Sumatra kusitisha huduma za daladala mojamoja Dar

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
kilima+sumatra.jpg
Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Ahmad Kilima


Kwa ufupi
“Kuanzia Juni 30, mwaka kesho, mamlaka itasitisha uendeshaji wa leseni kwa mmiliki mmoja mmoja anayetoa huduma katika barabara zilitotajwa” alisema Kilima.




MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), itasitisha utoaji wa leseni mpya za usafirishaji wa abiria katika Jiji la Dar es Salaam kwa mmiliki mmoja mmoja kuanzia Desemba Mosi mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Ahmad Kilima, ilisema hatua hiyo inatokana na kushauriana kati ya Sumatra, wamiliki wa Daladala, Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi (Dart) na wadau wengine.

Wakati wa mkutano wa kukusanya maoni uliofanyika mwanzoni mwa mwaka 2010 ,baadhi ya wamiliki wa daladala walipinga utaratibu huo kutokana na uwezo wao kifedha kuwa mdogo wakihofia kuwa kuwaathiri.

Walisema huduma ya usafirishaji kupitia kampuni, inalenga katika kuwaondoa kabisa katika biashara hiyo.

Baadhi ya wamiliki waliomba kuwepo kwa elimu ya kutosha kwa wamiliki juu ya mfumo huo mpya kabla ya kuanza kuutekeleza.

Katika taarifa yake, Kilima alisema safari ambazo zitasitishiwa utoaji wa leseni ni za Barabara ya Kilwa kuanzia Mbagala kwenda katikati ya Jiji na maeneo mengine.

Barabara nyingine ni ile ya Ali Hasani Mwinyi kuanzia Mwenge kwenda maeneo ya katikati ya jiji.

“Kuanzia Juni 30, mwaka kesho, mamlaka itasitisha uendeshaji wa leseni kwa mmiliki mmoja mmoja anayetoa huduma katika barabara zilitotajwa” alisema Kilima.

Alisema kwa wale ambao leseni zao zinaisha kabla ya Juni 30 mwaka kesho, mamlaka itaendeleza leseni zao kwa kuwapa leseni za muda mfupi zinazoishia Juni 30 mwakani.

“Katika kipindi cha kuanzia Desemba mosi mwaka huu hadi Juni 30 mwaka kesho, wasafirishaji wanaotoa huduma katika njia hizo, wanashauriwa kujiunga na kuanzisha makampuni au ushirika ili waweze kupewa leseni za kutoa huduma kuanzia Julai Mosi mwaka kesho,” alisema.

Alisema vigezo na masharti ya leseni za usafirishaji yatazingatiwa katika utoaji wa leseni hizo mpya.

Katika mkutano huo, Sumatra ilisema hali ya utoaji huduma katika jiji hairidhishi kutokana na kutokuwepo kwa utaratibu wa wamiliki kuwasimamia madereva na makondakta.
 
Back
Top Bottom