Sumatra tembeleeni bandari ya Dar mkaone wizi unaofanyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sumatra tembeleeni bandari ya Dar mkaone wizi unaofanyika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Manyanza, Jul 26, 2011.

 1. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kwa mara ya kwanza natoa shutuma zangu, nazielekeza kwa Mamlaka ya udhibiti Usafiri wa majini na nchi kavu (SUMATRA), kusema kweli hawa jamaa wamelala sana na kazi kubwa wanayofanya ni kukimbizana na makondakta na madereva wa daladala na wamesahau upande wa usafiri wa majini. Inasikitisha na inauma jinsi huduma hizi zinavyoendeshwa hasa kwa upande wa ukatishaji wa ticketi za kwenda visiwani Zanzibar, yaani wakala wa kukatisha ticketi wameingia tamaa wanauza ticketi zote kwa walanguzi na ukienda ofisini wanakwambia zimeisha lakini ukitoka nje ya ofisi zao wanakudaka wale walanguzi na kuanza kukuuzia ticketi kwa bei ya juu.
  Ticketi zinzuzwa kwa shilingi 25,000 na 35,0000 mpaka 40,000. Na bei ya ticketi ni shilingi 20,000 kwa boti za Azam na shilingi 15,000 kwa boti nyingine (itategemea unasafiri wakati gani)
  Kusema kweli hii inawaumiza sana wananchi wa kipato cha chini, na wale ambao huwa wamepanga bajeti ya safari halafu wanakuta bei imekuwa mara mbili zaidi. Na wakati mwingine huwa inatulazimu kukata tu ticketi kwa bei wanayotaka wao usipofanya hivyo na safari yako itakuwa imekufa na unaweza ukaghairi na kesho yake ukakuta mchezo uleule.
  Nawaomba SUMTRA walifanyie kazi hili suala maana limekuwa tatizo na mapolisi na wafanyakazi wote pale bandarini wanajua kila kitu lakini wamekua hawana response yoyote.
  Na ishu hii ya ulanguzi ipo sana kwa upande wa DSM, kwa Zanzibar haipo sana kama utataka kulanguliwa utakuwa umejitakia mwenyewe lakini ukienda ofisini hata kama boti bado dakika kumi kuondoka utapata ticketi bila wasiwasi. Lakini kwa DSM hata kama bado masaa matatu utaambiwa kwamba hakuna ticketi kwa sababu kuna wageni wengi sana wanaosafiri kwenda Zanzibar lakini walanguzi wanakua wanaziuza kwa bei kubwa huwa najiuliza wanazipataja hawa????
  SINAMENGI NAAMINI WADAU WATALIONA HILI NA KULIFANYIA KAZI
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,483
  Likes Received: 5,719
  Trophy Points: 280
  hivi na wewe unaamini kuna sumatra??haya si manungayepe ya serikali kuchota hela za uchaguzi na za kutatua matatizo yao madogomadogo kama uamini nenda kaulize safari zao wanavyolipana
   
 3. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  huwezi kuamini mkuu watu wanapata yabu sana pale bandarini wanavyopata tabu, jana jioni nilikuwa nakuja Zanzibar na nilikuwa na ndugu zangu watatu nilishindwa kuwalipia ticket maana ticket zilikuwa zinauzwa 40,000. kutoka 20,000.
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  kumbe usafiri wa kwenda zanzibar,aaah wafanye hata laki
   
 5. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Jamani, inchi kila kona inanuka michezo michafu siyo hapo tu!! Umelazimika kusema haya kwa sababu imekuuzi vya kutosha. Lakini nenda mahospitali( Ni vurugu tupu, utajuta kwenda bila hela kidogo ya nesi), nenda mashuleni ambako wanao wanasoma na unalipa ada( Hakuna mipango yeyote kila mwaka yale yale), nenda sehemu yeyote ile kama hawa jamaa wanaopanga bei za umeme ukiwepo, lakini mgao ukiwepo wanakaa kimyaaa, sema sehemu nyingine! kwa ufupi serikali ama imejitoa kabisa imebaki kupiga dili kama wananchi wavivu wanavyofanya au kuna tatizo kubwa la kiuongozi nchini kwetu ambapo pamegawanyika/pamemeguka kila sehemu.

  Nchi inakoenda siko, hakuna sehemu isiyokuwa na kashfa tena za kipuuzi. Mahakani ukienda, unapokewa na karani anakuuliza unataka nini unasema shida yako, anakuuliza una bei gani? Ukienda Uhamiaji nako hivyo hivyo! Hapo hapo hao watu wanalipwa mishahara lakini ujanja ujanja mwingi ambao ukidhibitiwa wengi wanakonda pengine hapa presha zitawapunguza.

  Tuendeleeni kupasa sauti, kwani sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, wataacha hiyo michezo michafu. Hakika hilo nalo ni neno, kwani ndo watanzania wengi tunaoamini hivyo.
   
Loading...