Queen V
JF-Expert Member
- Jan 19, 2012
- 776
- 1,330
Mwaka jana mwezi wa 7, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alitoa Marufuku ya kufanyika kwa mikutano ya kisiasa nchini na kwamba siasa hadi 2020.
Kama hiyo haitoshi, mwezi Novemba, 2017 Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) ilipiga Marufuku abiria kuzungumza siasa, dini, biashara ndani ya basi!
SUMATRA ilisema kuwa atakayebainika kufanya vitendo hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Agizo hilo lilikuja baada ya kudaiwa kuwapo kwa mvutano wa kupinga kanuni mpya kati ya SUMATRA na Chama cha Wamiliki Mabasi yaendayo Mikoani (TABOA) na Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri Dar es Salaam (UWAMADAR).
Bila kutaja ni sheria na kanuni ipi, Mkurugenzi wa SUMATRA amesema ufanyaji wa vitendo hivyo katika mabasi ni kinyume na kanuni za usafirishaji.
Wanasiasa wengine(maana wapo wanaofanya siasa hata kwenye mikutano isiyo ya chama) wamekatazwa kufanya siasa nchini maana mikutano na maandamano ya kisiasa ndio chachu ya ukuaji wa kisiasa.
Wananchi tumekatazwa kujadili siasa pia. Je Siasa zimemilikiwa na Chama/ Watu fulani?