SUMATRA oyee, Kituo Cha Mabasi Ubungo Hata sijafuatwa kuniuliza Naelekea Wapii?

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
4,291
2,466
Yani Nasafiri Kwenda Nje Ya Dar, Nafika Kituo Cha Mabasi Ubungo Hata Sijafuatwa Na Mtu Kunighasi Na Kuniuliza Naelekea Wapi. Naingia Kituoni Na Begi Langu Hakuna Mtu Anayenifuata.

Naanza Kuangaza Kutafuta Mabasi Yanakoelekea Ninakotaka Wala Hakuna Mwenye Time Nami. Si Mimi Tu, Hata Kwa Abiria Wengine.

Inabidi Nianze Kujipendekeza Kuuliza Taratibu Za Usafiri, Napewa Jibu Pamoja Na Nauli Kulingana Na Daraja La Basi.

No Kubembelezana. Natafuta Basi La Hadhi Yangu Napanda Na Kusubiri Kuondoka. Njiani Tunasimamishwa Na Trafiki, Anaingia Ndani Ya Basi Sambamba Na Afisa Wa Sumatra, Anatusalimu Na Kutupa Somo La Usalama.

Naye Wa Sumatra Anatueleza Yake Ikiwa Ni Pamoja Na Bei Za Nauli. Anatupatia Na Namba Za Kutuma Sms Kuulizia Nauli Ya Kule Uendako. Naona Ni Jambo Jema Sana.

Kioo Cha Mbele Naona Kuna Bandiko La Sumatra Na Namba Za Simu Za Kupiga Bure Kwa Jambo Lolote La Dharura Au Kero. All In All, Hii Ya Kutobugudhiwa Hadi Napanda Basi Ni Kiboko.

Sijui Walitumia Njia Gani
 
Hebu nipe hiyo namba ya sumatra nataka kujua nauli ya dar arusha kwa bas
 
Muda si mrefu tutaishi kama watu. Maana ilifika mahali kila mtu anaishi atakavyo yeye hata sehemu za jumuiya
 
Viongozi wa nchi hii ni wa ajabu sana.yaani wanafanya kwa kumuogopa mtu/magufuli badala wafanye kazi kwa misingi ya sheria na taratibu za kazi zao.sheria ni zile zile bali wanasubiri kufanya kazi kwa kubustiwa.
 
Hebu nipe hiyo namba ya sumatra nataka kujua nauli ya dar arusha kwa bas
Unaandika Dar - Arusha Kisha Unatuma Kwenda 15276. Utatumiwa Majibu, Ila Utakatwa Kiasi Cha Hela. Kama Si 150 Ni 300
 
Sasa waboreshe vituo vya mabasi viwe na hadhi za kimataifa kwani mabasi hupandwa na watu wa Mataifa mbali mbali.

Hebu linganisha kituo chetu cha mabasi chochote kile na hivi vya kimataifa:
main0808.jpg

&NCS_modified=20151102142458&MaxW=640&imageVersion=default&AR-151109797.jpg

ADG_BusTerminal_01_web_square.jpg
 
yaani elikuwa kero kukatiza hapo ubungo hata kama si msafiri wanakuja watu sio chini ya kumi
ni bora wamiliki wa gari sasa wanzishe e- bus ticketing
 
Katika mtihani mzito hapo stand ilikuwa ni huo wa kufuatana fuatana na ukizubaa utapewa tiketi ya basi jingine na kupandishwa jingine, hongera kwa waliohusika
 
Back
Top Bottom