RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Mamlaka ya Usafiri wa nchikavu na Majini (SUMATRA) ikishirikiana na Jeshi la Polisi nchini wamekamata mabasi 105 yenye makosa mbalimbali na mabasi 36 yamefikishwa Mahakamani ili kujibu tuhuma zinazo wakabiri.
Hayo yamesemwa na Afisa Mawasiliano wa Mamlaka ya Usafiri wa nchikavu na Majini (SUMATRA), David Mziray wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa Madereva na Makondakta wa mabasi hayo wamefikishwa katika mahakama za Kinondoni na Ilala jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa kutokana na Operesheni inayofanywa na
Mamlaka ya Usafiri wa nchikavu na Majini (SUMATRA) ikishirikiana na Jeshi la Polisi nchini imekuwa ikibaini baadhi ya madereva wanaokiuka Masharti ya leseni ya Kusafirisha abiria na wengine kutokuwa na leseni ndio maana wameona kuchukua hatua hiyo ya kukamata na kuwapeleka mahakamani madereva na Makondakta wanao kiuka masharti ya leseni zao.
Pia amewaasa wamiliki wa mabasi na wafanyakazi wakiwemo madereva na Makondakta wa mabasi ya Daladala kuzingatia masharti ya Leseni za usafirishaji wanapotoa huduma ya usafirishaji kwa umma na wananchi kwa ujumla wamewaomba kutoa ushirikiano pale ambapo wanaona madereva wanakiuka masharti ya reseni za usafirishaji, kuongeza nauli, kukatisha njia au kutumia njia ambayo haijapangwa na Mamlaka ya Usafiri wa nchikavu na Majini (SUMATRA).