Suluhu: Tunawaomba wasanii mjipange kuhamasisha wananchi kupigia kura ya ndiyo Katiba Pendekezwa

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,906
2,885
Siasa ni mchezo wa sanaa leo nimesikia rais kawaita makundi mbalimbali ya wasanii yaliyowasaidia wakati wa kampeni ili kuyapongeza ukweli ni kwamba rais na timu yake wanajua fika kua uchaguzi umeisha lakini wana kibarua kikubwa zaidi mbele yao cha kupigia kampeni katiba pendekezwa hivyo waliitwa ili wawekwe sawa kiakili
 
Wananchi wengi wamekatishwa tamaa na uchaguzi uliopita; Nategemea wachache watajitokeza kupiga kura & ndio ushindi wa CCM. Otherwise, sijui njia ipi itumike kuwahuisha tena ili wawe na mawazo kama ya kipindi kile cha Warioba.
 
Mbona heading ya topic haiendani na kilichoandikwa ndani?

Mh. Suluhu kayasema hayo ya kupigia chapuo wananchi wapige kura ya ndio kwenye huo mkutano?
 
Na hapa ndipo ninapopata shaka na dhamira njema ya JPM kwa hii Nchi, mi nadhani ili Nchi inyooke kama anavyotaka basi aruhusu rasimu ya warioba na sio ile ya Chenge na wenzake, huku kutumbua majibu kutakuwa na faida mpk kizazi kijacho kama kutaachwa mipango mizuri ndani ya Katiba jinsi ya kushuhulika na walafi wa mali za umma, lkn hii ya kufanya mtu kwa akili zake na ubabe hauna mwisho mzuri........
 
Ccm ni ile ile hawa wasanii watatumika kwa kiwango chao kazi ukiisha watabaki kulalamika mwananchi ni muda mwafaka wa kuamua kwa akili yako na si ya kushikiwa
 
Posible mimi naweza kuwa niko vizuri kichwani kuliko Vice na hata Presidaa mwenyewe.kuna mambo ni aibu
 
Ni mwendawazimu pekee ndo anayeweza kushawishiwa na kina kigosi, Jb na timu ya warembo, masikini magu anafikiri amechukua urais kwa urahisi kwaajili ya hawa wauza sura.
 
Wewe
Wananchi wengi wamekatishwa tamaa na uchaguzi uliopita; Nategemea wachache watajitokeza kupiga kura & ndio ushindi wa CCM. Otherwise, sijui njia ipi itumike kuwahuisha tena ili wawe na mawazo kama ya kipindi kile cha Warioba.

Wewe usiwakatishe tamaa wananchi. Kura tutapiga na tutaikataa katiba pendekezwa kwani haina Ibara muhimu zilizoko kwenye rasimu ya Jaji Warioba. Ibara kama za mbunge asiwe waziri, mgombea binafsi, kura za rais zihojiwe mahakamani, wabunge wazembe wawajibishwe na wapiga kura wao. Tume ya uchaguzi iwe huru na rais asiteue wajumbe nk.ni lazima zirudishwe kwenye katiba pendekezwa vinginevyo tupigie kura ya NO.
 
binafsi katiba sitaipigia kura maana hata nikiipa NO wataipa YES kura yangu haina maamuzi kwa kile sisiem walichopanga
 
Kichinjio changu nili kihifadhi kwa ajili ya kura za maoni ya rasimu ya katiba ya Warioba ,wasipo kuja na hiyo rasimu ya Warioba ,hichi kichinjio nakichimbia kaburi na ndio utakua mwanzo na mwisho wa kupiga kura
 
Kama wataleta hiyo Katiba yao pendekezwa sitakaa nipige kura nchi hii milele na milele...
 
Back
Top Bottom