SUMATRA tunaomba mabasi Tabata-Sokoni hadi Kariakoo/Buguruni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SUMATRA tunaomba mabasi Tabata-Sokoni hadi Kariakoo/Buguruni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Iga, Oct 29, 2008.

 1. I

  Iga Senior Member

  #1
  Oct 29, 2008
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  SISI wakazi wa TABATA tumeanzishiwa soko jipya kati ya Tabata Shule na Muslim au Al Farouk lakini tatizo ni usafiri.

  Isitoshe kwa kuwa tuko karibu na mwisho kabisa wa Tabata kuelekea barabara kuu ya Mandela kila gari likija linakuwa limejaa na tunapata adha kubwa ya usafiri wa kuaminika na kustarehe kwa kukaa kila asubuhi iendayo kwa Mungu.


  Kwa hiyo tunaamini kwamba tukipata mabasi yaendayo sokoni Kariakoo na Buguruni kwanza yatatuondolea kusimama kila tunaposafiri asubuhi na pili soko letu litajaa bidhaa kwa kuwa wachuuzi hapo watakuwa hawana matatizo ya kuleta bidhaa toka masoko makubwa popote pale yalipo hapa jijini.

  Halafu nisisahau kuwa wakazi wengi wa Tabata sasa hivi wanafanya kazi maeneo ya Kinondoni na Beach ya Bahari ya Hindi.

  Mnaonaje basi tukiwekea na mabasi ya TABATA-KWANYERERE na TABATA- MWANANYAMALA na TABATA-KINONDONI AU MOROCCO???
   
Loading...