Sumatra na usimamaizi mbovu wa vyombo vya usafiri - hasa mabasi

terabojo

JF-Expert Member
Aug 3, 2010
215
45
Wana JF, kutokana na ajali za kila siku za mabasi ya safari ndefu na dala dala mijini na hii ya meli zanzibara ninaomba nitoe hoja ifuatayo:

SUMATRA ambao ni wenye jukumu la kusajili kutoa leseni na kusimamia usafiri wa nchi kavu na majini (hasa kwa bara) ni wavivu na wanafanya kazi zao kwa kulipua lipua tu. Mfano mdogo nji kwa dala dala za Dar es Salaam. Ukitembeleea maeneo ya mbagala mwisho - Big Boni na rangi tatau utakuta magari yanyoanzia safari zake kwende sehemu za pepmebezoni yotte kwa muenekano hayafai kuwa barabarani - iwe tairi; bodi; na hata madereva wa magari hayo. Mengi hayana bima na maderva hawana leseni.

Kwa mabasi ya safari za mikoani nashindwa kuelewa kwa nini SUMATRA hawaweki utaratibu wa kudumu wa kukagua ubora wa basi kila baada ya muda fulani (utakaowekwa kitaalamu). Kwa mfano watengenezaji matairi wameweka kiwango cha matumizi ya tairi kwa maana ya kutembea kilomita kadhaa na hivyo SUMATRAakiawa makini wanaweza kuweka kumbukumba na kuwabana wamiliki wabadilishe matairi naka kadhalika.

Badala ya kuweka mkakati na utaratibu wa utendaji kazi kwa faida ya abiria na hata wamiliki wao wanakalia kutoza kodi (ambazo wanazitumia kujiongezea mishahara na marupurup kibao); na kusubiri ajali zitokee wapate sababu ya kuweka opersheni maalum kwa muda na kujitangaza ktk vyombo vya habari.
Nawakilisha
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom