Suluhisho Tutapata Lini

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,201
219
Miongoni mwa jamii ambazo mawazo yake ni rahisi kutambulika na kufunikwa ni jamii za kitanzania , kutokana na uzoefu nilionao katika kusoma hoja na mada zingine nyingi za watanzania sehemu nyingi tu katika mitandao , radio , magazeti , simu na nyingi zingine za kutolea habari .

Nasema ni rahisi kutambulika kwa sababu wengi wao kazi yao ni kulalamika tu bila kuleta suluhisho la hayo malalamiko yao au dukuduku lao , ni maajabu sana kumkuta mtaalamu wa barabara analeta mada katika mtandao kulalamika barabaa Fulani mbovu au imejengwa vibaya bila kutoa fikira mbadala ya nini kifanyike eneo lile na maeneo mengine aliyoyataja yeye .

Pia ni kawaida kuona mwanafunzi analeta dukuduku lake kuhusu masuala ya vyuoni mwao katika mitandao na magazeti kulalamika bila yeye kusema amefanya jitihada gain kuhakikisha walau amejaribu kuielimisha jamii au kundi la watu anao waandikia .

Hata usione ajabu kwa mtaalamu wa kilimo na afya akija kulalamika kuhusu idara zao za kazi jinsi wanavyochelewesha kazi , malipo wanavyolipwa , usumbufu mwingine katika idara hizo bila kutoa suluhisho la nini kifanyike kazi kulalamika tu mpaka mwisho .

Siamini kama kulalamika ndio njia pekeee ya kutatua matatizo na mambo mengine yaliyokuwa katika jamii husika , nashauri wengi wanaotoa mada , hoja na makala zao sasa waanze kurasa maalumu za kutoa suluhisho la nini kifanyike kuhusu malalamiko yao

Au kama wanahitaji msaada wa kitaalamu zaidi ni bora waulize kabla hawajaanza kutoa malalamiko yao katika magazeti na mitandao mbali mbali kama hawatafanya hivyo na kuendelea kulalamika tu basi watakuwa wanaikosea heshima jamii inayowaznguka jamii ambayo ina uchu wa kuelimishwa na kujulishwa vitu na mambo yanaendaji katika nchi yao .

Ndugu watanzania , watoa maoni , waandishi , wahariri , wasomaji na wachangiaji mbali mbali ,sasa tukilalamika tutoe na suluhisho la nini kifanyike kutokana na malalamiko yetu kama ni kitu cha kitaalamu zaidi jaribu kuonana na wataalamu ili wakushauri na kukupa msaada zaidi kabla ya kutoa malalamiko yako .

Hii itasaidia kadi na uwajibikaji wa haraka kwa watuhumiwa wa kitu kilichotajwa .
Ahsante
 
Back
Top Bottom