Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,602
Niliwahi kuandika hapa jukwaani na ntazidi kuandika. Ukitaka kukuza uchumi wa nchi tengeneza mazingira ya watu kujisikia wapo huru, hawabughudhiwi, wanajiskia kutendewa haki, hata uzalendo wa watu kwa nchi yao unakuwa mkubwa endapo mtu unahisi kwamba unatendewa haki. Na hi ina apply hata kwa wafanya biashara na wawekezaji, confidence ikipotea huwa wanakuwa na kawaida ya kuficha mitaji yao na hata shughuli za kuuchumi kwenye hizi nyakati huwa zinadorora.
Kipindi cha hayati Magufuli, confidence iliondoka yote kwenye uchumi, matokeo yake investiment ikashuka halafu ikapelekea money supply kutokuongezeka kwa kasi inayotakiwa ukiangalia hata credit growth ilikuwa ndogo mno. (pitia moja post zangu kuhusu hili utaelewa vizuri: Tuweke kumbukumbu zetu sawa, huu ndo uchumi wa Magufuli aliouacha, all facts! - Sehemu ya kwanza).
'Suluhunomics'
Naweza mpaka sasa kusema uongozi wa Rais Samia ni kama umeleta confidence kubwa sana kwenye uchumi, nimejaribu kuangalia money supply growth na credit growth kwa mwezi April, umeongezeka kwa kiasi kikubwa sana, hata kwenye upande wa ajira, ndani ya hii miezi mitatu kumetangazwa ajira nyingi sana upande wa private sekta, kwa watafutaji wa ajira mpya mtakubalina na mimi ni vile tu nchi yetu ina bahati mbaya huwa hai track hizi indicators na hili moja kwa moja nalitupa kwa wizara ya fedha na idara ya takwimu.
Na haya yote yanatokea kwa bajeti ile ile ya Magufuli, yaani mabadiliko yanaonekana kwa action za Rais za kuamua kutokuwa na roho mbaya na wivu na roho ya husuda.
Endelea kupiga kazi, Rais Samia najua wewe ukiendelea kuwa Rais hii nchi haki itaonekana, wengine sisi huwa tunapenda tu kuona tunaishi kwa haki na usawa.
Suala la katiba mpya mama pia ni la muhimu sana kwa uchumi wetu, kuna visheria vya kijinga kama ile ile sheria ya 'Anti-money laundering act' unatakiwa ufanye namna uiondoe maana ndio mambo yanatuwekea kiwingu na kushusha uwekezaji kutoka nje.
N.Mushi