'Suluhunomics' kwa miezi mitatu tayari karejesha confidence kwenye uchumi 'Bishana na namba'

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
4,520
2,000
Niliwahi kuandika hapa jukwaani na ntazidi kuandika. Ukitaka kukuza uchumi wa nchi tengeneza mazingira ya watu kujisikia wapo huru, hawabughudhiwi, wanajiskia kutendewa haki, hata uzalendo wa watu kwa nchi yao unakuwa mkubwa endapo mtu unahisi kwamba unatendewa haki. Na hi ina apply hata kwa wafanya biashara na wawekezaji, confidence ikipotea huwa wanakuwa na kawaida ya kuficha mitaji yao na hata shughuli za kuuchumi kwenye hizi nyakati huwa zinadorora.

Kipindi cha hayati Magufuli, confidence iliondoka yote kwenye uchumi, matokeo yake investiment ikashuka halafu ikapelekea money supply kutokuongezeka kwa kasi inayotakiwa ukiangalia hata credit growth ilikuwa ndogo mno. (pitia moja post zangu kuhusu hili utaelewa vizuri: Tuweke kumbukumbu zetu sawa, huu ndo uchumi wa Magufuli aliouacha, all facts! - Sehemu ya kwanza).

'Suluhunomics'
Naweza mpaka sasa kusema uongozi wa Rais Samia ni kama umeleta confidence kubwa sana kwenye uchumi, nimejaribu kuangalia money supply growth na credit growth kwa mwezi April, umeongezeka kwa kiasi kikubwa sana, hata kwenye upande wa ajira, ndani ya hii miezi mitatu kumetangazwa ajira nyingi sana upande wa private sekta, kwa watafutaji wa ajira mpya mtakubalina na mimi ni vile tu nchi yetu ina bahati mbaya huwa hai track hizi indicators na hili moja kwa moja nalitupa kwa wizara ya fedha na idara ya takwimu.

uchumi.JPG


Na haya yote yanatokea kwa bajeti ile ile ya Magufuli, yaani mabadiliko yanaonekana kwa action za Rais za kuamua kutokuwa na roho mbaya na wivu na roho ya husuda.

Endelea kupiga kazi, Rais Samia najua wewe ukiendelea kuwa Rais hii nchi haki itaonekana, wengine sisi huwa tunapenda tu kuona tunaishi kwa haki na usawa.

Suala la katiba mpya mama pia ni la muhimu sana kwa uchumi wetu, kuna visheria vya kijinga kama ile ile sheria ya 'Anti-money laundering act' unatakiwa ufanye namna uiondoe maana ndio mambo yanatuwekea kiwingu na kushusha uwekezaji kutoka nje.

N.Mushi
 

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
4,520
2,000
Samia kalegeza hali, ndani ya miaka miwili naamini mambo yatakuwa mazuri zaidi, angemalizia na Katiba Mpya ningempa zawadi.
Hata katiba mpya isipokuja sasahivi kama akitaka kuendelee kuwa na fairness mambo lazima yawe mazuri mno ndani ya miaka miwili.. mimi nimemuelewa sana.. hata hii ya kuchukua hatua dhidi ya Covid-19 ni mkakati wake wa ku win diplomasia ya kimataifa, maana kwa tulipofikisha na Magufuli tulikuwa tunaonekana Tanzania ni kama mtoto mtukutu
 

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
4,520
2,000
Tatizo walimpitisha jpm ili wamshinde Lowasa wakasahau madhaifu yake na sisi walipa kodi!!ona sasa ilivokula kwetu mazima!!aiseh jiwe ni hatari sana!!!
JK hakuamini macho yake, aliipata joto ya jiwe vema.. laiti mda ungekuwa unaweza kurudishwa nyuma wangefanya todauti
 

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
4,520
2,000
Sijui lengo kabisa la jiwe adi leo kwenye kukuza uchumi!!!!
Magufuli hakuwa na idea ya namna ya kukuza uchumi, possibly ni kwa sababu hakujipanga... Mwisho wa siku akaona namna ya kukuza uchumi ni ku dump pesa zote kwenye ujenzi wa miundo mbinu.

Anyway, japo miundo mbinu itatusaidia baadae ila kosa kubwa la Magufuli ni ku discourage private sekta kwa kuleta ubabe... Uchumi hautakagi ubabe
 

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
4,520
2,000
Magufuli alikua anatupeleka kwa shimo refu sana kiuchumi
Nadhani tulikuwa ndo tunaanza kuporomoka, uongozi wa Magu umekomea maali ambapo ni critical sana.... Hata yeye nadhani alishaanza ku give up na kuchoka... Unapojigundua umefanya blunders halafu unakuwa mgumu wa kula matapishi yako, kinachofuata ni ku give up
 

blogger

JF-Expert Member
Mar 13, 2012
5,334
2,000
Magufuli alikaa pale Ikulu 5+ years...
Akashindwa rekebisha maslahi ya wafanyakazi.

MAMa ndani ya siku mia kapandisha madaraja..

Ee Mungu Baba tulindie Rais huyuu..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom