SUMATRA yaifungia kampuni ya mabasi ya City Boy ambayo mabasi yake mawili yalisababisha ajali jana

Pistol

Senior Member
Oct 13, 2015
194
86
Mamlaka ya Usafiri Ardhini(SUMATRA) imeifungia Kampuni ya City Boy, ambayo mabasi yake mawili jana yalisababisha ajali mbaya iliyopelekea watu 30 kupoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa.

Jana taarifa zilienea mtandaoni kuwa ajali hiyo ilisababishwa na uzembe wa madereva kwa kile kilichofahamika kuwa walikuwa wakifanya mchezo barabarani kwa kukimbizana huku wakipishana kuelekea kila upande, na ikapelekea kutokea kwa ajali hiyo mbaya.

Pia inasemekana kuna basi moja kati ya hayo mawili lilipigwa tochi na polisi kwa kuzidisha speed.

=======

SUMATRA yafungia mabasi 12 ya City boy kutokufanya safari zake kwa kusababisha ajali na kuuwa watu 30.

Mamlaka ya usafiri wa Majini na nchi kavu (SUMATRA) imeyafungia mabasi 12 ya kampuni ya City boy kutokufanya safari zake kufuatia jana mabasi hayo mawili ya kampuni hiyo kusababisha ajali na kuuwa watu 30 eneo la Manyoni mkoani Singida.

Kwa mujibu wa Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida ACP Thobiasi Sedoyeka aliyekuwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo jana 04 Julai 2016 alisema kuwa ajali hiyo ilisababishwa na uzembe wa madereva kwa kuendesha kwa mwendo kasi na kufanya mzaha Barabarani

Mabasi hayo mawili ya City boy yalikuwa yakitokea Dar-es-Salaam kwenda Kahama na lingine likitokea Kahama kwenda Dar-es- Salaam,huku baadhi ya mashuhuda wakisema kuwa mbasi hayo baada ya kukutana yaliwashiana taa na kuanza kuya yumbisha kama ishara ya kusalimiana na hatimaye kugongana.

Chanzo: ITV
 
Hii ni rahisi sana,kinachofuata hapo ni kusajili kampuni kwa jina lingine,tena hili halikupaswa kusubiri kufungiwa kwani kwa tukio lile tayari image ya kampuni imechafuka hivyo hakukua na namna yoyote unaweza kwepa hilo.
Watabadili rangi na jina then wataendelea.
Hiki ndicho watakacho fanya vunginevyo wafuatiliwe vizuri,tusubiri!
 
Ukweli viongozi wetu wajaribu kuwa proactive na sio hizi ishu za kusubiri majanga halafu ndio waje na maamuzi. Taarifa zinazoenea ni kuwa madereva wa hiyo kampuni huwa wanasalimiana kwa utaratibu huo(ikimaanisha salamu hizo hazikuanza jana) je nikwanini hawakuwahi kuchukuliwa hatua toka mwanzo kabla ya hili kutokea? SUMATRA na police walikuwa wapi wakati wote huo?
 
Kampuni inamakosa gani? Kosa ni la mfanyakazi na si la tajiri.
Hii ni dalili ya kukosa pa kutokea wakaona wamwonee tajiri. Adhabu wanastahili askari wa usalama barabarani na madereva. Hawa madereva hasa wa Arusha-Kanda ya ziwa na makonda wao wanatafuna mirungi njia nzima mpaka macho yanakuwa mekundu lakini askari wanapotezea.

Kuadhibu kampuni ni kutafuta pa kutokea, ni uonevu, ni kukatisha tamaa wawekezaji, lichunguzwe na lirekebishwe kisheria/kikanuni/kimaamuzi.
 
Back
Top Bottom