Suluhu mgogoro wa Arusha ni kurudia uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Suluhu mgogoro wa Arusha ni kurudia uchaguzi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 11, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  TUMELAZIMIKA kurudia wito tulioutoa kwa Serikali juzi kwamba suluhisho la mgogoro wa umeya katika Jiji la Arusha unaweza kutatuliwa iwapo tu uchaguzi utarudiwa kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa kisheria.

  Tumelazimika kufanya hivyo kwa sababu mbili kubwa: Kwanza, ni kauli zinazokinzana ambazo zimetolewa na viongozi wa chama tawala na serikali yake kuhusu suala hilo. Tunadhani kuwa kauli hizo kamwe haziwezi kuleta suluhisho la tatizo hilo.

  Wakati Serikali ikisema kuwa mgogoro huo ni wa kisiasa, hivyo sharti umalizwe kisiasa, Katibu Mkuu wa chama hicho kinachounda serikali hiyo, Yusuf Mkamba anasema na kusisitiza kwa sauti kubwa kuwa mgogoro huo ni wa kisheria, hivyo ni mahakama tu inayoweza kuutatua.

  Pili, kitendo cha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana kuanza kuchukua hatua za awali za kushughulikia mgogoro huo kimetupa matumaini kuwa pengine huo ni mwanzo wa safari ya kuelekea kwenye maridhiano kati ya vyama vya CCM na Chadema kwa njia ya mazungumzo badala ya kwenda mahakamani kama anavyotaka Makamba.

  Habari zinasema kwamba Waziri Mkuu huyo, akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha jana walikutana na IGP, Said Mwema ili kubaini ukweli kuhusu ushiriki wa polisi katika kuzima maandamano ya wafuasi wa Chadema yaliyofanyika mjini Arusha Jumatano iliyopita. Habari zinasema pia kuwa Waziri Mkuu Pinda anatafuta namna ya kukutana na viongozi wa Chadema ili kuwasikiliza kabla ya kupiga hatua nyingine katika juhudi zake za kufanikisha maridhiano.

  Sisi hatuna shaka yoyote kuhusu dhamira na nia njema ya kiongozi huyo kutaka mgogoro huo umalizwe kwa maridhiano na kwa kutoa haki kwa pande zote zinazokinzana. Tumekuwa tukisisitiza mara nyingi kwamba unyenyekevu wa kiongozi huyo ni silaha kubwa inayowafanya wananchi wamuelewe na kumpenda. Kwa kutokuwa mbabe, Waziri Mkuu Pinda anazo sifa za kutatua migogoro, na nadharia ya migogoro inaelekeza kuwa mtu wa namna yake huweza kupatanisha pande zinazokinzana kwa haraka na pasipo gharama kubwa.

  Wakati tukiungana na Serikali kwa kusema kuwa mgogoro huu ni wa kisiasa, hivyo lazima umalizwe kisiasa, tunaishauri Serikali kuwa itakuwa imetenda haki kwa pande zote mbili iwapo itaamuru kurudiwa kwa uchaguzi huo. Ikumbukwe kwamba kiini cha mgogoro huo ni hatua ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kukiuka kwa makusudi kanuni na taratibu za uchaguzi wa meya wa jiji hilo, ikiwa ni pamoja na kutowashirikisha madiwani wa Chadema katika uchaguzi huo.

  Kulipeleka suala hilo mahakamani ni kudhalilisha mahakama kwa kuzigeuza vyombo vya michezo ya kisiasa. Mahakama zetu zimezidiwa na mlundikano wa kesi, na tunaweza kusema wanaotaka suala hilo liende kule wanataka kuchelewesha muda kwa kujua kwamba hukumu yake haitatoka leo wala kesho. Ndio maana tunashauriwa kuwa tusipeleke kule kesi ambazo zinaweza kumalizwa na vyombo vingine, tena katika muda mfupi, vikiwamo vya usuluhishi.

  Tunatoa angalizo kwa Waziri Mkuu Pinda kuwa tunaposhauri kuwa uchaguzi huo wa meya urudiwe, tunataka usiwepo uwezekano wa kuifanya halmashauri hiyo ya Arusha isiongozwe na vyama vya CCM na Chadema kwa zamu kwa kisingizio cha kufurahisha kila upande. Yafaa ieleweke kwamba hali ilikuwa hivyo katika Halmashauri ya Kigoma-Ujiji baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 kwa sababu vyama hivyo vilikwenda suluhu kwa idadi sawa ya madiwani.

  Kwa upande wa viongozi wa ngazi ya juu wa vyama hivyo, tunawashauri mchukue tahadhari kubwa kabla ya kutoa matamshi kuhusu mgogoro huo. Tunadhani kuwa kauli za Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, kwa mfano, zimekuwa hazijengi bali zinabomoa juhudi zinazofanywa na viongozi wa serikali ambayo inaundwa na chama chake, kuwa ngumu.
   
 2. Kahema

  Kahema JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2011
  Joined: May 21, 2010
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  na uchaguzi wa rais urudiwe basi, au kwa sababu hajafa mtu? maana kama swala ni wizi hata jk aliiba kura nani asiye jua?
   
 3. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Haki inapatikana mahakamani pekee.
  Naungana na Mh Makamba kwamba anayeona hakutendewa haki, akaitafute mahakamani.
  Chadema wamekuwa msitari wa mbele kutumia mahakama katika mambo mengi. Inashangaza katika hili wanaburuza miguu.
  Nadhani wanaona kuwa hakuna tija.
  Na wewe mtoa mada unasingizia kuwa itakuwa ni kuilundikia mahakama kazi .... bla bla...
  Lakini ukumbuke kuwa hilo ndilo jukumu la msingi la vyombo vya sheria.
  Suala la kesi kuchukua muda mrefu si hoja pia kwani waweza kufungua kesi na kuomba isikilizwe kidharura....chadema wanalijua hilo vizuri.

  The bottom line is: Nendeni mahakamani, kama hamtaki kaeni kimya na kumwacha Mstahiki Meya aliyechaguliwa kihalali afanye kazi tulizomtuma.

  Tumechoshwa na kelele za kipuuzi.
   
 4. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Amechaguliwa na nani? Mtachoshwaje na kelele mnazoanzisha? Wangeshindwa kihalali wangenyamaza. Waambie wenzako mliochoshwa muache kuiibia Tanzania hamtapigiwa kelele na awaye yeyote :rip:
   
 5. s

  shemu Member

  #5
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 15
  Kishongo kweli wewe nimpenda amani? Kama nikweli basi inabidi ukubaliane na mtoa hoja usilete ushabiki wa kisiasa kwenye mambo ya msingi kama haya labda kama unapenda kuona damu inaendelea kumwagika jambo ambalo siyo utamaduni wa Mtanzania. Kuiba waibe kwenye watu wengi lakini kwa wachache ambao hata mtoto mdogo akiona au kusikia anajua wamechakachua!? Heeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!
   
Loading...