Suluhisho ni kujiuzuru na kuwapisha wenye uwezo wa kufanya kazi wafanye | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Suluhisho ni kujiuzuru na kuwapisha wenye uwezo wa kufanya kazi wafanye

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Apr 21, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  French novelist Emile Zola once wrote"If you shut up truth and bury it under the ground,it will but grow,and gather to its self such explosive power that the day it burst through it will blow up everything in its way"Nimeanza na nukuu hii kutokana na hali ya nchi yetu inavyo jidhihirisha ndani ya utawala wa serikali inayojiita sikivu ya CCM.Ukweli unajaribu kuzikwa ama kupuuzwa na mawaziri katika kuitafuna nchi yetu ni bomu zaidi ya scud ambalo hata kama itafanyika jitihada ya kutmia patriot ni msaada wa Mungu tu ndiyoutakaoweza kunusuru.

  Huwezi kuwadanganya watu wakati wote,na ikitokea ukafanikiwa ipo siku watagundua na kukufanya adui wao namba moja.Watanzania wamechoshwa na ufisadi unaofanywa na watu waliopewa dhamana ya uongozi.Hatukuwapa fursa ya kujitajirisha kwa rasilimali zetu na kama kasungura ni kadogo lazima tugawane wote na kufaidi keki hiyo ya taifa.Kitendo cha CAG kutoa ripoti yake na kutokuchukuliwa hatua imeongeza kiburi kwa mawaziri wa serikali hii na kutoa majibu ya kejeli.Namaanisha tungekuwa na utamaduni wa kuwajibishana kila mmoja angetimiza wajibu wake na kusukuma gurudumu la maendeleo mbele.Watendaji wameipa kisogo nchi kazi iliyo baki ni kutafuna mali ya umma bila huruma.

  Kelele hazitoshi kwa wabunge,kinachoatakiwa ni azimio,na kama spika ni kikwazo tusome kanuni barabara naye awajibishwe kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye.Sipendi staili hii ya bunge kuacha kazi yake ya kuisimamia serikali na kuwa vinara wa kuitetea serikali,kama kuna mgawo mnaoupata wabunge kutokana na mchwa hawa wasio na huruma kuna haja gani ya kuwa na wawakilishi wa aina hii?Na shauri waziri mliopatikana na tuhuma hizi kaeni pembeni kama kweli mnamheshimu aliyewateuwa kuliko kuja kudhalilishwa na wananchi tutakapo ingia barabarani.Haitaji kupima,Watanzania tumeshapima tumeona mnastahili kuchukua maamuzi kuliko kuwalazimish kuachia ngazi.:target:
   
Loading...