Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Sumaye anasema nchi za Ulaya Chama kikishindwa uchaguzi kinakubali na kupisha wengine lkn mbona pia hasemi kwamba nchi hizo hizo za Ulaya Chama kikishindwa Uchaguzi basi Kiongozi wa Chama aliyekiongoza Chama chake kwenye Uchaguzi hujiuzulu? Mbona Mbowe bado Mwenyekiti chadema ingawaje amekiongoza chadema kwenye chaguzi tatu na ameshindwa zote? Mbona hilo Mzee Sumaye huliongelei?
Kama unataka (Sumaye) tuwaige Wazungu wa Ulaya basi tuwaige kila kitu na siyo pale tu ambapo tunanufaika, hivyo nilitegemea uanzie na Mwenyekiti wako Mbowe kama swala ni kuwaiga Wazungu aondoke kwa maana ameshashindwa uchaguzi mara tatu hivyo hawezi kuwa na jipya!
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye amezitaka nchi za Afrika kuhakikisha zinakubali kubadilishana madaraka pale chama kimoja kinaposhindwa kuongoza ili kuepusha nchi kuingia kwenye machafuko.
Aidha, Sumaye alisema ni vyema wataalam wakaongoza nchi kwa kubuni mbinu mbalimbali za kujikwamua kiuchumi.
Sumaye aliyasema hayo jana Jijini hapa wakati akizungumza kwenye kongamano la Nafasi ya Wasomi na Wafanyabiashara Katika Kujenga na Kukuza Uchumi wa Nchi, lililoshorikisha viongozi wa vyama, wafanyabiashara na wasomi wa kada mbalimbali wa Arusha.
Sumaye alisema uongozi ni kubadilishana nafasi na katika nchi za Ulaya kwa mfano, chama kikishindwa kutawala kinakubali lakini kwa nchi za Afrika kuna uroho wa madaraka au ubinafsi.
"Tunataka kuwajengea uwezo wasomi wetu kwa kujiamini na kujipatia fursa za kujikwamua kiuchumi," alisema Sumaye ambaye alikuwa Waziri Mkuu kwa miaka 10 mfululizo kati ya 1995-2005, kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi.
"Ubinafsi tuache, tukishindwa uchaguzi achia ngazi.Mimi niliyasema haya nikiwa CCM na leo hii nipo Chadema nasema unapoang'angania madaraka, aidha unaogopa ukiachia utasababisha machafuko au ubinafsi."

(Kwa hisani ya Blogu ya Mpekuzihuru!)