Suluhisho rahisi kwa wanaodhani wamepungukiwa nguvu, wanaosumbuka kurudia tendo au kuwahi kufika

Asante sana Mkuu kwa hekima zako, Umeeleweka vizuri, Ikikupendeza mkuu naomba uzipe maelezo kidogo point zako kwa msaada zaidi kwa wengine wetu. Labda mtu azingatie vyakula gani apunguze/aache vipi, labda unaposema kukosekana ka lugha moja unamaanisha nini na pia unapozungumzia mazingira ya mpambano (unamaanisha labda kuzoeleka kwa mazingira au usafi wake au uzuri wake)

Many thanks

1. Kuwa makini na baadhi ya aina ya vyakula...
Chakula humfanya mwanadamu aendelee kuishi kwani hubeba nishati na virutubisho vya madini vyenye kupelekea uboreshaji wa afya ya mwili.

Wataalamu wa masuala ya ngono na vichocheo mwilini hupendekeza aina fulani fulani za vyakula ambavyo kama mwanaume akipendelea kula basi huongeza 'libido'.

Baadhi ya vyakula hivi ni kama komamanga, parachichi, mvinyo mwekundu, chaza na pweza, tikiti maji na mbegu zake, chokoleti, pilipili, tangawizi n.k

2. Kukosekana kwa lugha ya aina moja ya kimapenzi baina ya mume na mke...
Miili huwa inaongea haswa linapokuja suala la ngono baina ya mwanaume na mwanamke...
Si watu wote wenye uwezo wa kutafsiri lugha hii ingawaje kila mmoja wetu amejaaliwa kuwa na uwezo wa kutambua.
Kwa wanaume walio na uzoefu wa kutongoza kwa ishara ni wepesi sana kuwaridhisha wanawake kuliko wale wanaume wenye kutumia vitendo zaidi.
Kwa kawaida tongozo huwa halina ukomo haijalishi wewe ni mume au mke (yes namaanisha mwanaume aliyeoa au mwanamke aliyeolewa), ngono nzuri ni ile ambayo matokeo yake ni hutokana na mume au mke kumtongoza mwenzake.

3. Mazingira ya eneo la mpambano na usafi wa mwanamke...
Mazingira ya utulivu na usafi maridhawa ni jawabu tosha la matokeo ya ngono nzuri yenye utulivu pia.
Mwanaume huwezi kuwa na mawazo straight ya kingono katika mazingira ambayo bado unajiona ni stranger hata kama ni nyumbani kwako, mathalani unahofia jirani atakuja kugonga kuomba chumvi n.k

Pia usafi na matunzo ya mwili wa mwanamke kwa kiasi kikubwa huamasisha au hufifisha matamanio ya kingono.

Many thanks Mkuu Sibonike. Nimeipenda point yako ulivyoichambua haswa swala la UBINAFSI. Hahahahahaa all about GIVING sio!!!!
Mwenye kufahamu na afahamu ulichonena hapa.

Mkuu suala zima lipo kwenye mental pride kama ulivyoainisha - kujiweka katika hali ya kuona kuwa tendo ni la kawaida. Naunganisha hilo na signature yako ''Happiness doesn't result from what we GET, but from what we GIVE'' Dr. Ben Carson.
Nasema hivyo kwa sababu mara nyingi kwa kwa kutojua mwanaume huwa selfish kwenye tendo lenyewe. Anamaliza yeye bila kujali mwenzake kama kafika au la. Mwanamke asiporidhika anaweza kumtangazia mwanaume kuwa hana uwezo na akijua anakosa confidence. Tayari inaingia kichwani kuwa hawezi na anabaki na hali hiyo. Suluhisho? kumridhisha, kuliko kujiridhisha kwanza!
 
Last edited by a moderator:
changia kwa niaba yangu

Haya ngoja nichangie kidogo,ila mambo mengi karibu yote mkuu Tized na Watu 8 wamemaliza.

Kuna jambo dogo sana lakini wengi wanalipuuzia na linawaathiri wanaume wengi bila kujua nalo ni maneno ya vijiweni,kumekuwa na maneno mengi kwamba mwanaume aliyekamilika lazima aende sijui raundi 3 na kuendelea,mara aliyekamilika lazima awe na inch 6,mara sijui style hii mwanaume akifanya lazima mwanamke akuheshimu.

Sasa basi mwanaume anapokutana na mwanamke kimwili anakuwa na matarajio meng kichwani pake kutokana na yale maneno ya vijiweni alosikia anaposhindwa kutimiliza hayo huanza kujiona yeye hafai au labda ana tatizo,hofu hujengeka moyoni mwake tayar hapo ndo mwanzo wa tatizo,hana ujasiri anapokutana na mpenzi wake unakuta hata mshindo mmoja tu inakuwa tabu sana.

La muhimu kila mmoja ajielewe ana uwezo gani,wote hatujaumbwa kulingana,kama wewe uwezo wako ni kimoja kisha ndo upite muda ndo uendelee kubali hali yako boresha hiyo hali yako na mtu wako naye afurahi,yaweza kuwa single but heavy,kama wewe sijui inch 4 jikubali ulivyo boresha hali yako utaona mambo ni mazuri,jua style unazozimudu usisikie maneno ya mtaani,wote hatulingani kuna anayekimbia mita 100,200,400 na wengine marathon lakini siye wote ni wanariadha,kila mmoja aridhike na uumbaji aliopewa aboreshe mazingira yake atafurahia maisha.

Lingine la mwisho naona hapa mmekazia swala la usafi kwa mwanamke ni kweli kabisa ke anahusika sana,ila hata nyie baadhi yenu me ni wavivu sana kuoga,unakuta mwanaume katoka kwenye shughuli zake za mchana kutwa anafikia kukutana na mwanamke hata haogi moja kwa moja kwenye makamuzi,mwili hujapata hata refreshment hapo game likiwa mbaya anajiona mpungufu kumbe tu hajaruhusu mwili nao upate ahueni.
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana na wewe Mkuu Ndibalema!

Visingizio vimekua vingi sana vya kwa nini hawafanyi mazoezi lakini pia uvivu umechangia sana kama ulivyosema.
Wengi pia wala ile akili bado kuwa mazoezi ni ya watu wagonjwa au wanaotaka kupunguza mwili kitu ambacho hata jamii yenyewe ndio inaona hivyo.

Inafaa sasa watu waamke watafute muda wa kufanya mazoezi iwe ni alfajiri au usiku. Mbona watu wanakesha Bar au Club hadi asubuhi vizuri tu? kwani kabla ya kwenda kupumzika ukipasha viungo moto au ule muda wa kuamka ukarudisha nusu saa nyuma si tayari una muda? Kwa nini mwanaume mzima alale hadi saa mbili/tatu asubuhi amesahau nini usingizini? watu wanaamka hata weekend mapemaa hao wapo kwenye mazoezi mbali mbali na mabonaza n.k. Nafikiri tutakapo amua kuacha visingizio singizio tutasaidika zaidi.

Asante Mkuu
Yoote yaliyoelezwa ni ya msingi sana lakini kwa kukazia tuu, swala la mazoezi ni muhimu zaidi pengine kuliko yote hapo.

Siku hizi vijana wamekuwa wavivu sana kufanya mazoezi ndio maana mikiki mikiki kadhaa tuu mtu limi nje kama jibwa.
Alafu fasta unakimbilia kumtafuta mzizimkavu akuelekeze dawa za kuongeza nguvu na kunenepesha uume.
 
Last edited by a moderator:
Hahahaaaaa.. Sasa Mkuu Mtambuzi kwa kuwa nyani mzee amekwepa mishale mingi sana, yafaa sasa utupe siri uliotumia mkuu kudumu na mama ngina haswa kwenye nyanja hizo ili vijana wako tupate shule mkuu!!! (tufaidi utambuzi wako)

Tized, Wanaume wangezingatia haya uliyoyasema hapa hakika wasingekimbilia kununua MKUYATI
 
Last edited by a moderator:
Haya ngoja nichangie kidogo,ila mambo mengi karibu yote mkuu Tized na Watu 8 wamemaliza.

Kuna jambo dogo sana lakini wengi wanalipuuzia na linawaathiri wanaume wengi bila kujua nalo ni maneno ya vijiweni,kumekuwa na maneno mengi kwamba mwanaume aliyekamilika lazima aende sijui raundi 3 na kuendelea,mara aliyekamilika lazima awe na inch 6,mara sijui style hii mwanaume akifanya lazima mwanamke akuheshimu.

Sasa basi mwanaume anapokutana na mwanamke kimwili anakuwa na matarajio meng kichwani pake kutokana na yale maneno ya vijiweni alosikia anaposhindwa kutimiliza hayo huanza kujiona yeye hafai au labda ana tatizo,hofu hujengeka moyoni mwake tayar hapo ndo mwanzo wa tatizo,hana ujasiri anapokutana na mpenzi wake unakuta hata mshindo mmoja tu inakuwa tabu sana.

La muhimu kila mmoja ajielewe ana uwezo gani,wote hatujaumbwa kulingana,kama wewe uwezo wako ni kimoja kisha ndo upite muda ndo uendelee kubali hali yako boresha hiyo hali yako na mtu wako naye afurahi,yaweza kuwa single but heavy,kama wewe sijui inch 4 jikubali ulivyo boresha hali yako utaona mambo ni mazuri,jua style unazozimudu usisikie maneno ya mtaani,wote hatulingani kuna anayekimbia mita 100,200,400 na wengine marathon lakini siye wote ni wanariadha,kila mmoja aridhike na uumbaji aliopewa aboreshe mazingira yake atafurahia maisha.

Lingine la mwisho naona hapa mmekazia swala la usafi kwa mwanamke ni kweli kabisa ke anahusika sana,ila hata nyie baadhi yenu me ni wavivu sana kuoga,unakuta mwanaume katoka kwenye shughuli zake za mchana kutwa anafikia kukutana na mwanamke hata haogi moja kwa moja kwenye makamuzi,mwili hujapata hata refreshment hapo game likiwa mbaya anajiona mpungufu kumbe tu hajaruhusu mwili nao upate ahueni.

Mkuu Tized angalia hoja ya everlenk hapo kwenye red. Nadhani anakomelea issue ile ile kwamba kitu kimeingia kichwani na inakuwa shida kubwa.

Mwanamke mwenye uelewa anaweza kumsaidia kumuweka sawa mwanaume mwenye tatizo hili. Lakini kumpata wa aina hiyo ni suala lingine!
 
Hahahaaaa... Sasa mkurugenzi wa Mabazazi tupe basi moja mbili tatu unazotumia huko kemp kumudu foleni ya wake wotee hao na hio michepuo ya ubazazini bila sisi kusikia manung'uniko humu kwenye suala zima la utoshelevu.

Bora mkuu umetoa elimu sawia kwa hawa wala chips na mazoezi hawafanyi
 
Nimempata sana, everlenk amepigilia msumari wa moto sana apo. yuko vizuri aisee!!!

Nakubaliana na wewe 100 kw 100 mkuu Sibonike. Dada zetu wajue nao wana wajibu wa kutuweka vizuri na wajue lawama sio nzuri hata kidogo kwenye mahusiano. na pia wasitegemee kila watachosikia kwenye magroup yao kipo kwa kila mwanaume. Kila mtu ni tofauti na kipekee. wasitulinganishe linganishe.

Mkuu Tized angalia hoja ya everlenk hapo kwenye red. Nadhani anakomelea issue ile ile kwamba kitu kimeingia kichwani na inakuwa shida kubwa.

Mwanamke mwenye uelewa anaweza kumsaidia kumuweka sawa mwanaume mwenye tatizo hili. Lakini kumpata wa aina hiyo ni suala lingine!
 
Last edited by a moderator:
Nimempata sana, everlenk amepigilia msumari wa moto sana apo. yuko vizuri aisee!!!

Nakubaliana na wewe 100 kw 100 mkuu Sibonike. Dada zetu wajue nao wana wajibu wa kutuweka vizuri na wajue lawama sio nzuri hata kidogo kwenye mahusiano. na pia wasitegemee kila watachosikia kwenye magroup yao kipo kwa kila mwanaume. Kila mtu ni tofauti na kipekee. wasitulinganishe linganishe.

Mkuu Tized angalia hoja ya everlenk hapo kwenye red. Nadhani anakomelea issue ile ile kwamba kitu kimeingia kichwani na inakuwa shida kubwa.

Mwanamke mwenye uelewa anaweza kumsaidia kumuweka sawa mwanaume mwenye tatizo hili. Lakini kumpata wa aina hiyo ni suala lingine!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom