SUMATRA, basi la Skyline linatuibia abiria kwa kututoza nauli tofauti tofauti

Mar 16, 2015
75
28
Basi la skyline linalofanya safari zake kutoka Dar kwenda Arusha (T335 DGB). linatuibia abiria wake kwa kututoza nauli tofauti wakati wote tunaelekea sehemu moja..

Mfano mimi wamenicharge 32800, kuna mtu nimepanda nae yeye kalipa 18000, kuna dada amelipa 30000 mwingine yupo nyuma yangu kalipa 25000.. halafu wote tunaelekea Moshi.

Hii ni kinyume kabisa na sheria na utaratibu ambao kila siku sumatra mnatuambia .. ila leo nimewaambia kupitia simu ila naona hakuna hatua mliyoichukua hadi sasa, chukueni hatua haraka inavyotakiwa maana wajibu wangu wa kutoa taarifa nimeshautimiza na nyie timizeni wajibu wenu ... Naambatanisha na tiketi hapa chini

Msisubiri mpaka Rais aje ofisini kwenu maana najua mtausoma ujumbe huu...
 
Yani wewe unalipa nauli yote hiyo kipindi hiki??
Au wewe ni mshamba wa kusafiri??

Vitu vingine ni vyakupambana sisi wenyewe ndugu!
 
Kwani nauli halali ni kiasi gani? Huyo aliyelipa ndogo huenda anaelewa soko, au anaweza kuzungumza (negoatiate skills) au katoa kubwa lakini kaandikiwa ndogo.
 
kweli wewe wakuja yaani umetoa nauli 32000 kwenda Moshi/Arusha?hata liwe basi gani silipi zaidi ya 20,000.
 
Sumatra inatakiwa kufumuliwa na kusukwa upya ifanane na awamu hii, hawa watu muda mwingi wamejifungia maofisini huku abiria wakiumizwa, nashindwa kuelewa kwanini simu yao namba 00800110020 huwa haipokelewi, haieleweki wanamhudumia nani kama hawataki kupokea simu za wateja
 
Kupitia simu yako ya mkononi sasa unaweza kupata viwango vya nauli na madaraja ya mabasi ya kwenda mkoani
Tuma neno
NAULI
UNAKOTOKA
UNAKOENDA
tuma ujumbe huo kwenda namba 15276
Mfano
"NAULI DAR MWANZA" send to 15276
utapokea ujumbe wa viwango vyote vya nauli kwa kila daraja la basi
 
Basi la skyline linalofanya safari zake kutoka Dar kwenda Arusha (T335 DGB). linatuibia abiria wake kwa kututoza nauli tofauti wakati wote tunaelekea sehemu moja..

Mfano mimi wamenicharge 32800, kuna mtu nimepanda nae yeye kalipa 18000, kuna dada amelipa 30000 mwingine yupo nyuma yangu kalipa 25000.. halafu wote tunaelekea Moshi.

Hii ni kinyume kabisa na sheria na utaratibu ambao kila siku sumatra mnatuambia .. ila leo nimewaambia kupitia simu ila naona hakuna hatua mliyoichukua hadi sasa, chukueni hatua haraka inavyotakiwa maana wajibu wangu wa kutoa taarifa nimeshautimiza na nyie timizeni wajibu wenu ... Naambatanisha na tiketi hapa chini

Msisubiri mpaka Rais aje ofisini kwenu maana najua mtausoma ujumbe huu...
Aisee hawa jamaa sio msaada kabisa, juzi mimi pia nililipishwa nauli kubwa kuzidi inayotakiwa nikaripoti kwenye namba yao iliyotolewa kwenye vipeperushi lakini hakuna kilichofanyika mpaka nahisi huenda kwa kuripoti huku tunakuwa tunawapa dili watu wa SUMATRA wanawatafuta wenye magari na kumalizana kishkaji badala ya kuwapiga ile faini ya 250,000/-..
Cha kufanya kuanzia sasa ni kuwa wabishi kwenye magari na ikiwezekana ukipanda basi lipa nauli elekezi na watangazie abiria wote kuwa nauli elekezi kutoka A mpaka B ni shilingi kadhaa, kama kuna alielipa zaidi akukabidhi tiketi na mkifika popote penye askari mtoe lalamiko kwa pamoja mtasaidiwa (ikishindikana chukueni hatua mkononi mumuadhibu mwizi huyo)..mimi juzi nimepigwa nauli hiyo nikategemea nitasaidiwa kwa kuripoti lalamiko langu SUMATRA na TRAFIKI MAKAO MAKUU ambapo sikusaidiwa na nimejifunza kutokana na makosa sitakubali kupigwa tena kizembe
 
Back
Top Bottom