SUMATRA/Jeshi la Polisi kagueni mabasi machafu ya Mkoani

Masulupwete

JF-Expert Member
Feb 15, 2012
2,366
2,397
Msiishie kuangalia kama gari ni zima na ina kibali cha route husika. Mkague na usafi wa mabasi.

Kuna magari unaingia hapo ndani hadi unajisikia kichefuchefu kwa jinsi yalivyo machafu. Halafu fikiria ndo utakaa humo kwa kutwa zima. Come on guyz, tupo uchumi wa kati sasa, lazima tubadilike.

Siku si nyingi niliingia basi moja ya Dodoma-Dar (leo sitalitaja) ilinilazimu kuendelea tu na safari kwa sababu tayari nilikuwa na tiketi mkononi, nilikata tiketi bila kuona hilo basi lenyewe.

Makochi ya basi ni machafu utafikiri umeingia kilabu cha kuuza mataputapu halafu bei zao ni zile zile za kwenye ubao. Hapo unapoenda kuweka kichwa chako huwezi kupatazama mara mbili, pachafu kama nini.

Muwashauri wasiweke makochi ya nguo maana nguo zina kawaida ya kunyakua kila aina ya uchafu kirahisi badala yake watumie canvasi.
 
LATRA Na Jeshi La Police
Siku Hizi Sumatra Imevunjwa Ikawa
LATRA Na TASAC
...Umelonga kweli Mkuu Masulupwete! Gari linakuwa.kama shimo LA Takataka! Kondakta mchafu kama amelala kwenye mataputapu!
Wenye mabasi jiongezeni, msijue kupokea nauli ya abiria tu!
 
Kwasaaa Ni Shida Sasa Dodoma Kunatakiwa Bus Safi Siyo Unatoka Kwenye Bus Utafikiria Umepanda Kutoka Kigoma 😏😑
 
Waanze na Saibaba lile la Mchana Dar to Moshi/Arusha.
Hilo basi waliache kabisa,linatusaidia sana sie watorokaji kazini siku ya Ijumaa na kurudi dar jumapili jioni,Wenye kulijua hilo basi wanaliitaga Zoazoa ikifika mchana na ukalikosa hilo basi yaani hapo inakubidi tu ulale kama ni Moshi ama Arusha
 
Mkuu unamaanisha lisisumbuliwe (in makondaz voice) hata kama linajaza chawa, viroboto na kunguni kwa sababu nyie linawasitiri au?

Huna maslahi apo mkuu?
 
Kwasaaa Ni Shida Sasa Dodoma Kunatakiwa Bus Safi Siyo Unatoka Kwenye Bus Utafikiria Umepanda Kutoka Kigoma
Usalama si kwenye mabasi tu, yaangaliwe magari yote. Sijui kwenye majiji, mikoani kuna magari yatembea utadhania kuna taka zinachomwa moto nyuma yake. Yanatoa moshi nyuma gari halionekani.
 
Mkuu unamaanisha lisisumbuliwe (in makondaz voice) hata kama linajaza chawa, viroboto na kunguni kwa sababu nyie linawasitiri au?

Huna maslahi apo mkuu?
Hapo umemjibu vyema.. inawezekana hajui kwamba, kupanda/kutumia basi safi na salama ni haki yake kwa kuwa analipa nauli halali.
Nakumbuka miaka saba iliyopita nilianzisha valangati pale Ubungo bus terminal baada ya kupanda basi chafu, cha ajabu abiria wakaanza kunishambulia kwa maneno.. eti nawachelewesha,mara ningepanda ndege.. nilikomaa mpaka likasafishwa.
Ila nilijifunza kwamba, watanzania bado tuna safari ndefu sana kufikia maendeleo chanya.
 
Msiishie kuangalia kama gari ni zima na ina kibali cha route husika. Mkague na usafi wa mabasi.

Kuna magari unaingia hapo ndani hadi unajisikia kichefuchefu kwa jinsi yalivyo machafu. Halafu fikiria ndo utakaa humo kwa kutwa zima. Come on guyz, tupo uchumi wa kati sasa, lazima tubadilike.

Siku si nyingi niliingia basi moja ya Dodoma-Dar (leo sitalitaja) ilinilazimu kuendelea tu na safari kwa sababu tayari nilikuwa na tiketi mkononi, nilikata tiketi bila kuona hilo basi lenyewe.

Makochi ya basi ni machafu utafikiri umeingia kilabu cha kuuza mataputapu halafu bei zao ni zile zile za kwenye ubao. Hapo unapoenda kuweka kichwa chako huwezi kupatazama mara mbili, pachafu kama nini.

Muwashauri wasiweke makochi ya nguo maana nguo zina kawaida ya kunyakua kila aina ya uchafu kirahisi badala yake watumie canvasi.
champion ilo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom