SUMATRA yatangaza nauli halali ya Mbezi, Kibaha, Mlandizi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
MAMLAKA ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA),mkoani Pwani ,imewaasa wamiliki wa mabasi madogo ya abiria (daladala) yanayofanya safari zake Mbezi -Kibaha kuacha kupandisha nauli tofauti na zilizotangazwa kisheria.

Imesisitiza nauli halali kutoka mbezi hadi Kibaha ni Tsh 500 badala ya 800 wanayoitoza kwa sasa kwa abiria na Mbezi-Mlandizi ni Tsh .1,600 badala ya Tsh 1,800/2,000 inayolipishwa sasa.

Aidha kuanzia sasa basi litakalobainika kutoza nauli tofauti na elekezi atafikishwa mahakamani ama kutozwa faini.

Hayo aliyasema na Ofisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchikavu na Majini (SUMATRA) Mkoa wa Pwani, Omary Ayubu, mjini Kibaha baada ya kufanya zoezi la kushtukiza kukamata magari yenye makosa mbalimbali, kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoani hapo kupitia kitengo cha usalama barabarani.

Alisema wamekuwa wakipokea malalamiko mengi kutoka kwa abiria kuwa wanatozwa nauli kubwa suala amabalo ni kinyume na sheria.

Ayubu alitaja viwango vya nauli vinazopaswa kulipwa kuwa ni Mbezi- Kiluvya kwa Komba sh.400 badala ya sh.700 na Mbezi-Picha ya Ndege sh.700 badala ya 900.

Maeneo mengine ni Mbezi hadi Mlandizi sh.1,600 badala ya 1,800/2,000, Mbezi- Kongowe sh.1,100, Mbezi-Vigwaza 2,100, Mbezi-Chalinze 3,200, Mbezi-Lugoba 4,100 na Mbezi-Msata 4,600 .

“Leo katika operesheni hii tumekamata magari 21 kutokana na makosa ya kutokuwa na ticket na kutoza nauli kubwa “

“Madereva nane watapelekwa mahakamani kutokana na kuzidisha nauli kinyume cha sheria na tunawataka wamiliki kuzingatia masharti ya leseni,” alisema Ayubu.

Alisema wataendelea kuwachukulia hatua za kisheria madereva wanaokiuka sheria na ameshukuru wananchi kwa ushirikiano wao wa kutoa taarifa juu ya magari yanayoendelea kutoza nauli ambazo ni kinyume cha utaratibu.

Ayubu aliwataka madereva kuwa na katabia ka kugomo kwani haina faida na badala yake mwenye malalamiko aende ofisini na kuandika barua ndani ya mwezi mmoja ili malalamiko yao yaweze kutafutiwa ufumbuzi.

Nae kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Pwani,Salum Morimori alisema kuwa walifanya ukaguzi kwenye mabasi hayo ili kuangalia ubora wa magari .

Alieleza kumekuwa na malalamiko toka kwa abiria kutopewa tiketi, abiria kuchanganywa na mizigo ,ubovu wa magari,matairi mabovu na kuchakaa kwa viti kwenye magari hayo.

Morimori alisema ,hadi sasa magari 35 yamekamatwa ,kati yake 21 ni makosa yanayosimamiwa na SUMATRA na 14 ni ya kiusalama barabarani.

“Tumefanya zoezi hili la kusthtukiza kwa kushirikiana na wenzetu SUMATRA ili kuwajengea kumbukumbu madereva kufuata sheria za usalama barabarani,” alisema Morimori.

Hata hivyo, alisema kuwa lengo ni kuhakikisha usalama wa wanajamii hasa wanaotumia vyombo vya moto wabaki salama.

“Wamiliki na madereva wahakikishe wanaboresha vyombo vyao viko salama kwa kufanya marekebisho hasa mipira na tunahitaji wanajamii kushirikiana nasi ili kukabiliana na madereva ambao wanakiuka sheria za usalama barabarani” alisema Morimori.
 
wamegundua hawatoi risiti na wakitoa hawaandiki kiasi cha nauli.
 
sumatra ni waonevu wakubwa, hawafanyi uchunguz kikamilifu, bei ya vipuri na mafuta haishuki, pia ruti hii inaongoza kwa daladala ni nyingi mno, askari wengi wanakaa kibaha hivyo wakipanda wanapanda bure hii loss nani anaiona, halafu wajaribu kushusha nauli ya mwendokasi ndio tutawaelewa
 
Hongereni SIUMATRA nasubiri TRA nao watangaze mapato yetu mazuri kwa mwezii huu
 
Hiyo nauli ni ndogo, uendeshaji wa vyombo vya usafiri ni mgumu vipuri, mafuta na spare parts nyingine kodi iko juu na bado wanatoa bei isiyo na faida
 
Washushe bei mafuta, watoe kodi za hovyo kwenye vipuri waone kama wamiliki hawatokubali.
 
Bado nashangazwa na SUMATRA.
Tegeta-Makumbusho 500/-
Mawasiliano -Tegeta 500/-
Mbagala-Makumbusho 500/-
Makumbusho-Temeke 500/-
Hivi haya maeneo yana distance sawa?
Maana Kibaha-Mbezi nako 500 while Mawasiliano-Mbezi ni 500/-
 
Bado nashangazwa na SUMATRA.
Tegeta-Makumbusho 500/-
Mawasiliano -Tegeta 500/-
Mbagala-Makumbusho 500/-
Makumbusho-Temeke 500/-
Hivi haya maeneo yana distance sawa?
Maana Kibaha-Mbezi nako 500 while Mawasiliano-Mbezi ni 500/-
VP kuhusu mbagala gongolamboto? Mbezi- kibaha hapana umbali wowote,kama hakuna foleni hakika 15 tu,sema daladala zinatumia hadi nusu saa
 
  • Thanks
Reactions: SDG
VP kuhusu mbagala gongolamboto? Mbezi- kibaha hapana umbali wowote,kama hakuna foleni hakika 15 tu,sema daladala zinatumia hadi nusu saa
Sumatra bado kwenye upangaj wa nauli kuna shida sana.
Mbagala-Makumbusho 500/-
Ila Makumbusho-Bunju 750/-
 
Bado nashangazwa na SUMATRA.
Tegeta-Makumbusho 500/-
Mawasiliano -Tegeta 500/-
Mbagala-Makumbusho 500/-
Makumbusho-Temeke 500/-
Hivi haya maeneo yana distance sawa?
Maana Kibaha-Mbezi nako 500 while Mawasiliano-Mbezi ni 500/-
ONGEZA NA HII HAPA:
Tegeta to K/koo/Posta 500/-
Nyaishozi to Makumbusho 750/-
Bunju Sokoni to Makumbusho 750-
Yaani [HASHTAG]#SUMATRA[/HASHTAG] inabidi itoe muelekeo sahihi maana umbali hautoi usawa wa nauli.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
ONGEZA NA HII HAPA:
Tegeta to K/koo/Posta 500/-
Nyaishozi to Makumbusho 750/-
Bunju Sokoni to Makumbusho 750-
Yaani [HASHTAG]#SUMATRA[/HASHTAG] inabidi itoe muelekeo sahihi maana umbali hautoi usawa wa nauli.
Niliwah kuwauliza,wakasema wanaangalia na ubora wa barabara, sasa najiuliza inamaana Bagamyomo road ni mbaya zaidi ya kawawa road na Kilwa road?
 
Gongo la Mboto hadi Kisarawe mjini kuna umbali usiozidi km 6 lakini nauli iliyopangwa na sumatra ni shilingi 700/=
 
Back
Top Bottom