SUMATRA yatoa ofa ya usafiri mikoa ya kaskazini

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), imetoa nafasi chache kwa wamiliki wa kampuni za mabasi yaendayo mikoani wanaotaka kubadilisha leseni za safari zao kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya kaskazini, wafanye hivyo.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri Barabarani, Leo Ngowi, alisema ofa hiyo imetolewa baada ya kuona kuna abiria wengi wanaokwenda Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara wakitokea Dar es Salaam.

Alisema kwamba, baada ya SUMATRA kuanza operesheni ya kudhibiti upandaji wa nauli kiholela, kwa kushirikiana na polisi wa kikosi cha usalama barabarani, wamebaini kuna abiria wengi wanaobaki Dar es Salaam kutokana na uchache wa mabasi yanayokweda mikoa hiyo.

“Miezi hii ni ya kuelekea sikukuu na kama inavyofahamika, watu wa mikoa ya kaskazini wamekuwa na tabia ya kurudi kwao kujumuika na familia zao kuaga mwaka na kukaribisha mwaka mpya.

“Sasa takribani wiki moja katika operesheni ya kudhibiti hali nauli zisipandishwe hovyo, tumeshuhudia abiaria wakibaki kila siku. Sasa tumeona ni vema tukatoa ofa kwa kampuni zingine kubadili leseni zao na kwenda mikoa hiyo.

“Tunaomba kampuni chache zifike hapa Sumatra kuanzia leo (jana) ili zibadilishe leseni kwa ajili ya kufanya safari za kwenda huko mikoa ya kaskazini hadi Januari 20, 2013 na baada ya hapo, zitarudi kwenye barabara za awali,”alisema Ngowi.

Katika hatua nyingine, aliwaonya madereva wa mabasi ya mikoani na mengine kuacha mwendo kasi ili kuepuka ajali za mara kwa mara katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu.

“Tunaomba wamiliki na madereva wasipandishe nauli kiholela kwa lengo la kujinufaisha wenyewe kwani tutakapobaini ukiukwaji huo, tutazifungia kampuni za usafirishaji na watalazimika kuwarudishia abiria kiwango cha nauli kisichozidi Sh 250,000 ikiwa ni pamoja na faini.

“Kwa upande wa abiria tunawaomba washirkiane na polisi pamoja na Sumatra pale wanapobaini kutapeliwa na pia tunawaomba waepuke kununua tiketi vichochoroni,”alisema.
 
Safi sumatra haya majitu yamezoea kutukamua hela msimu wa sikukuu.....
 
Safi sana kama walivyosema wawe wachache isije wakakimbilia kule na kwingine ikawa shida tena...hasa njia ya mbeya na dodoma naona magari ni mengi sana!
 
Safi sana!! Hizo ndizo busara bhana, sio minguvu na kelele kila mwisho wa mwaka. Nimetamani niwe njiani (Kibaha, Chalinze, Korogwe, Mombo, Same, Mwanga, Kiborloni) kupata kisusio, mbege, ndafu, marafiki.. Ngoja nimalize shule. Mwakani nimooo!!
 
Maamuzi ya kiutendaji hayo, yanazingatia mahitaji ya wanainji.
Hongera Sumatra!
 
haya ni maamuzi ya kilevi!yaani ni sawa na kuhamisha tatizo kutoka kaskazini ,kulirudisha dar na sasa watalupeleka mikoa mengine.
Hawa ndio watendaji vihiyo!
 
Back
Top Bottom