SUMATRA walazimika kuruhusu magari madogo (daladala) kwenda mikoa mbalimbali ikiwemo Moshi na Arusha

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,804
2,000

Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA wamelazimika kuruhusu magari madogo maarufu daladala kwenda mikoa mbalimbali ikiwemo Moshi na Arusha baada ya idadi kubwa ya abiria kukosa nafasi kwenye mabasi makubwa.

ITV imefika kituo kikuu cha mabasi Ubungo na kushuhudia msongamano wa abiria huku wengine wakirudi nyumbani baada ya kukosa usafiri ambapo akizungumzia suala la kutoa vibali kwa daladala kwenda mikoani mkurugenzi wa udhibiti wa usafiri wa barabara SUMATRA Bw. Johansen Kahatano amesema wamefanya hivyo ili kusaidia abiria waliokosa huduma.

Wakizungumza na ITV baadhi ya abiria waliokosa usafiri wamedai kuwa walishindwa kukata tiketi mapema kutokana na kuona hakuna tatizo la usafiri tangu mwezi huu uanze hivyo wameshangazwa na hali waliyoikuta kituoni hapo.

Kufuatia uhaba huo wa magari baadhi ya wamiliki wa mabasi wametumia fursa hiyo na kutoa mabasi yaliyokuwa karakana kwa matengenezo ambapo baada ya kufanyiwa ukaguzi na askari yakaonekana kuwa na kasoro hivyo kuzuiliwa kuendelea na safari ili hali walikuwa wameshapakia abiria.

Wakati huo huo naibu kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Lucas Mkondya amewatahadharisha watumiaji wa barabara kutii sheria za usalama barabarani ili kuepuka kusherekea sikuu za mwisho wa mwaka mahabusu kwani kamera za usalama zitakuwepo kila kona ya jiji.
 
usser

JF-Expert Member
Sep 25, 2015
12,045
2,000
Wachaga tukigoma kusafir mwisho wa mwaka lazma zaid ya,mabus 100 yabak emty yakiwa yamepak tu kwa kukosa abiria
 
Mwasita Moja

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,906
2,000
Si chadema wanasema watu hawasafiri kwa sababu maisha magumu, magufuli amebana??

Kila hoja wanayodandia bavicha wanaishia kuaibika tu,

Shame on you bavicha shetani yupo upande wenu awamu hii.
 
Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,804
2,000
Si chadema wanasema watu hawasafiri kwa sababu maisha magumu, magufuli amebana??

Kila hoja wanayodandia bavicha wanaishia kuaibika tu,

Shame on you bavicha shetani yupo upande wenu awamu hii.
Mbona Ccm wenyewe wanadai hali ngumu ila ni kipindi cha mpito?
Na wengine wanasema zilikuwa ni fedha za ufisadi?
 
zithromax

JF-Expert Member
Apr 26, 2016
1,633
2,000

Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA wamelazimika kuruhusu magari madogo maarufu daladala kwenda mikoa mbalimbali ikiwemo Moshi na Arusha baada ya idadi kubwa ya abiria kukosa nafasi kwenye mabasi makubwa.

ITV imefika kituo kikuu cha mabasi Ubungo na kushuhudia msongamano wa abiria huku wengine wakirudi nyumbani baada ya kukosa usafiri ambapo akizungumzia suala la kutoa vibali kwa daladala kwenda mikoani mkurugenzi wa udhibiti wa usafiri wa barabara SUMATRA Bw. Johansen Kahatano amesema wamefanya hivyo ili kusaidia abiria waliokosa huduma.

Wakizungumza na ITV baadhi ya abiria waliokosa usafiri wamedai kuwa walishindwa kukata tiketi mapema kutokana na kuona hakuna tatizo la usafiri tangu mwezi huu uanze hivyo wameshangazwa na hali waliyoikuta kituoni hapo.

Kufuatia uhaba huo wa magari baadhi ya wamiliki wa mabasi wametumia fursa hiyo na kutoa mabasi yaliyokuwa karakana kwa matengenezo ambapo baada ya kufanyiwa ukaguzi na askari yakaonekana kuwa na kasoro hivyo kuzuiliwa kuendelea na safari ili hali walikuwa wameshapakia abiria.

Wakati huo huo naibu kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Lucas Mkondya amewatahadharisha watumiaji wa barabara kutii sheria za usalama barabarani ili kuepuka kusherekea sikuu za mwisho wa mwaka mahabusu kwani kamera za usalama zitakuwepo kila kona ya jiji.
lakini watu ni wanafiki sana kuna uzi uliokuwa huku ukisema mabasi mengi yamekosa abiria
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom