Sumatra yazifungia boti za kasi Ziwa Victoria

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
Sumatra%2814%29.jpg

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na Majini (Sumatra).



Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na Majini (Sumatra) imezifungia kwa muda usiojulikana boti ziendazo kasi za kampuni ya Lake Express kutoa huduma ya usafiri katika Ziwa Victoria jijini Mwanza kutokana na vyombo hivyo kubainika kuwa na kasoro nyingi za kiufundi.
Hatua hiyo inafuatia Sumatra kupitia wataalamu wake kuzifanyia ukaguzi na kubaini zina mapungufu mengi ambayo yamewafanya kuzizuia kutoa huduma ya usafiri kati ya miji ya Mwanza na Bukoba.
Ukaguzi huo ambao ni wa pili ulifanywa na maofisa wa Sumatra Januari mwaka huu ambapo ilibainika kuwa boti hizo bado zimeshindwa kukidhi viwango vya kuziwezesha kutoa huduma ya usafiri.
Mkurugenzi wa Usalama wa Majini wa Sumatra, Kapten King Chiragi, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na Nipashe kuhusu matokeo ya ukaguzi wa mamlaka hiyo kwa boti hizo mapema mwaka huu. Alikiri kuwa kama boti hizo zitaruhusiwa kubeba abiria kwa sasa zinaweza kusababisha madhara makubwa kwa jamii ikiwemo ajali kwa kuwa zina mapungufu makubwa ya kiufundi.
Sumatra ilikubali ombi la kampuni ya Lake Express ya kutaka boti hizo zifanyiwe ukaguzi na baada ya ukaguzi huo, watalaamu walibaini kuwa hazifai kusafirisha abiria.
Akizungumza na Nipashe mapema mwaka huu, Chiragi alisema boti hizo zilikuwa zinatoa huduma ya usafiri kati ya miji ya Mwanza na Bukoba, lakini zilisimamishwa baada ya kuoenekana zina matatizo ya kiufundi.
Hata hivyo, Chiragi alisema mmiliki wa boti hizo kwa sasa ameomba kufanya safari zake kati ya Mwanza na visiwa vidogo katika Ziwa Victoria badala ya kwenda Bukoba kama ilivyokuwa awali endapo atakamilisha matengenezo yake.
Boti hizo ziendazo kasi ziliingizwa nchini wakati wa uongozi wa awamu ya tatu lakini aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli alizinyima kibali cha kusafirishwa kupelekwa Mwanza kupitia barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa maelezo kuwa hazikutimiza taratibu.
Badala yake, boti hizo zilisafirishwa kupitia Kenya hadi Mwanza.
Dk. Magufuli aliwaelekeza wamiliki wa boti hizo kuzipunguzaukubwa kabla ya kuzisafirisha, lakini wakikataa ushauri huo.



CHANZO: NIPASHE
 
Wakati huu usafiri wa Bukoba Mwanza unapotesa watu najiuliza tungeku wapi kama waziri Magufuli asingetuzuilia zile meli ziendazo kwa kasi? Zilishaletwa hadi Mombasa, akasema kamwe hazitakanyaga barabara za Tanzania. Wakataka ziende Kisumu zipitie ziwa Victoria, akakimbia Kenya akaziwekea sooo! Leo tunataabika! Hivi ingekuwa ni vita na hizo no zana kijeshi, angezizuia zisiende front line?
 
Wakati huu usafiri wa Bukoba Mwanza unapotesa watu najiuliza tungeku wapi kama waziri Magufuli asingetuzuilia zile meli ziendazo kwa kasi? Zilishaletwa hadi Mombasa, akasema kamwe hazitakanyaga barabara za Tanzania. Wakataka ziende Kisumu zipitie ziwa Victoria, akakimbia Kenya akaziwekea sooo! Leo tunataabika! Hivi ingekuwa ni vita na hizo no zana kijeshi, angezizuia zisiende front line?

Wanasemaga kama jambo hulijui so vizuri kuliongelea
Mleta huzi hujui unachokiongelea.
Hizi meli zilisafirishwa kupitia kisumu na zikafika hadi Mwanza na kuanza kufanya kazi.Nilisafiria meli hizi siku moja kwenda Bukoba.
Lakini yalikuwa maboti mazee na hayakufanya kazi muda mrefu yakasimamishwa na mamlaka husika kuwa yanaweza kuleta hatari. Huu ndio ukweli
 
Hizo boti zilishafika Mbona na zikaanza na kazi,, ila zilipata shida ziwani kwenye issue ya proppelling force,, ujuwe maji ya ziwa ni mazito tofauti na ya bahari mepesi,, sasa inaonekana huko zilikotoka zilikuwa Zinafanya kazi baharini... Zilipata shida sana ziwani
 
Back
Top Bottom