Sumaye afunguka suala la familia yake kunyang'anywa mashamba mawili!

CHADEMA kama taasisi naona sasa kinatetereshwa..

Haya matamko ya sumaye kuhusu mashamba yake alitakiwa akayafanyie huko na isiwe chini ya kivuli cha CHADEMA au ofisi ya CHADEMA..
Mambo kama haya ndo huwa yanauwa chama. Kila mtu anajitahidi kutumia chama kwa maslahi binafsi.
 
Sumaye si mtu wa kumhurumia hata kidogo.... this is what we call "what goes around comes around". Na kuna tofauti kubwa sana kati ya siasa za Lowasa na yeye...hasa kimatamshi....japo wote walihama CCM. Lowasa mjanja mjanja sana....Sumaye anyang'anywe mpaka boxa...anatafuta kiki tu na huruma ....JPM nyoosha ruler tu baba.
Nimecheka sana! Hadi boxer!
 
Mambo kama haya ndo huwa yanauwa chama. Kila mtu anajitahidi kutumia chama kwa maslahi binafsi.
Chama kinaelekea kukosa agenda ya kusimamia..

Sumaye anataka tatizo lake lichukuliwe kama tatizo la chama, huu ni udhaifu mkubwa!

Ni jambo la ajabu sana, chama kimefanywa kama hakina kiongozi!
 
Chanzo cha kuingia ndani ya mgogoro ni yeye kuhamia CDM.Kwa mantiki hiyo hapa palikuwa mahali muafaka.
Mkuu, unafikiri mimi hilo silijui? Nalitambua vyema..

Lakini ni sahihi mtu kukitumia chama katika matatizo yake? Kama yangekuwa ni maeneo ya chama yametwaliwa ingekuwa sahihi lakini sio kwa ardhi binafsi ya mtu na familia yake..

Hawa watu waliotoroka huko CCM ninwatu wakuishi nao kwa makini sana!
 
Tumeacha mambo ya msingi aliyosema na kumsakama mtu. Ameeleza hatua kwa hatua ya kilichotokea na pia suala la utawala bora. Hatugusi issues zilizomo tuna attack personalities what kind of people! Ule msemo wa kifalsafa unaosema simple minds zinadiscuss watu unadhihiri. I am Sorry!
Kuna wengi wamekutwa na makubwa hawasemi na orodha inaongezeka ninajua marafiki zangu walioUmia kupitia huu mtindo tunaoendelea nao na kuushabikia. MUNGU ATUNUSURU
 
Wakati nikisoma masters tulikuwa na kipengele kimoja muhimu sana cha "Book Critique" yaani unasoma vitabu na kisha kuvichambua critically ukibainisha strengths, weaknesses. relevance etc. yaani unaangalia kilichomo au content yake kabla hata ya kuangalia maisha ya mwandishi.
Kwa hiyo bila kumwangalia Sumaye tunaangaalia kwanza hoja zake tunazichambua kwa hoja kisha baadae twaweza kusema "ingawa ni hivi au vile inaelekea msemaji amechukua uelekeo ... kwa sababu ya historia yake au so and so ... Mmenipaata?
 
Najua ni ubaya ambao hatutakiwi kuushabikia, lakini wale wote walioshiriki kuutengeneza huu mfumo nawaombea mungu wapate tabu za maana na wao ili wajue Watanzania wanapata tabu kiasi gani. Baba yangu alifukuzwa kazi kwa kuonewa kabisa akafika mpaka kuonana na waziri wa kazi kipindi hicho na alikuwa kwenye haki lakini haya majitu yalivyoutengeneza mfumo wa rushwa na kutokumjali mtu wa hali ya chini bado baba yangu hakuipata haki yake. Leo yanalilia lia nini? JPM wasomeshe namba kwa lugha zote, kikurdi, kilatino, kigujurati, kichina, kifaransa, kiarabu, na hata kisukuma ikiwezekana
 
CHADEMA hamnaga kulialia hovyo, kama vipi arudi CCM arejeshewe mashamba yake
 
Sumaye amechanganyikiwa tu.mapori ameyazuia kwa miaka 20 leo analalamika kwani hajui sheria?
 
Adhabu ni hapahapa duniani. Aliyomfanyia mtu mmoja wa Arusha aitwaye Askofu hatujasahau. Ndiyo hayahaya yanamkuta na yeye. Allah subhana huwataallah anatoa majibu sasa....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah.....karma na malipo ni hapahapa...hakuna akie msafi...hao wanaojiona wamesimama sasa kimamlaka na kiutawala wajue kuna kesho , kuna kizazi chao....Case study iwe zSumaye...ni nan alijua kwamba yatamkuta yaliyomkuta.....Hakuna aliye msafi hata kidogo...kila mtu tumemsikia ni skendo kibao...hivo visasa viishe haki na busara itawale zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom