kifalsafa unaosema simple minds zinadiscuss watu unadhihiri. I am Sorry!
Kuna wengi wamekutwa na makubwa hawasemi na orodha inaongezeka ninajua marafiki zangu walioUmia kupitia huu mtindo tunaoendelea nao na kuushabikia. MUNGU ATUNUSURU
Usishangae, tangu awamu hii imeanza kumekuwepo na ongezeko kubwa sana la kiwango cha ujinga. Ukisoma kwa utulivu press release ya Sumaye, unaweza kubaini kuwa nchi hii sasa inaongozwa kwa chuki kubwa sana. Na ukweli ni kwamba taifa hili linaandaliwa kuingia katika machafuko huku wajinga wakishangilia!
 
Mie nimeona hata yeye bwana lukuvi angeweza kuwa magerezani.........Nahisi kunaharufu ya damu sehemu.
 
Jamani. ninaomba mnivumilie, maana nimesoma hotuba yote neno kwa neno ya Ndugu yetu Mtanzania mwenzetu ambaye aliwahi kututumikia sisi wananchi watanzania katika nafasi ya Uwaziri Mkuu kwa kipindi cha Miaka kumi mfululizo na miaka tisa kama naibu waziri. Huyu si mwingine bali ni Mh. Sumaye.

Nampongeza sana kwa hatua yake ya kutoka hadharani kusema yaliyo moyoni juu ya kile kinachoendelea kuhusu umiliki wa baadhi ya mali za familia. Pamoja napongezi hizo, ningependa kuhoji baadhi ya mambo na kutoa dukuduku zangu kuhusu hoja zake kwa mstakabali wa nchi yetu. Mimi kama raia wa kawaida ningependa kupata ufafanuzi kutoka ama kwake ama yeyote ambaye ameisoma hotuba yote na kuielewa vyema. Ni kwa nia njema kabisa ya ustawi wa taifa letu, kuhoji kwangu ama dukuduku zangu zisitafsiriwe vinginevyo.
Hoja na dukuduku nitaziweka chini ya nukuu. Karibu.
---------------------
Mnamo Machi 1996 kampuni ya Wami & Magole Farmers
Cooperative
Society Limited ilibadirisha jina na kuitwa Morogoro Farmers Primary Society Limited. Aidha, tarehe 27 November, 2001 Morogoro Farmers Primary Society Limited walimuulizia ndugu Esther Sumaye shamba hilo na baada ya kukamilisha taratibu zote za kisheria ikiwa ni pamoja na kulipa ushuru kwa Serikali uhamishaji wa miliki (Transfer) ulikamilishwa mwaka 2002 kwa mujibu wa kifungu cha 61 cha Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1996.
Muda mchache baada ya kuwa waziri mkuu (1996) inabadili jina. Baadaye kampuni inashindwa kulipa deni (swali: ilikuwa idaiwa na nani na kiasi gani nini kilisababisha kushindwa kulipa deni?) na miaka mitano baadaye kampuni inamuuzia Mama Esther shamba kwa njia ya dhabuni (wadhabuni wengine walikuwa akina nani na walitoa offer ya kiasi gani?). Inatia dukuduku kidogo, maana Mama alimilikishwa shamba hilo mwaka 2002 kwa sheria ya Ardhi iliyoboreshwa mwaka 1996 mwaka mmoja ukiwa waziri mkuu (ningependa kujua ni vipengele gani vilibadilishwa kwenye sheria hiyo ya awali).

Hali ya shamba la mama Esther Sumaye haijabadilika kati ya mwaka 2012 na mwaka 2017 na labda imekuwa nzuri zaidi.
Hapa mheshimiwa umenichanganya (consistency ni muhimu); shamba limeboreshwa ama bado halijaboreshwa?

Aidha kwa kesi ya wakina Halima Mdee na Esther Bulaya nilimsikia Mheshimiwa Spika Job Ndugai akiongea kwa hasira sana na kusema waende kokote wanakotaka kwenda lakini mwaka mzima hakanyagi mtu hapa! Inawezekana taratibu za Bunge sasa zimebadilika, lakini nijuavyo mimi spika ni kiongozi wa Bunge na maagizo anayoyatoa ni maamuzi ya Bunge na siyo yake.
Mheshimiwa unashindwa hata neno moja la kukemea lugha za kuudhi za akina Halima kwenye chombo muhimu kwenye masuala ya nchi yetu kiutawala? Hapa pia umenichanganya. Yawezekana taratibu hazikufuatwa kwa namna walivyoadhibiwa lakini kitendo cha kutotoa onyo hadharani kwa Halima kinatupa wasiwasi kuwa uwenda uwajengi vizuri vijana hawa kuwa watumishi muhimu na wanoheshima nchini. Hata BAK kabadilika sana, anatumia lugha za kuudhi mara nyingi .Natafakari!
Nataka tu nitahadharishe kuwa tukianza kujenga visasi hakuna atakayepona au kama atapona basi inabidi aikimbie nchi mara tu baada ya kipindi chake cha uongozi.
Vitisho hivi kwa utawala, si sahihi. Kauli yako hii inaweza kutafisiriwa kama tishio wa watendaji wa serikali, mahakama, na hata bunge kufanya kazi zao kwa ufanisi (unataka kuwaogopesha, hili halikubaliki). Acha wafanye kazi zao. Kauli inaachochea antagonism badala ya suluhu. Ifikirie tena kauli yako, Mheshimiwa.
CCM imeshavuka hatua hiyo na watu wameichoka hivyo ni vema kujenga uwezo wa chama kingine ili kishike dola badala ya CCM vinginevyo nchi nchi inaweza kuingia katika hali mbaya ya usalama
Kauli hii si rafiki hata kidogo, tena ukizingatia kilichokuwa kinaendelea huko Wilayani Rufiji. Viongozi wa CCM waliuawa. Chuja kauli zako maana waweza leta sintofahamu isiyokusudiwa, Mheshimiwa. Ama toa maelezo ya kutosha juu ya hili.
Katika mfumo sahihi wa demokrasia ya vyama vingi chama kimoja hakitakiwi kikae madarakani zaidi ya miaka kumi mfululizo na ikizidi sana kumi na mitano lakini siyo miaka hamsini au sitini kama inavyokuwa kwa CCM. Ukiona chama kinakaa zaidi ya miaka ishirini madarakani ujue hapo mfumo wa vyama vingi ni wa jina tu
Mkuu ili la demokrasia ya vyama kukaa miaka kumi umelijua ulipoingia Chadema? Naamini ulilijua mapema. Sasa wakati tunaanda katiba mpya mbona hukutoa maoni yako juu ya kuweka ukomo wa vyama vya siasa kutawala miaka kumi tu. Hivi unadhani Chadema, ambayo wewe ni mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, wako tayari kuendesha nchi kwa miaka kumi ama kumi na tano tu!? Ebu tufafanulie hili vizuri, Mheshimiwa.
Ingekuwa serikali haiuogopi upinzani ingeendelea kusinzia kama kawaida yake. Na kama serikali isingeubana upinzani kuanzia bungeni hadi kwenye mikutano ya hadhara nina uhakika kasi ya maendeleo yetu ingeongezeka sana
Unaamini kweli maneno yako haya...ebu chukulia hili la Lissu kutaka watanzania tutengwe na jumuiya za kimataifa kiuchumi, kisiasa na kidiplomasia!! Wangeruhusiwa hawa waongee holela kwenye maeneo ambayo hawajulikani(hawawakilishi), si wangepopolewa mawe tu! Uoni kama rais alitoa wazo zuri la kuhakikisha kila mtu anafanya siasa kwenye jimbo lake ili aje apimwe vizuri ifikapo 2020 asije akaleta visingizo vya nilikuwa nafanya ziara za kichama!? Unalionaje hilo, Mheshimiwa.

Ajue kuwa kama sisi wengine tungekuwa na roho mbaya na dharau kama yeye, wengine wao, ikiwa ni pamoja na yeye, wasingekuwa hapo walipo leo na pengine wangekuwa hata magerezani.
Hapa mheshimiwa, umeharibu kabisa. Yaani kumbe kwenye kipindi cha utawala wenu, kuna baadhi mlikuwa mnawaacha wanafanya mambo yasiyofaa bila hata kuwachukulia hatua?! Sasa hapa Chadema unawapa courage gani katika masuala ya kusimamia sheria!?
======
Kumradhi tena kwa maelezo mareefu. Nasubiri tafakuri yenu.
 
Sumaye mjanja; typical Chadema. Ni wao waliofaidika utawala wa CCM; Watanzania wengine wakaachwa nyuma. Sasa Waziri Mkuu na Rais wametoka kwenye maeneo yaliyoachwa, kiba Sumaye wanawadharau. Waliokuwa wamefaidika wanaikimbia CCM ili wazidi kula pato la taifa kivyao. Mwuluzeni Sumaye: kwa nini alitoja CCM? Kuba nini CCM haikufanya wajati kwa miaka 10 alikuwa Kiongozi wa juu kabisa? Anataka madaraka gani ambayo hakuwa nayo ili awasaidie Watanzania? Anataka madaraja amsaidie nani hasa? Amechoka, ametumikia umma kwa miaka 10. Ana pensheni nzuri ya serkali. Ana majumba ana mashamba. Anataka nini zaidi Chadema kuubgana na kina Tundulussu kuifitinisha nchi yake? Aliuwa watu 55 wa CUF mwaka 1995 akiwa Waziri Mkuu, akikaimu Raus BWK akiumwa. Akaingiza mbwa Msikitini mwembechai. Watanzania wakamsamehe kuwa ni kazi ya uongozi. Leo ansema CCN dhalimu, yeye hakuwa dhalimu Pemba? Hayo ni tisa: la kumi ni jwamba je, Sumaye aliyapataje mashamba nchi nzima? Kwa nini akamsukumia mkewe? Uchoyo, ubinafsi, ulafi, ukabila. Apuuzwe!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sumaye anapaswa awashauri wanafamilia wake walionyang'anywa mashamba na serikali waende mahakamani. Kuwaita waandishi wa habari sidhani kama itasaidia sana. Hata hivyo, inavyoonekana mashamba hayo ni yake na si ya wanafamilia wake. Kimsingi sioni sababu ya yeye kulalamika, aende mahakamani akakate rufaa kama kweli hayo mashamba anayamiliki kihalali
 
"Wakati wa kampeni, baadhi ya viongozi wa CCM walidiriki kusema huyu Sumaye dawa yake ni kumfilisi kwa kuchukua mashamba. Kunyang'anywa mashamba yangu na ya familia tuliyonunua kihalali ni visasi dhidi yangu baada ya Mimi kuhama CCM".

Hayo maneno yamesemwa na Waziri Mkuu wa zamani Frederick Sumaye wakati akiongea na waandishi wa habari.

Maneno ya Sumaye ni sawa na mfa maji asiyeacha kutapatapa kwa kutafuta huruma kwa Wananchi ya kutaka kusamehewa arudishiwe mashamba aliyoshindwa kuyaendeleza na hivyo Serikali kuyarudisha mikononi mwake kwa matumizi mengine.

Sumaye analalamika kutwa akiwa anasahau kuna sheria inayotaka mashamba yaendelezwe vinginevyo yatanyang'anywa. Ni ajabu kuilalamikia sheria ambayo yeye alishiriki kuitunga. Ama anataka kusema ukiwa Waziri Mkuu ni kigezo cha kuwa juu ya sheria?

Sumaye ameenda mbali, anatumia kigezo cha kufanyiwa kisasi cha kuhama CCM ndio maana anachukuliwa mashamba yake na ya familia yake. Anasahau wapo hata Wabunge na viongozi ndani ya CCM wamechukuliwa mashamba yao. Mfano ni Mbunge wa Morogoro Mjini (CCM) Mohammed Aboud ambaye naye amechukuliwa shamba lake.

Hakuna sababu ya kuona anafanyiwa visasi wakati kuna sheria; hana sababu ya kuona anaonewa kwa kuhama CCM wakati Vigogo waliopo CCM nao pia wanachuliwa mashamba yao wasiyoyaendeleza.

Sumaye anapaswa kuelewa kila siku Wakulima na wafugaji wanapigana kutokana na kugombea ardhi ambayo Sumaye na wenzake wameitamia pasipo kuiendeleza.

Watu wanakosa maeneo ya kufanya shughuli za kilimo, ufugaji, uwekezaji wa viwanda, makazi kutokana na baadhi ya Watu wachache kujimilikisha Ardhi Kubwa. Huku ni kukosa uzalendo na huruma kwa Watu wengine na Taifa.

Sumaye aache kutapatapa, aelewe sheria ni msumeno haiangalii sura ya Mtu, dini, cheo, hadhi, kabila wala rangi ya mtu.

Shilatu E.J

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole Fredrick Sumaye!

2017 umeporwa ulichopora 2002

2012 Waziri wa Ardhi alitetea 'Uhalali' wa Shamba lako la Mvomero Bungeni kwa kuwa alipewa Maelekezo na Jk kuwa asikupore sio kuwa ulikuwa na Uhalali

Jk Mzungu wa Roho hakuwa na Muda wa kufuatilia Mali za Mtu hata uwe Adui yake vipi Mie nakumbuka tulikuwa tunafanya Semina za TASAF ( Mfuko wa maendeleo wa Rais) kwny Hotel za Freeman Mbowe japo Mbowe alikuwa Mmoja wa Viongozi wa Genge la Kumhujumu Jk!

Huyu JPM ndie 'Mwefrika' halisi lazima awasimamie kwa kucha
 
Kama umesoma vizuri ni kuwa kesi iko mahakamani na zuio lishatolewa issipokuwa muhimili mmoja ushaamua
 
"Wakati wa kampeni, baadhi ya viongozi wa CCM walidiriki kusema huyu Sumaye dawa yake ni kumfilisi kwa kuchukua mashamba. Kunyang'anywa mashamba yangu na ya familia tuliyonunua kihalali ni visasi dhidi yangu baada ya Mimi kuhama CCM".

Hayo maneno yamesemwa na Waziri Mkuu wa zamani Frederick Sumaye wakati akiongea na waandishi wa habari.

Maneno ya Sumaye ni sawa na mfa maji asiyeacha kutapatapa kwa kutafuta huruma kwa Wananchi ya kutaka kusamehewa arudishiwe mashamba aliyoshindwa kuyaendeleza na hivyo Serikali kuyarudisha mikononi mwake kwa matumizi mengine.

Sumaye analalamika kutwa akiwa anasahau kuna sheria inayotaka mashamba yaendelezwe vinginevyo yatanyang'anywa. Ni ajabu kuilalamikia sheria ambayo yeye alishiriki kuitunga. Ama anataka kusema ukiwa Waziri Mkuu ni kigezo cha kuwa juu ya sheria?

Sumaye ameenda mbali, anatumia kigezo cha kufanyiwa kisasi cha kuhama CCM ndio maana anachukuliwa mashamba yake na ya familia yake. Anasahau wapo hata Wabunge na viongozi ndani ya CCM wamechukuliwa mashamba yao. Mfano ni Mbunge wa Morogoro Mjini (CCM) Mohammed Aboud ambaye naye amechukuliwa shamba lake.

Hakuna sababu ya kuona anafanyiwa visasi wakati kuna sheria; hana sababu ya kuona anaonewa kwa kuhama CCM wakati Vigogo waliopo CCM nao pia wanachuliwa mashamba yao wasiyoyaendeleza.

Sumaye anapaswa kuelewa kila siku Wakulima na wafugaji wanapigana kutokana na kugombea ardhi ambayo Sumaye na wenzake wameitamia pasipo kuiendeleza.

Watu wanakosa maeneo ya kufanya shughuli za kilimo, ufugaji, uwekezaji wa viwanda, makazi kutokana na baadhi ya Watu wachache kujimilikisha Ardhi Kubwa. Huku ni kukosa uzalendo na huruma kwa Watu wengine na Taifa.

Sumaye aache kutapatapa, aelewe sheria ni msumeno haiangalii sura ya Mtu, dini, cheo, hadhi, kabila wala rangi ya mtu.

Shilatu E.J

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni huyu huyu aliwahi nukuliwa akisema ukitaka mambo yakunyookee jiunge na CCM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sumaye mbinafsi sana , Mwabwepande aliacha mapori mpk watu wakafanya uharifu yy alikuwa wapi kwanini asiishi kwenye mashamba yake ? Huyu mwizi kama wengine walipora maeneo kwa sababu ya cheo chake sasa kaingia kiongozi mzalendo ngoja waisome namba watalimia meno
 
"Wakati wa kampeni, baadhi ya viongozi wa CCM walidiriki kusema huyu Sumaye dawa yake ni kumfilisi kwa kuchukua mashamba. Kunyang'anywa mashamba yangu na ya familia tuliyonunua kihalali ni visasi dhidi yangu baada ya Mimi kuhama CCM".

Hayo maneno yamesemwa na Waziri Mkuu wa zamani Frederick Sumaye wakati akiongea na waandishi wa habari.

Maneno ya Sumaye ni sawa na mfa maji asiyeacha kutapatapa kwa kutafuta huruma kwa Wananchi ya kutaka kusamehewa arudishiwe mashamba aliyoshindwa kuyaendeleza na hivyo Serikali kuyarudisha mikononi mwake kwa matumizi mengine.

Sumaye analalamika kutwa akiwa anasahau kuna sheria inayotaka mashamba yaendelezwe vinginevyo yatanyang'anywa. Ni ajabu kuilalamikia sheria ambayo yeye alishiriki kuitunga. Ama anataka kusema ukiwa Waziri Mkuu ni kigezo cha kuwa juu ya sheria?

Sumaye ameenda mbali, anatumia kigezo cha kufanyiwa kisasi cha kuhama CCM ndio maana anachukuliwa mashamba yake na ya familia yake. Anasahau wapo hata Wabunge na viongozi ndani ya CCM wamechukuliwa mashamba yao. Mfano ni Mbunge wa Morogoro Mjini (CCM) Mohammed Aboud ambaye naye amechukuliwa shamba lake.

Hakuna sababu ya kuona anafanyiwa visasi wakati kuna sheria; hana sababu ya kuona anaonewa kwa kuhama CCM wakati Vigogo waliopo CCM nao pia wanachuliwa mashamba yao wasiyoyaendeleza.

Sumaye anapaswa kuelewa kila siku Wakulima na wafugaji wanapigana kutokana na kugombea ardhi ambayo Sumaye na wenzake wameitamia pasipo kuiendeleza.

Watu wanakosa maeneo ya kufanya shughuli za kilimo, ufugaji, uwekezaji wa viwanda, makazi kutokana na baadhi ya Watu wachache kujimilikisha Ardhi Kubwa. Huku ni kukosa uzalendo na huruma kwa Watu wengine na Taifa.

Sumaye aache kutapatapa, aelewe sheria ni msumeno haiangalii sura ya Mtu, dini, cheo, hadhi, kabila wala rangi ya mtu.

Shilatu E.J

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa shilatu,je na mahakama nayo iliamua nini kihusu mashamba ya sumaye?au serikali iko juu ya sheria

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukitaka mambo yakunyokee njoo ccm. Alitamka maneno hayo mzee Sumaye akiwa waziri mkuu akiwaambia wafanyabiashara. Kwa hiyo kinyume chake Ukitaka mambo yakupindie hama ccm. Mimi nadhani Mh. Sumaye alihama akijua hayo. Nashauri atulie tu mfumo aliouacha ndiyo unaoendelea .Miaka kumi ya uwaziri mkuu usijue madhara ya mfumo uliouenzi na unafanikisha zaidi uliyoyaacha. Mbona mitaani wapo wafanyabiashara waliofiliska kwa kuunga upinzani na wakati huo yeye ni PM. Au in mkuki kwa nguruwe sasa uefika kwa binadamu. Nilidhani alijiandaa kuumia kidogo au sana kwa maamuzi take sasa kelele mapema.? Je wakigusa pensheni zake na marupurupu ya u PM atasemaje? Hivi afanye reference huko Malaysia kuna waziri mkuu mstaafu alizushiwa kesi ya kubaka ili asigombee urais upande Wa upinzani. Sasa Luna mawili ama asiseme aliyatarajia nawanyonge anaowaeleza hawatamsaidia maana hats yeye aliumiza baadhi kwa kutumika mfumo au aendelee kusema lakini ajue hata zaidi ya hayo yatampata. Dunia ya tatu ndio hatua tuliyopo. Democracy ya vyama Vinci kwetu ni foreign body na kwa mwili (mfumo) lazima ureject foreign body. Nyerere alisafiri mpaka gereza alimofungwa mzee Kaunda akala naye jela akamuombea chiluba amtoe na akamshauri aache siasa. Nyerere alijua siasa za dunia .the winner takes all even your survival is in his hands. Mimi nadhani raid anatekeleza utamaduni alioukuta sasa waliouasisi wasishangae sisi wadogo tunaujua ndiyo maana tunakaa kimya. Waelewa wakidai katiba mpya walioko madarakani wanang'aka , sasa ikiwaminya wanapotoka madarakani ndyo wajue wanyonge tunaishije huku chini. Mbona bado sana kwa yeye kujiunga na upinzani bado mfumo unamkuna haujaanza kumchuna ngozi. Mzee pole nakuombea maisha mema maana sipendi binadamu mwenzangu akiumia . maana maandishi matakatifu yanasema furahini na ndugu zenu wanapofurahi pia huzunikeni na ndugu zenu wanapohuzunika. Kinyume chake ni watu Wa shetani .Narudia tena POLE SANA. KARIBU URAIANI . NI NCHI YETU TUNAIPENDA NA NI VOINGOZI WETU TUNAWAPENDA .JAMII HUPATA VIONGOZI AMBAO NI STAHILI YAO WALA SI KWA BAHATI MBAYA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfa maji siku zote haachi kutapatapa, atashika hata jani alimradi limuokoe.

Saa tano asubuhi hii kada wa CHADEMA Fredrick Sumaye anaongea na waandishi wa habari kutafuta huruma kwa wananchi ili kulalamika na hivyo kutaka asamehewe na kurudishiwa mashamba aliyopora miaka ya nyuma na kushindwa kuyaendeleza na hivyo serikali kuyarudisha mikononi mwake kwa matumizi mengine. Sumaye analalamika kwa waandishi wa habari akiwa amesahau sheria inayomtaka aendeleze shamba alilopewa ndani ya miaka mitatu vinginevyo ananyang'anywa na pia anasahau kuwa sheria haitaki blabla bali nyaraka.

Kama haitoshi sio Sumaye pekee aliyenyang'anywa shamba bali hata wabunge na vigogo ndani ya CCM mfano mbunge wa morogoro mjini ( CCM ) Mohamed Aboud, na hata wasio kuwa na vyama. Hivi Sumaye ni nani hadi aogopwe na sheria? Kuwa waziri mkuu mstaafu ni kuwa juu ya sheria?
Sumaye acha kutapatapa. Fanya kazi.

=====



PRESS CONFERENCE AUGUST 2017

UFAFANUZI JUU YA RAIS KUCHUKUA MASHAMBA YA MABWEPANDE NA MVOMERO YA WANAFAMILIA YANGU NA MENGINE YANAYOHUSIANA NAYO

Frederick T. Sumaye

Chadema Zonal Office, Dar es Salaam Tarehe 22 Agosti, 2012.

Ndugu wanahabari,

Ndugu zangu wanahabari nawashukuru sana kwa kuitikia wito wangu japo ni kwa taarifa ya muda mfupi sana.
Utangulizi
Leo nimewaiteni hapa kwa ajili ya kuzungumzia au kutolea ufafanuzi haya yaliyotokea kuhusu Mhe. Rais kuchukua mashamba ya wanafamilia yangu na nikiihusisha na hali ya siasa ilivyo tangu awamu ya tano iingie madarakani hadi sasa hasa kuhusiana na haki za raia. Vyombo vingi vya habari vimeripoti kuwa Rais ametwaa mashamba mawili yanayohusiana na mimi au familia yangu; moja likiwa eneo la Mabwepande wilaya ya Kinondoni lenye ukubwa wa ekari 33 na lina hatimiliki na lingine likiwa wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro lenye ukubwa wa ekari 326 nalo pia lina hatimiliki. Shamba la Mabwepande linamilikiwa na mwanangu aitwaye Franklin na la Mvomero linamilikiwa na mke wangu mama Esther Sumaye.
Historia fupi
Ili kupata mtiririko mzuri wa mambo haya ya familia yangu kunyang’anywa mashamba na bila shaka na mali zingine, ni vizuri kupata historia kuanzia nyuma kidogo. Kama mjuavyo mimi nimekuwa kiongozi wa muda mrefu katika nchi hii; nimekuwa Mbunge wa jimbo kwa awamu nne (miaka 20) na kati ya hizo awamu mbili nilipita bila kupingwa. Katika kipindi hicho nimekuwa naibu waziri na waziri kwa karibu miaka 9 na waziri mkuu kwa miaka 10 yaani awamu mbili mfululizo. Nimeacha ubunge kwa hiari yangu mwenyewe mwaka 2005 na hivyo sikuwa tena serikalini tangu mwaka huo wa 2005. Katika kipindi cha awamu ya nne nikiwa ccm sijawahi kuwa na mgogoro wowote na serikali.

Migogoro yangu na serikali ilianza mara tu baada ya mimi kutoka CCM na kujiunga na UPINZANI mwezi wa nane mwaka 2015. Nilipotoka ccm niliita press conference na nilieleza wazi kwanini natoka ccm na nilitamka wazi kuwa natoka ccm kwa manufaa ya nchi na ccm yenyewe. Wakati natoka ccm mimi nilikuwa mwanachama wa kawaida asiyekuwa na cheo chochote hata sikuwa mjumbe wa kamati yoyote au

mwakilishi wa aina yoyote katika chama. Sikuwa hata mjumbe wa mkutano mkuu wa kata. Kilichonishangaza ni kuwa kutoka kwangu CCM kulinizushia uadui wa ajabu na wenzangu wengine hasa viongozi wa CCM. Itakumbukwa kuwa ni maneno mengi yasiyopendeza yalisemwa juu yetu sisi tuliokihama Chama cha Mapinduzi. Wengi nadhani hawakukumbuka kuwa vyama vya upinzani ni vyama halali kama ccm ilivyo na kukihama chama cha mapinduzi siyo uhaini.

Wako baadhi ya viongozi wa CCM walidiriki hata kusema hadharani kwenye mikutano ya kampeni kuwa “Huyu Sumaye dawa yake ni kumfilisi kwa kumnyang’anya mashamba.” Hayo yalisemwa wazi na yaliandikwa katika baadhi ya magazeti, ninyi hapa ni mashahidi, yalitamkwa hadharani na baadhi ya viongozi wa CCM Morogoro na Dar es Salaam. Mimi pamoja na baadhi ya watu tulichukulia kuwa hayo ni maneno ya kampeni na hatukutaka kuyatilia maanani, lakini kumbe hayakuwa maneno ya kampeni bali ni ya kweli.

Aidha niliweke tu wazi kuwa mimi binafsi tangu migogoro hii ilipoanza sikutaka kuyazungumza mambo haya katika vyombo vya habari na badala yake nilipenda kutumia njia za mazungumzo zaidi. Mwezi wa kumi mwanzoni mwaka 2016 nilikwenda kuonana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi, kumwelezea matatizo tunayokabiliana nayo kuhusu mashamba yetu kutishiwa kunyang’anywa na kuwa sababu zinazoelezwa hazina uhusiano na kutokuendelezwa. Nilimwambia sitaki kulumbana na serikali kwenye vyombo vya habari kwa sababu niliamini busara itachukua nafasi yake.

Baada ya hapo nilionana pia na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr. Steven Kabwe na kumweleza hayo ya shamba la mama la Mvomero na kwamba shamba hilo linatumika kikamilifu. Aidha nilimwambia kuwa katika tathmini ya awali ya mashamba pori, shamba hilo halikuwa katika orodha lakini ameagizwa kutoka juu kuwa shamba hilo liwemo katika orodha ya mashamba pori. Akanibishia lakini nilijua ujumbe umefika. Nilimwambia mkitaka kulichukua hilo shamba labda mtumie nguvu lakini kisheria hamtaweza, na kweli ndicho kilichofanyika. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nilimwambia acheni kulipa visasi vya kisiasa kwa sababu mkivianzisha hata ninyi hamtakuwa salama. Kwa bahati mbaya tahadhari nilizowapa naona zimeangukia kwenye masikio yasiyosikia.

Tarehe 27 Oktoba, 2016 Mhe. Lukuvi aliongea na vyombo vya habari kuhusu shamba la Mabwepande kwa kejeli kubwa sana dhidi yangu bila punje ya heshima kwangu. Nilitaka kumjibu hadharani lakini busara ikanielekeza nitumie njia ya kwenda mahakamani ili kuzuia dhamira ya serikali ya kuchukua shamba. Kwa hiyo tulifungua kesi tatu, mbili kwa shamba la Mabwepande, kesi moja dhidi ya wavamizi na nyingine dhidi ya serikali izuiwe na mahakama kutekeleza uonevu wake hadi kesi ya msingi itakapoamuliwa; na kesi nyingine moja kwa shamba la Mvomero kupinga dhamira ya serikali ya kutaka kufuta hati ya shamba hilo. Kwa mashamba yote mahakama kuu imetoa zuio la mashamba hayo kutokuingiliwa na serikali hadi hapo shauri za msingi zitakapoamuliwa na mahakama. Kwa kutumia utawala wa sheria

wanaoujua Rais Magufuli na waziri wake Lukuvi, wamekwishachukua mashamba hayo bila hata kujali kama kuna kesi na amri za mahakama dhidi ya hatua yao hiyo.

Wiki iliyopita nadhani tarehe 14 Agosti Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi alizungumza na vyombo vya habari Morogoro akijaribu kuhalalisha kitendo ambacho serikali imekifanya ya kunyang’anya mashamba 14 mkoani humo likiwemo la mama Esther Sumaye. Sina utetezi kwa mashamba mengine lakini nitayazungumzia mashamba yanayoihusu familia yangu, shamba la Mabwepande na shamba la Mvomero. Nataka nirudie kuwa sikutaka kulumbana na serikali kwa njia hii lakini kwa sababu wao ndiyo wanaolianzisha kila mara, safari hii nimeona sina budi na mimi nitumie vyombo vya habari ili Watanzania wajue ukweli katika sakata hili la mashamba ya ‘Sumaye’ na ikiwezekana dunia ijue kinachoendelea Tanzania.

Aidha busara niliyokuwa naisubiria itumike kumaliza jambo hili naona imeshindikana na njia za haki za kikatiba nazo zimeingiliwa kwa kutumia mabavu ya dola hivyo nimebakiwa na hili la angalau kuwafanya watanzania wajue ukweli na kumwachia Mungu atuamulie maana yeye ndiye mwenye kujua ukweli na kutenda haki.
Shamba la Mabwepande, wilaya ya Kinondoni, ekari 33
Shamba hili lilinunuliwa na mtoto wetu Franklin kwa niaba ya familia yetu kutoka mtu binafsi, Mzee Abdallah Kimberete mwaka 1999 na kupatiwa hati miliki mwaka 2002 kwa jina la Franklin Frederick Sumaye ambaye ni moja wa watoto wetu. Tuliendelea kulilima shamba hilo tukipanda mahindi, kunde na alizeti kwa miaka mingi bila matatizo. Katika shamba hilo pia tulichimba kisima kirefu cha mita 120 japo hatukukikamilisha kwa maana ya kuweka pampu kwa sababu kilihujumiwa na watu wabaya. Tangu wakati huo hadi leo hii shamba lina hatimiliki na linalipiwa kodi zote kila mwaka.

Mwaka 2007 serikali ilitoa tangazo la kulifanya eneo hilo la Mabwepande kuwa eneo la Mipango Miji na kuzuia maendeleo yoyote (permanent developments) katika eneo hilo mpaka serikali itakapotoa utaratibu wa kuliendeleza. Hivyo hatukuliendeleza kwa maana ya kujenga majengo lakini tuliendelea kulilima hadi hapo tutakapopata taratibu kamili za mipango miji ya matumizi ya eneo hilo kama yalivyo maeneo mengine katika eneo hilo. Ukweli tulipenda sana eneo hilo tulitumie kwa jambo litakalofaidia wengi na tulipanga kujenga chuo kikuu kwa ubia na watu wengine wa ndani na nje.

Wakati tunapanga mipango hii, mwezi Septemba mwaka 2015 wakati wa kampeni shamba hili na mashamba mengine tena mengine ya viongozi wa CCM yalivamiwa na wavamizi. Tulipeleka taarifa sehemu zinazohusika kwa maana ya polisi Wazo na serikali ya kijiji lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kuwaondoa wavamizi wetu. Lakini wavamizi katika yale mashamba mengine waliondolewa haraka kwa nguvu ya

jeshi la polisi na maeneo yale ambayo mengine labda yalikuwa hayajawahi kutumika kwa shughuli zozote yakawa salama. Tulifanya kila juhudi ili wavamizi waondolewe lakini kila juhudi ziligonga ukuta. Mimi binafsi nimeenda kwa mkuu wa wilaya wakati huo Bw. Paul Makonda tukaenda naye mpaka kwenye mkutano wa kijiji/kitongoji cha Mapwepande ambapo wavamizi walikuwepo na wakadai kuwa shamba hilo ni pori. Nilimwambia Bw. Paul Makonda kama wavamizi wanasema shamba hilo halijalimwa tangu miaka ya 2000 basi twende shambani halafu hata mtu moja tu atuonyeshe mti au magogo aliyoyang’oa shambani. Hakuna hata mtu moja aliyekubali kwenda kutuonyesha kwa sababu shamba lilikuwa safi wala halikuwa pori. Mkuu wa wilaya aliagiza kuwa shughuli zote zisimame kwa wiki mbili atakapotoa maamuzi.

Lakini usiku ule ule kulikuwa na kikao cha siri katika eneo hilo ambacho kiliongozwa na baadhi ya viongozi ikiwataarifu kuwa wao (wavamizi) waendelee tu na shughuli zao, na wakaendelea kweli. Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya alinishangaza pale alipowaambia wavamizi kuwa ikibidi ataniomba nigawe sehemu ya shamba hilo kwa wavamizi hao. Baada ya kuona amri yake hakuna aliyeitii na wavamizi wanaendelea na ujenzi nilijitahidi kumwona mkuu huyo wa wilaya mara kadhaa lakini ilishindikana na simu yangu akawa hapokei tena.

Alipokuja mkuu wa wilaya mpya Bw. Hapi nilienda kumwona na kumwelezea tatizo la wavamizi katika shamba letu la Mabwepande. Mwanzoni alikuwa kama ananielewa baadaye akageuka naye akawa hapokei simu yangu tena. Lakini yeye alienda hatua moja mbele kwa sababu alikwenda katika eneo hilo na kuwaambia wavamizi wasitoke katika eneo hilo kwa sababu watalipeleka kwa Mhe. Rais kufuta hatimiliki na wao wavamizi ndiyo watakaopewa eneo hilo. Na hilo ndilo lililofanyika hivi sasa. Huyu ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika wilaya yake ya Kinondoni.

Nilikwenda pia kumwona IGP, wakati huo Bwana Ernest Mangu, na kumwandikia barua nikihitaji msaada wake au aniruhusu mimi niwatoe wavamizi kwa nguvu. Baada ya kufuatilia, majibu ya IGP yalipatikana kutoka kwa aliyekuwa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Simon Sirro, ambaye alimwagiza RPC wa Kinondoni kuwa “suala la shamba la Sumaye liachwe kama lilivyo kwa sababu lina maagizo kutoka juu.” Niliporudi kwa IGP alicheka tu na kunishauri niende mahakamani nisitumie nguvu.

Kama nilivyokwisha eleza, tulifungua kesi mbili Mahakama Kuu kwa kufuata taratibu zote za kisheria, moja dhidi ya wavamizi na nyingine dhidi ya serikali. Kesi ziko mahakamani zinaendelea, mahakama imeweka zuio la muda (Court Injunction) kwa shughuli yoyote kutoendelea katika eneo hilo na wahusika wote yaani wavamizi na serikali wana habari na hatua hizo za mahakama. Leo tunavyoongea shamba hilo limetwaliwa na Rais tena kwa maagizo yale yale ya kusema ligawanywe kwa wananchi na wale wavamizi wapewe kipaumbele kama alivyowatangazia mkuu wa wilaya bwana Alli Salum Hapi hapo nyuma.

Napenda niwakumbushe kuwa Waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mhe. William Lukuvi tarehe 27 Oktoba mwaka 2016 alizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake. Ujumbe mkuu katika mazungumzo yake alikuwa anawaasa wananchi wasivamie maeneo ya watu wanayoyamiliki kihalali na hata kama hayajaendelezwa wasiyavamie bali waiachie serikali itachukua hatua za kisheria kuyafuta maeneo hayo.

Alipoulizwa swali na mwandishi moja kuhusu shamba la Sumaye Mabwepande mbona serikali haiwaondoi wavamizi wa muda mrefu waliovamia shamba hilo? Hapo lugha ya Waziri ikabadilika na kusema shamba hilo halijaendelezwa siku nyingi na mhusika amekwishapewa notisi ya siku 90 ya kunyang’anywa shamba. Lukuvi alimwuliza afisa Ardhi Mteule wa wilaya Kinondoni, “tulishatoa notisi ya kufutwa, si ndiyo?” aliendelea kusema hiyo taarifa haijafika ofisini mwake ili Rais atie saini yake.

Hata swali lake lilikuwa linaonyesha ni kitu anachokifuatilia kwa karibu kwa maslahi fulani. Kwa kejeli kubwa na chuki ya dhahiri na dharau kubwa kwangu Lukuvi alisema, “Sisi katika utendaji wetu hatuangalii sura ya mtu.”….”Kama wewe ulifikiri kwa sababu ulikuwa Waziri Mkuu hatutachukua hatua sasa umejibiwa kwamba tumechukua hatua na ofisa aliyechukua yuko pale.”

Baada ya maneno hayo ya waziri Lukuvi mimi nilijiuliza maswali kadha. Moja, hivi kama taarifa ya notisi ya kufuta hatimiliki haijafika ofisini kwa waziri, Lukuvi alijuaje habari ya notisi hiyo kuandikwa? Swali ambalo Waziri anamwuliza Afisa wake, “Tulishaandika notisi…si ndiyo?” maana yake ni yeye aliagiza hiyo notisi iandikwe na anajua notisi iko wapi na imeandikwa lini na kwa sababu gani.

Pili, kama ujumbe wa Lukuvi kwa umma ni kuwa watu wasivamie maeneo ya watu yanayomilikiwa kihalali hata kama hayajaendelezwa, kwa nini uvamizi ni halali kwa eneo Sumaye, eneo lake analomiliki kihalali na wala siyo pori kama inavyodaiwa, serikali imegoma kuwaondoa wavamizi kwa muda wa miezi kumi na minne na badala yake inawaambia wavamizzi wasiondoke kwa sababu watakabidhiwa hilo shamba? Sababu ni wazi ni kwa sababu Sumaye ananyang’anywa kwa sababu ya tofauti, ni sababu ya visasi vya kisiasa.

Tatu, Waziri Lukuvi anasema salama ya Sumaye ni aliendeleze shamba hilo ndani ya muda uliotolewa wa notisi wa siku 90 huku akijua fika kuwa notisi anayoisemea imetolewa siku 108 zilizopita (wakati huo) na wala mimi au yeyote katika familia yangu hakuna aliyepata hiyo notisi! Hivi inaingia akilini kuwa barua muhimu iliyotumwa kwa rejesta isinifikie kwa zaidi ya 90? Mimi siyo mtu wa anwani isiyojulikana hata simu zangu zinajulikana, hivyo hiyo barua imepotezwa njia kwa makusudi na njama hizo Waziri Lukuvi na wataalam wake na viongozi wengine wa serikali wanazijua na mimi kwa kiasi fulani nazijua pia.

Nne, huyu ni Waziri wa Ardhi anayesema niendeleze eneo hilo ndani ya siku 90, ni maendeleo yapi anayoyataka? Hivi hajui kuwa wizara yake ilikwishazuia shughuli za

maendeleo ya kudumu (permanent developments) katika eneo hilo kwa notisi ya serikali tangu mwaka 2007? Kisheria eneo hili lilikuwa shamba hadi mwaka 2007 na baada ya hapo maeneo yote ya Mabwepande yamekuwa chini ya mipango miji, anataka niliendelezeje eneo la mipango miji bila maelekezo sahihi ya serikali?

Tano, huyu ni Waziri wa Ardhi anayeniambia nikaendeleze eneo hilo ndani ya siku 90 wakati anajua fika kuwa eneo hilo lilemejaa wavamizi ambao wanaambiwa na serikali wasitoke maana shamba litachukulia na Rais na wao wavamizi ndiyo watakaopewa shamba hilo wagawane viwanja. Hivi kwa akili ya Waziri huyu ni kipi kingeanza, mimi nikaendeleze eneo ambalo liko chini ya himaya ya wavamizi wanaolindwa na serikali au serikali yake iwaondoe kwanza hao wavamizi ili mimi sasa nikafanye maendeleo anayoyasema Lukuvi? Waziri hapa anacheza mchezo wa mbwa mwitu na mwana kondoo tu. Tuache kiini macho tuseme ukweli.

Sita, na mwisho nataka nimwulize Waziri Lukuvi, Afisa Mteule wako ametoa hiyo notisi ya kunyang’anya shamba mwaka moja baada ya shamba kuvamiwa, na wavamizi hao walikwishagawana viwanja na kujenga vibanda vyao hivyo shamba hilo lilikwishasafishwa na ujenzi kuendelea. Shamba limevamiwa Septemba, 2015 na notisi ya kutoendelezwa shamba Juai, 2016, mwaka moja baadaye. Sasa hii notisi ya kutokuendelezwa shamba imetumia utaalam gani, ni kutokana na sura ya shamba kwa wakati huo wa notisi au ni utabiri wa kienyeji unaoona kuwa shamba hilo mwaka moja uliopita lilifananaje au alikuwa na picha za anga alizopiga mwaka moja uliopita ambazo zimeonyesha eneo hilo kuwa pori?

Maana wakati notisi inatolewa eneo limekwisha safishwa na vibanda vingi vimekwisha jengwa. Mkiwa na lengo la kumwonea mtu mwoneeni kwa akili. Haiingii akilini shamba lililovamiwa kwa mwaka mzima liko kwenye milki ya wavamizi unaitolea notisi ya kutokuendelezwa.

Mimi hatujagombana na Lukuvi juu ya shamba hilo wala juu ya madaraka yake kama Waziri wala juu ya mimi kuwa Waziri Mkuu mstaafu. Hivyo nashangaa hayo maneno na dharau na kejeli yote yanatokana na nini. Nataka nimwambie Mhe. Lukuvi mimi sijawahi kuidharau serikali wala kiongozi wa ngazi yoyote na yeye nataka anitambue mimi kama kiongozi mojawapo katika nchi hii na ninayestahili kuheshimiwa hata kama nimeihama CCM na kujiunga na chama cha upinzani. Ajue kuwa kama sisi wengine tungekuwa na roho mbaya na dharau kama yeye, wengine wao, ikiwa ni pamoja na yeye, wasingekuwa hapo walipo leo na pengine wangekuwa hata magerezani.
Shamba la Mvomero, wilaya ya Mvomero, Ekari 326

Shamba hili lilikuwa la Chama cha Msingi cha Ushirika kiitwacho Morogoro Farmers Primary Cooperative Society. Chama hiki walipata mkopo na kuweka shamba hili kama dhamana. Mkopo ulipowashinda kulipa, wanachama wa Ushirika huo
waliamua waliuze shamba lao kuliko kuuzwa na mdai. Walifuata taratibu zote za kisheria za vyama vya ushirika, wakapata vibali wilayani na hatimaye kutoka kwa mrajis msaidizi ambaye ni afisa ushirika wa Mkoa ambaye ndiye mwenye mamlaka ya kutoa idhini hiyo. Shamba likatangazwa na watu wengi walishiriki katika zabuni na zabuni ya mama Esther Sumaye ikashinda na kuuziwa shamba hilo. Baada ya taratibu zote za malipo kukamilika, Esther alikabidhiwa hatimiliki mwaka 2002 na hati hiyo imeandikwa kwa jina la Mrs. Esther Frederick Sumaye.

Kwa hiyo shamba hilo siyo la kijiji cha Mvomero kama wengi wanavyofikiri, lilikuwa mali ya wanaushirika ambao kwa hiyari yao na kwa kufuata taratibu zote za sheria na za serikali waliliuza. Shamba hilo hivi sasa nalo limetwaliwa na Rais kwa kisingizio kile kile cha kutokuendelezwa na kutokulipa kodi ya serikali mambo ambayo yote ni uwongo kama nitakavyoeleza hivi punde.

Ili kupata mtirirko mzuri nianzie nyuma kidogo. Mwanzoni mwa mwaka jana, 2016, Mhe. Rais alipita maeneo ya Mvomero na kuagiza kuwa mashamba yote ambayo hayajaendelezwa apelekewe orodha ayafute. Baraza la madiwani walikaa kupitia orodha hiyo na shamba la Esther Sumaye halikuwa mojawapo ya mashamba yaliyopelekwa kwa Rais kwa sababu waliona lina shughuli nyingi za kilimo na ufugaji. Hata hivyo baada ya hapo nilipata taarifa za chini chini kuwa kuna maagizo kutoka juu ili shamba hilo lijumuishwe katika orodha ya mashamba yasiyoendelezwa.

Nilikwenda kumwona mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr. Steven Kabwe nilimweleza hivyo hivyo kuwa nina habari zisizo rasmi kuwa umeagizwa shamba la Esther liingizwe katika orodha ya mashamba yasiyoendelezwa na kuwa yeye binafsi amepewa jukumu hilo. Nilimwambia yale yale niliyomwambia Mhe. Lukuvi kuwa mnafanya hivyo kwa sababu za kisiasa nikamwambia kwa sheria hamtaweza kulichukua labda Rais atumie nguvu. Akanibishia kuwa hana maagizo hayo lakini nilijua ilibidi afanye hivyo.

Mwezi wa nane mwaka jana tulistukizwa kupewa barua ya onyo (warning letter) kuwa tutoe maelezo ndani ya mwezi moja kwa nini hatutekelezi masharti ya hati ya shamba na pia hatukutii kanuni za ‘The Town and Country Planning (Use Classes) Regulations, 1960 as amended in 1993’. Barua haikufafanua ni nini tumeharibu au ni nini hatukufanya. Mama Esther alifuatilia kwa kuonana na afisa mteule mwenyewe lakini hakupata ushirikiano zaidi ya kuambiwa akasome sheria na kanuni za mipango miji ambayo alimpatia kurasa za sheria na kanuni zinazohusika. Kwa masharti ya hatimiliki ya shamba, shamba lile ni kwa “Agricultural purposes” ambayo kanuni (regulations) zinasema shughuli zake ni pamoja na kilimo, ufugaji wa wanyama mbali mbali na hata hifadhi ya misitu na mengineyo.

Hata hivyo tulijibu hiyo barua kwa ukamilifu wake. Pamoja na haya yote, mwezi wa kumi mwaka jana Mama Esther alipewa notisi ya siku 90 ya kunyang’anywa shamba. Notisi yenyewe kama kawaida haikufafanua ni nini hasa tulichokosea. Kodi ya ardhi tumelipa mpaka mwaka husika na matumizi ni kama nilivyoelezea. Tumejiuliza na nimewauliza wengine ikiwa ni

pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na pia Wakuu wa Mikoa ya Pwani na Morogoro tulipokutana, kuwa, “hivi ninyi mmewahi kuona Ruvu Ranch au Kongwa Ranch imelimwa kwa trekta au miti yake yote kufyekwa?” Kila moja alijibu “hapana.” Sasa hili la Sumaye ni nini si mseme? Tatizo liko wazi ni kuwa Sumaye amehama CCM na kuingia Upinzani lazima anyang’anywe mashamba ili afilisiwe.

Kama nilivyoeleza awali, ili kupinga hii dhamira chafu na ya uonevu ya serikali, tulifungua kesi mahakama kuu ili kuzuia serikali isiendelee kufanya uonevu wake mpaka shauri hilo litakapoamuliwa na mahakama. Mahakama ikaweka zuio lakini serikali ikaendelea na dhamira yake bila kujali wala kufuata utawala wa sheria kwa Rais kutwaa hilo shamba kabla kesi tuliyofungua mahakama kuu kufikia uamuzi.

Wakati shamba hilo linatwaliwa tarehe 27 April, 2017 kwa barua iliyoandikwa tarehe 2 Mei, 2017 ambayo ilifika posta ya Dar es Salaa tarehe 19 Julai, 2017, yaani zaidi ya miezi miwili, na sisi kuipata mwanzoni mwa mwezi Agosti, 2017; shamba hilo lilikuwa limelimwa zaidi ya ekari 50 ya mazao mbali mbali na lina mifugo kwa maana ya ng’ombe zaidi ya 200 na kondoo zaidi ya 300. Kuna nyumba za kudumu za kuishi, ghala la kuhifadhia mazao, trekta na vifaa/mashine za shamba, mabanda ya mifugo, visima viwili virefu vya maji na umeme umekwisha ingizwa hapo shambani. Shamba hilo lina hatimiliki na linalipiwa kodi zote za serikali bila kukosa.

Mwishoni mwa wiki iliyopita waziri Lukuvi alizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro kujaribu kuuelewesha umma kwa nini serikali imetwaa mashamba 14 mkoani Morogoro. Sababu kubwa alizotoa waziri huyo ni kuwa mashamba hayo hayakuendelezwa na kuyaita mashamba pori na pili yalikuwa hayalipiwi kodi ya serikali. Lakini kwa upande wa shamba la Mama Esther Sumaye, Waziri Lukuvi auambie umma sababu nyingine kwa sababu shamba hilo halidaiwi na serikali na kwa uwekezaji wa mali hizo zote nilizozielezea, huwezi kusema shamba hilo halijaendelezwa.

Nataka nimkumbushe waziri Lukuvi kuwa shamba hilo la Mama Esther Sumaye serikali kwa kupitia wizara yake katika Mkutano wa Bunge wa Sita, Kikao cha Pili cha tarehe 01/02/2012 ilijibu swali la mbunge wa Mvomero Mheshimiwa Amos Makala ilikiri kuwa shamba limepatikana kihalali na linatumika kama masharti ya hati miliki inavyotaka. Nanukuu sehemu ya Hansard ya jibu la serikali:

Mheshimiwa Spika …..napenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kuwa shamba lenye hati Na. 21919 lililoko katika kijiji cha Mvomero, Wilaya ya Mvomeru lenye ukubwa wa ekari 326 linamilikiwa na Bibi Esther Sumaye. ……. Mheshimiwa Spika, kumbukumbu zilizoko kwenye Wizara yangu zinaonesha kuwa awali shamba hilo lilikuwa likimilikiwa na Mvomero River Farmers Limited ya Mvomero kuanzia mwaka 1978 hadi Julai 1985 ilipohamishiwa kwa kampuni ya Wami & Magole Farmers Cooperative Society Limited ya Morogoro. Mnamo Machi 1996 kampuni ya Wami & Magole Farmers
Cooperative Society Limited ilibadirisha jina na kuitwa Morogoro Farmers Primary Society Limited. Aidha, tarehe 27 November, 2001 Morogoro Farmers Primary Society Limited walimuulizia ndugu Esther Sumaye shamba hilo na baada ya kukamilisha taratibu zote za kisheria ikiwa ni pamoja na kulipa ushuru kwa Serikali uhamishaji wa miliki (Transfer) ulikamilishwa mwaka 2002 kwa mujibu wa kifungu cha 61 cha Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1996.
Mheshimiwa
Spika, kwa kuwa Bibi Esther Sumaye anamiliki shamba hilo kwa mujibu wa sheria na kuliendeleza kwa kuzingatia masharti ya hatimiliki, Serikali inaheshimu haki zake na hivyo haitaweza kumnyang’anya kwani itakuwa ni ukiukwaji wa haki za kumiliki mali kama zilizoaihinishwa kwenye Ibara ya 24 (1) na (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.”
Hali ya shamba la mama Esther Sumaye haijabadilika kati ya mwaka 2012 na mwaka 2017 na labda imekuwa nzuri zaidi. Sasa ningependa tu kumwuliza waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, je ana kumbukumbu ya majibu hayo ya wizara yake kuhusu shamba hilo la Mvomero? Je hiyo serikali ambayo mwaka 2012 iliyojibu hivyo kupitia wizara yake ni hii hii ya Tanzania inayoongozwa na ccm au ile ilikuwa siyo serikli ya Tanzania?

Kama serikali tena kupitia wizara yake ilikiri kuwa shamba hilo linamilikiwa kihalali na limeendelezwa kwa kuzingatia masharti ya hatimiliki yake, kwanini Mhe. Lukuvi asiwe na ujasiri wa kusema shamba la mama Esther Sumaye linatwaliwa kwa sababu za kisiasa kama kisasi kwa mume wake kukihama chama cha mapinduzi na kujiunga na upinzani? Huo ndiyo ukweli japo Mhe. Lukuvi na wenzake hawatausema hadharani.

Utawala
Bora

Utawala bora ni utawala unaoheshimu katiba, unaofuata sheria, unaotii demokrasia na unaojali haki za watu na mali zao. Kuna taratibu ambazo huwekwa ili vigezo hivi vya utawala bora vifanye kazi. Utaratibu mojawapo ni kuwa na nguzo tatu za dola zinazoshirikiana lakini zilizo huru kutenda kazi zao bila kuingiliana kati ya nguzo moja na nguzo nyingine au nguzo moja kuingilia uhuru na utendaji wa nguzo zingine za dola. Nguzo tatu za dola ni Utawala (The Executive), Bunge (Legislature) na Mahakama (Judiciary).

Utawala ambayo ndiyo serikali ni chombo cha manguvu na mabavu na ina tabia ya kutaka kujifanya kana kwamba ndiyo nguzo muhimu kuliko zingine na hujisikia hivyo kwa vile ndiyo nguzo yenye vyombo vya dola kwa maana ya majeshi na taasisi zingine za usalama nakadhalika. Nguzo hii ndiyo inayoweza kuvuruga utawala bora katika nchi na hata kuiingiza nchi katika matatizo makubwa ya kiusalama.

Nguzo zingine mbili za Bunge na Mahakama kazi zake zinaeleweka na hazina nafasi kubwa ya kuingilia nguzo zingine isipokuwa pale ambapo wajibu wake wa kazi unataka iwe hivyo. Kwa mfano Mahakama kama kuna kesi kati ya serikali na raia binafsi, kazi ya mahakama ni kutafsiri sheria na kutoa hukumu bila kujali anayeshindwa ni serikali au ni huyo raia. Bunge ni chombo cha kutunga sheria na pia lina kazi ya kuishauri na kuisimamaia serikali kwa niaba ya wananchi.

Hali ikoje Tanzania?

Iko hali ya wazi na dhahiri nchini mwetu kuwa tangu utawala wa awamu ya tano uingie madarakani, “utawala bora umeanza kuwa bora utawala.” Tunashudia matumizi ya nguvu za dola hata ambapo pasingestahili nguvu hizo zitumike. Katika awamu hii kwa mara ya kwanza tumeshuhudia jeshi la polisi lenye silaha likiingizwa ndani ya bunge kuwapiga na kuwatoa nje wabunge wasio na silaha wanaobishana bungeni kwa kwa sababu ndiyo kazi yao ya msingi kupingana kwa hoja. Siyo sahihi kupiga watu wanaopingana kwa hoja.

Siyo mara ya kwanza wabunge wa upande moja kutokukubaliana na upande mwingine au hata na Spika na Spika katika hali ya namna hiyo huahirisha bunge ili vyama vikakae katika “caucus” zao kutulizana hasira na busara ichukue nafasi yake badala ya hasira.

Hali ya namna hii huikumba mabunge mengi sana duniani wengine hata kufikia hatua ya wabunge kuchapana makonde lakini huoni jeshi la nje likiingizwa bungeni maana bunge lina askari wake. Kilichotokea kwetu ni, kwanza, mhimili wa utawala umeingilia mhimili wa kutunga sheria yaani Bunge, na pili kuwatisha wabunge ili waogope kuikosoa serikali jambo ambalo ni wajibu wao wa msingi, na kwa kiasi kikubwa serikali imefanikiwa sana katika hili.

Siyo bunge tu ambalo limeingiliwa na serikali bali hata mahakama. Tumemsikia Mhe. Rais akiwaambia majaji na mahakimu siku ya mahakama duniani kwanini kesi za serikali zinashindwa mahakamani! Kwa tamko hilo kutoka kwa mtu kama Rais wa nchi maana yake anataka mahakama zitoe ushindi kwa serikali hata kama serikali ndiyo yenye makosa. Aidha alitamka kuwa sasa na mawakili wanaowatetea watuhumiwa nao wakamatwe wawekwe ndani. Tumeshuhudia pia mara kadhaa mali za watu zikitwaliwa na serikali bila kufuata sheria na wakati mwingine kesi za pingamizi zikiwa mahakamani.

Nyumba za watu zinavunjwa hata kama kesi ziko mahakamani na pengine nyumba zenye hati ya serikali hiyo hiyo. Mashamba na viwanda vinachukuliwa bila kufuata taratibu za sheria nk. Sipingi serikali kuchukua mali ya raia au kuvunja nyumba ya raia lakini taratibu za sheria lazima zifuatwe. Kwa upande wa viwanda, kwa mfano, viwanda hivi vilikuwa vya serikali ikashindwa kuviendesha na serikali kwa baraka na maelekezo ya Chama cha Mapinduzi ikaviuza.

Kisheria mnunuzi alipomaliza kulipia kiwanda alichokinunua akapewa hati zake za kukimiliki, kiwanda hicho ni mali yake na siyo mali ya serikali tena. Kama kuna masharti aliyopewa muhusika, utawala bora unaitaka serikali izungumze na mhusika na ikishindikana impeleke mahakamani ili umiliki wa kiwanda hicho urudi serikalini

lakini siyo vinginevyo. Sheria isipofuatwa waathirika wa nyumba zinazobomolewa, mashamba yanayonyang’anywa, viwanda vinavyonyng’anywa na uwekezaji unaonyang’anywa maeneo yao wakiamua kwenda mahakamani nchi hii tutalipa fidia kubwa sana na hiyo ni fedha za kodi zetu ambazo zingefanya shughuli nyingine za maendeleo.

Aidha kuna matamko mengine hasa yanayotolewa na Mhe. Rais na Mhe. Waziri Mkuu ambayo yanatekelezwa na vyombo husika bila hata kuwa amri halali kwa maana ya kutokutangazwa katika gazeti la serikali. Matamko mengine yana athari kubwa kwa wananchi.

Kwa mfano, waziri mkuu aliwahi kuagiza kuwa pombe ya viroba isionekane kwenye mabaa ndani ya kipindi kifupi nadhani cha wiki kama mbili. Waziri mkuu anajua viroba vya konyagi vinatengenezwa na kampuni halali ya kwetu Tanzania tena iko DSM, kulikuwa na ugumu gani kuiagiza kampuni hiyo isitengeneze viroba hivyo badala yake unatoa amri isiyo rasmi ambayo imetoa hasara kubwa kwa wafanyabiashara halali walionunua pombe hiyo kihalali na kuilipia kodi ya serikali?

Wako wafanyabiashara waliokamatwa na kutiwa ndani na yuko moja (hatujui kama wako wengine) wa Dodoma aliyejipiga risasi na kupoteza maisha. Nimewahi pia kumsikia Mhe. Waziri Mkuu akitoa agizo kuwa kuanzia sasa binti wa shule akipata mimba wazazi wake wote wawili watafungwa miaka 30 jela. Mwanzilishi wa amri hizi za imla ni Mhe. Rais mwenyewe na sina hata haja ya kuyarudia ila ajue tu ameyaambukiza katika ngazi nyingi za utawala wake. Sasa wakuu wa wilaya wanaweka watu ndani masaa 48 bila kufuata sheria zinavyotaka, wanaagiza mashamba ya watu yafyekwe bila kufuata sheria na matamko mengine mbali mbali.

Hali hii ya uongozi wa kiimla sasa imeanza kuikumba hata mhimili wa Bunge. Mhimili wa Bunge ndiyo wananchi tunategemea uwe mhimili wa mfano wa kujenga na kutetea demokrasia. Naona hali inaanza kubadilika kwa sababu kila moja anaanza kuiga kudhani jinsi unavyoonyesha mabavu ndivyo unavyoonekana kiongozi bora. Sipendi kuingilia mambo ya bunge lakini kama yana athari kwa umma hatuwezi kunyamaza. Mwishoni mwa kipindi cha bajeti mwaka huu, baada ya kupigia kura bajeti, nilimsikia kiongozi wa bunge akisema wale wabunge ambao hawakuipigia bajeti kura ya ndiyo hawatapata mgao wa bajeti katika majimbo yao maana wameikataa bajeti.

Nilidhani utani lakini sasa kuna maeneo ambayo yako chini ya wapinzani miradi ya maendeleo imeanza kuondolewa. Mimi najiuliza, tamko la Mhe. Spika na haya yanayotokea ni “coincidence” tu au alikuwa na maagizo kutoka muhimili mwingine yaani utawala? Aidha kwa kesi ya wakina Halima Mdee na Esther Bulaya nilimsikia Mheshimiwa Spika Job Ndugai akiongea kwa hasira sana na kusema waende kokote wanakotaka kwenda lakini mwaka mzima hakanyagi mtu hapa! Inawezekana taratibu za Bunge sasa zimebadilika, lakini nijuavyo mimi spika ni kiongozi wa Bunge na maagizo anayoyatoa ni maamuzi ya Bunge na siyo yake.

Pili mhimili wa mahakama ndiyo wenye haki ya kutafsiri sheria na hakuna muhimili mwingine ambao maamuzi yake hasa yale yanayoumiza mtu mwingine yakawa ndiyo ya mwisho. Mahakama inao uwezo hata wa kuiambia bunge kuwa sheria mliyoitunga ni mbovu na bunge inabidi liirejee sheria hiyo na kufanya marekebisho. Naomba Bunge letu lisiingie kwenye mtego huu wa kudhani kutumia mabavu ndiyo kuonekana u shupavu.

Utawala
wa visasi

Kama nilivyoeleza, kuna mifano mbali mbali inayodhihirisha watu kusakamwa kwa sababu tu ya kuwa katika upinzani. Kusakamwa huko ni pamoja na kunyang’anywa baadhi ya haki au stahili wanazostahili, kunyang’anywa mali na mengineyo ambayo ni mabaya zaidi na sitayasema kwa leo lakini yakiendelea itafika siku yake nitayasema. Nataka tu nitahadharishe kuwa tukianza kujenga visasi hakuna atakayepona au kama atapona basi inabidi aikimbie nchi mara tu baada ya kipindi chake cha uongozi.

Hali hii ikishajengeka lazima viongozi wetu wawe wezi ili katika kipindi cha uongozi wajiwekee akiba ya kutosha nje ya nchi itakayowasitiri wakiwa wakimbizi. Nawaomba wahusika waache hii dhambi maana itawatafuna, tena wengine wenu mna mali nyingi, wengine mna mabasi wengine mna mahoteli makubwa makubwa, na mengineyo mengi wala siyo shamba za wakina Sumaye.

Kutoka CCM kwenda Upinzani

Mimi nilitoka CCM na kujiunga na CHADEMA kwa hiari yangu mwenyewe kwa maslahi ya umma. Wakati natoka CCM mwezi Agosti 2015 nilieleza kwa ufasaha sana kwanini ninatoka CCM na kujiunga na Upinzani. Labda nirudie tu kwa ufupi labda hata wanaonifungia visasi wakielewa wanaweza kunipongeza badala ya kuniumiza.

Siasa ya vyama vingi ni ushindani wa kisiasa na ushindani sahihi unapokuwepo, mnufaika ni mwananchi kama ilivyo kwa biashara ya ushindani wanaonufaika ni walaji kwa maana ya kupata huduma nzuri na bei nzuri. Siasa ya vyama vingi inakuwa na maana tu kama kuna vyama angalau viwili vyenye nguvu zinazolingana lingana ili wananchi wawe na amani wanapochagua kiongozi wao wa juu kuwa anaweza kutoka chama A au chama B. Hapo ndipo wananchi wataanza kunufaika na mfumo wa vyama vingi vya siasa. Lakini kwa sura tuliyonayo sasa ya kuwa na chama kimoja ndicho kina haki tu ya kuongoza nchi iwe kwa haki au hapana, mfumo wa namna hii una madhara makubwa mawili.

Moja hautaleta maendeleo kwa umma kwa sababu chama na serikali yake hawana sababu ya kuwajibika ipasavyo kwa sababu wanajua kuwa inyeshe mvua liwake jua wao ndo washindi wa kura. Sababu ya pili ni kuwa hakuna chama chochote cha siasa chini mfumo wa vyama vingi ambacho kimetawala milele. Hata kingefanya vizuri namna gani watu watakichoka na watataka mabadiliko. CCM imeshavuka hatua hiyo na watu wameichoka hivyo ni vema kujenga uwezo wa chama kingine ili kishike dola badala ya CCM vinginevyo nchi nchi inaweza kuingia katika hali mbaya ya usalama.

Kwa hiyo nimetoka CCM ili kujenga nguvu ndani ya upinzani ili kuiepusha nchi na balaa inayoweza kutokea kwa chama kimoja kung’ang’ania kukaa madarakani hata kama watu wamekichoka na wanataka mabadiliko. Katika mfumo sahihi wa demokrasia ya vyama vingi chama kimoja hakitakiwi kikae madarakani zaidi ya miaka kumi mfululizo na ikizidi sana kumi na mitano lakini siyo miaka hamsini au sitini kama inavyokuwa kwa CCM. Ukiona chama kinakaa zaidi ya miaka ishirini madarakani ujue hapo mfumo wa vyama vingi ni wa jina tu.

Kwa hiyo mimi nimehama CCM kwa maslahi ya umma na siyo kwa maslahi yangu binafsi. Kwa sababu nilihama CCM kwa maslahi ya umma na hayo malengo hayajatimia, suala la kufikiri tabu yoyote ya binafsi kama hii ya kunyang’anywa mashamba kwamba ati inaweza kunirudisha CCM ni ndoto ya mchana. Watanzania wote naamini wameona manufaa ya upinzani kuwa na nguvu. Juhudi mbali mbali zinazofanywa na serikali hivi sasa ni matokeo ya nguvu kubwa iliyoongezeka kwa upinzani. Ingekuwa serikali

haiuogopi upinzani ingeendelea kusinzia kama kawaida yake. Na kama serikali isingeubana upinzani kuanzia bungeni hadi kwenye mikutano ya hadhara nina uhakika kasi ya maendeleo yetu ingeongezeka sana. Na haya ndiyo madhara ya chama kimoja kutawala kwa muda mrefu na kuzuia vyama vingine visijitokeze au kuviziba pumzi .

Alipata ardhi kwa nguvu ya madaraka yake, amenyang'anywa ardhi kwa nguvu ya madaraka ya mtawala, awe mpole
 
Yawezekana kweli sumaye ana makosa lkn kulikua na uharaka gani wa kuyachukua mashamba yake wakati kesi zipo mahakamani?
Hapo ndipo swala LA visasi linapoingia.
Umuhimu wa mahakama uko wapi kama serikali haiiheshimu?
 
Back
Top Bottom