Sumatra uzi ule ule! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sumatra uzi ule ule!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by akili, Mar 29, 2010.

 1. a

  akili Member

  #1
  Mar 29, 2010
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SISI wakazi wa Dar na vitongoji vyake tunajua leo wenye daladala wameamua kufanya unyama wao na kuonyesha kukosa utu na ubinadamu wao. Tunaikubali shida hii ya leo, na tunawapa moyo SUMATRA kuwa sheria za nchi barabarani lazima zifuatwe.
  Tunataka wakati ufike watoto, wanafunzi, wazee, walemavu na wagonjwa waweze kusafiri bila hofu ya maisha yao au viungo vyao.
  Wafanyakazi wanaweza kufanya mgomo lakini athari zao zisije moja kwa moja kwa wananchi. Jamaa hawa, hata hivyo, wakifanya mgomo ni kwamba wanaharibu maisha yote ya kila siku ya mwananchi.
  Ni muhimu hata hivyo serikali kuwa na msimamo dhabiti na wakimabadiliko ikiwa ni pamoja na kuwadhibiti wale wote wanaogoma kila wakipata kisingizio.
  Tunaamini kwamba wakati umefika wa 'resourece redistribution' kwa maana wote wanaogoma basi wabaki na magari yao majumbani mwao na serikali iwawezeshe wananchi mitaani, kwenye kata na kwenye majimbo ya uchaguzi kumiliki daladala mpya, kubwa za kistaarabu kupitia kampuni zitakazoendeshwa kibiashara na katika utaalamu wa juu kabisa wa kiufundi na kimkakati hususan katika kufanya usafriri uwe wa raha, starehe na kistaarabu kote jijini na kufagia pembeni uchafu huu wa daladala binafsi zinazotuletea dhiki, wizi na vifo kila siku iendayo kwa Mungu.
  Ninaamini serikali ikiviwekea dhama vikundi binafsi vya watu mitaani, kwenye kata na kwenye majimbo ya uchaguzi tutawawezesha wananchi kumiliki miradi ya kuwapatia riziki yao ya kila siku na wakati huo huo kuwezesha kuwepo na usafri salama na ustaarabu zaidi jijini.
  Mgomo wa daladala safari hii utumike kama njia ya kusafisha barabara zetu ili zisiwe na daladala bomu, daladala zinazojali fedha kuliko utu, daladala zinatugeuza wananchi kuwa ng'ombe badala ya binadamu.....
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Mar 29, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  Kwanini mnaililia na kuipongeza Sumatra?
   
 3. jossey1979

  jossey1979 Senior Member

  #3
  Mar 29, 2010
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 168
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Have those guys gone on srike!! If so poleni sana wakazi wa Dar, Ninavyojua jiji letu hilo ni vigumu sana kwa watu wenye magari binafsi kumpa m2 lifti kutokana na sababu za kiusalama.
  Poleni sana.
   
 4. S

  SIPENDI Member

  #4
  Mar 29, 2010
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mimi kwa mtazamo wangu naona waendelee kugoma lakini pia kama serikali iko makini ifanye kitu ambachi kitawashangaza watu lakini kwa ajili ya manufaa ya watanzania. Mimi nadhani serikali ingetangaza tenda ya madereva kutoka nje ya nchi madhalan China. Tukiwa na madereva kutoka nje italeta mapinduzi hasa katika matumizi ya barabara.
   
Loading...