Suluhu ya kudumu ktk sector ya elimu nchini

chichimizi

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
1,074
1,500
TUTAFUTE SULUHU YA KUDUMU KWA TATIZO LA WAALIMU NCHINI.

Kashasha

[HASHTAG]#Hadi[/HASHTAG] kufikia mwaka 2014 tulikuwa na shule za msingi Tanzania 16,343.Shule hizi kwa pamoja zilikuwa na idadi ya wanafunzi zaidi ya milioni 8 hadi kufikia 2014.

[HASHTAG]#Baada[/HASHTAG] ya Elimu ya msingi kuwa bure udahili kwa mwaka jana umeongezaka ambapo walioandikishwa darasa la kwanza mwaka 2016 ni 1, 896, 000. Idadi hii imeongezeka kwa zaidi ya wanafunzi 614,000.

[HASHTAG]#Akisoma[/HASHTAG] Hotuba ya Bajeti ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015 mjini Dodoma,waziri wa elimu wakati huo Dr Shukuru kawambwa alisema nchi ilikuwa inakabiliwa na uhaba wa waalimu wa shule za msingi 30,949. Hapa Tunazungumzia uhaba kabla ya Mpango wa Elimu bure kuanza ambapo umeongeza idadi ya wanafunzi. Tukumbuke idadi ya waalimu tunaowahitaji unakwenda sambamba na idadi ya wanafunzi waliopo shuleni.

[HASHTAG]#Mwaka[/HASHTAG] jana Ripoti ya Haki elimu ilikuja na tafiti inayozungumzia mafanikio na changamoto zinazoikabili Elimu ya bila malipo nchini. Katika ripoti ile wanadai kuwa kwa sasa baada ya mpango huu kuanza mwalimu mmoja anahudumia wanafunzi 164 badala ya wanafunzi 45 kitaalamu (1:45).

[HASHTAG]#Kwa[/HASHTAG] maana hiyo kwa ratio hiyo elimu ya msingi pekee inahitaji waalimu 200,000 kama idadi ya wanafunzi kwenye shule zetu6 itakuwa milioni 9 tu. Ukitumia Ratio hiyo ya Twaweza ya 1: 164 yaani mwalimu mmoja wanafunzi 164 utaona kuwa idadi ya waalimu waliopo nchini kwa sasa ni waalimu 54, 878. Kwa hiyo ili ratio ya kitaalamu ikidhi haja tunapaswa kuajiri zaidi ya waalimu 145,000 wa shule za msingi tu hapa ndipo utapata ratio ya 1:45 ambayo inahitajika kitaalamu.
6
[HASHTAG]#Serikali[/HASHTAG] inadai itawapunguza waalimu wa sekondari wa sanaa waliozidi kwenye shule za sekondari waende kufundisha shule za msingi ili kulipunguza tatizo. Akijibu swali bungeni Mh Ndalichako mwaka jana alidai kuwa ni kweli shule za sekondari zina upungufu wa waalimu wa sayansi huku waalimu wa masomo ya Sanaa wakiwa na zidio la waalimu 7,888.

[HASHTAG]#Mwaka[/HASHTAG] jana huo huo Naibu katibu mkuu wa Tamisemi ndugu Bernad Makali mwaka jana aliiambia kamati ya bunge (PAC) Kuwa kuna zidio la waalimu wa sanaa 7,463 idadi hii haitofautiani sana na Idadi ya Mh Waziri.

Je waalimu hawa 7, 888 au waalimu 7,463 wanaweza kumaliza tatizo la upungufu wa waalimu 145,000??? Jibu ni kwamba haiwezekani.

[HASHTAG]#SERIKALI[/HASHTAG] IFANYE NINI SASA.

Kwanza naipongeza Serikali kwa uamuzi huu wa kuwapunguza waalimu wa sanaa katika shule za Sekondari.

Aidha waalimu hawa walikuwa wakipata6 malipo ambayo hayaendani na kazi wanazozifanya huku wale wenzao wa shule za Msingi wakitaabika kweli kweli.

[HASHTAG]#Lakini[/HASHTAG] pia Serikali iangalie inawezaje kumaliza tatizo hili kwa kuweka solution ya kudumu. Swala la kuajiri waalimu waliopo mtaani hili halikwepeki kwa kuwa pamoja na upungufu niliouonyesha kwa miaka mitatu ya Nyuma bado idadi ya wanafunzi wanaosajiliwa kuanza Darasa la Kwanza inazidi kuongezeka huku waalimu wakipungua kutokana na Sababu mbalimbali kama vile vifo, na kustaafu.

Vivyo hivyo kwa kuwa waalimu wa sanaa watapunguzwa toka Sekondari baada ya Muda tatizo la uhaba wa waalimu kwa shule za Sekondari utajitokeza tena upya.

#Ni vizuri serikali ikaangalia uhitaji halisi wa waalimu kwa ngazi zote huku wakiangalia wanaostaafu miaka 5 ijayo.

Elimu ni kitu sensitive sana kinachohitajika kupewa kipaumbele cha kipekee sana.
 

kluger

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
2,098
2,000
Suluhu ni ngumu kupatikana, kwa sababu viongozi wanatumia kundi hili la walimu kisiasa zaidi, huo ni mtaji wa chama fulani cha siasa !
 

Kingdavi.ii

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,180
2,000
Tatizo ni sera tamko na atakachotamka waziri ndiyi Sera ya Elimu badala ya kufuata taraitibu na sheia/miongozo ya Elimu.
Ni vyeama tukawa na Sera bora ambayo haiwezi badilishwa na waziri badala take tuwe na time ya kusimamia Elimu na walimu kwani walimu wanatumika kisiasa mfano ni chama chao cha cat.
Nb
Kila mmoja wetu anawajibu was kuhakikkisha wabafunzi na wananchi wanapatiwa Elimu bora kupitia Sera bora badala ya sare na bora Sera
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom