SUMA JKT wachukue tenda ya sukari

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,185
18,513
Inavyo onekana wafanya biashara wa sukari wanataka kupima nguvubya serikali kwa kutumia pesa nyingi walizo nazo.

Kama mtu anaweza ficha tani elfu 4 ina maana anaweza nunua sukari yote ya kiwanda na akaificha.

Kwa kuwa serikali inajua viwanda vyote vya sukari na imepunguza sukari kwa manufaa ya viwanda hivyo basi
1. Serikali iingie mkataba na viwanda vyote juu ya uwazi wa watu wanao nunua sukari kuhakikisha inawafikia watumiaji

2. Serikali ifanye mpango wa kuiwezesha suma jkt kujihusisha na bidhaa hii

3. Serikali itoe adhabu kali kwa mfanya biashara yoyote atakaye patikana ana sukari wakati watu wanatafuta sukari. Kinacho takiwa mfanyabiashara auze stock yake yote kama demand ipo .
 
serikali ikiamua inaweza mimi nashauri waanze kwanza na hawa hawa wanaificha kitu cha kwanza waende viwandani ili kubaini mlolongo mzima wa sukari tangia pale inapotoka viwandani kwenda kwa hao walanguzi wakubwa kisha waangalie leja za hao walanguzi mm naamin sukari bado ni nying sana nchi hii.
lakini pia serikali ivunje hii bodi ya sukari koz hakuna wanachosimamia kama mtu atalangua tani 5000 na kukaa nayo na bodi imekaa kimya na wasijue la kufanya adi takukuru ndo waingilie kati sioni umuhim wao
 
Unataka kusema Tanzania kuna bodi ya sukari? kama ipo basi ni jipu?
 
tatizo huu mfumo wa kukabidhi watu binafsi baadhi ya mambo nyeti ndio yanatutokea puani now
 
Mi najiuliza kitu kimoja, ivi mara baada ya kiwanda kuzalisha hawa walanguzi wanakuja kuchukua sukari yote.
Kwa sababu kama production ni continuous process why watafute walioficha badala ya kwenda tu kiwandani na kuona namna ya kufanya kwenye new produced sugar?
 
Labda tu niipongeze serikali ya awamu ya tano kwamba sasa imeanza kuamka.
Ninaiomba iwachukulie hatua kali wote watakaobainika kuhodhi sukari kwenye ghala zao kwa nia ya kujipatia faida kubwa huku wananchi wanateseka. Ningeishauri serikali kuwa umefika wakati sasa kwa wafanyabiashara wanaotumia pesa zao, na hasa wenye asili ya ki asia, pale wanapobainika tu na makosa ya uhujumu uchumi, na mengine makubwa ya jinsi hiyo wafutiwe uraia wao huo wa kujianfikisha na wafukuzwe nchini mara moja na kuzuiwa kurudi nchini.
Huwa nakumbuka kisa cha mgiriki Stein aliyefukuzwa nchini na Baba wa Taifa baada ya kuiweka serikali mfukoni hawatofautiani na hawa wanaotumia pesa yao kuvuruga juhudi za JPM.
Hawa wakatwe tu. Hivi majuzi ktk gazeti moja la kila siku ilielezwa kuwa mmiliki wa Q Consult anatumia pesa zake kurubuni watendaji wa mradi wa coco, kwa jeuri anayoitoa wapi? Japo mada ni tofauti lkn ni mifano dhahiri inayoitukanisha serikali kwa wananchi wake. Wapewe repatriation ndipo wengine watakoma. Pamoja na ubazazi wa Iddi Amin "Dadah" wa Uganda, mimi binafsi nilipongeza hatua ya kuwafukuzilia mbali wa asia. Leo hii walioko Uganda wana "ADABU"
 
kama jkt ni jeshi la kujenga taifa basi lianzishe mashamba ya miwa badala ya kufanya uchuuzi wa sukari. pia watengeneze matrekta na siyo kuuza power tiller.
 
wawe na mashamba ya miwa na viwanda waache kuuza yale matrekta yanang'aa utadhani prado...matrekta ya wapi yale..
 
wawe na mashamba ya miwa na viwanda waache kuuza yale matrekta yanang'aa utadhani prado...matrekta ya wapi yale..

Itolewe amri kama alivyo toa kwa mashirika ya hifadhi kazi ya jkt na magereza iwe ni kilimo
 
Suma JKT wajipange kwanza... mambo yao bado hayajanyooka sana.... kuna ujeshi/ uraia hv kutengeneza confusion kwenye utendaji wao...
 
Back
Top Bottom