Suluhisho la usugu wa changamoto katika utoaji wa huduma za kijamii

Twalib Mtoli

New Member
Jul 15, 2021
1
0
Kushindwa kukamilika kwa wakati katika miradi mbalimbali yamaendeleo na kusuasua kwa utoaji wa huduma kwa ufanisi pamoja na kukosekana kwa ufanisi na weledi katika kusimamia na utoaji wa huduma hizo ni moja kati ya changamoto kubwa nchini.

Moja kati ya sababu inayopepelekea kutokea kwa hali hii ni mfumo uliopo ambao ni ngumu kumuunganisha kiongozi wa juu (mwenye mamlaka ya kuwawajibisha wa chini) au viongozi wa idara mbalimbali katika ngazi ya juu na jamii ambayo ndio watu wa chini na wapokea huduma.Viongozi wa juu wana nguvu kubwa katika kuwawajibisha watendaji wa chini na wasimamizi wao.

Kauli za Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, mawaziri au wakuu wa idara pekee baada ya kutokea changamoto katika utoaji wa huduma katika taasisi zenye kuhumia umma hazitoshi kuhakikisha kuwa changamoto zimefanyiwa kazi na mapungufu yameondoshwa ili jamii ipate huduma bora kwa ufanisi.

Baadaya kiongozi wa juu kutoa kauli za onyo au makememeo au maelekezo kwenda ngazi ya chini ambako tatizo limeonekana au kutokea..Ni nani ana jukumu la kuhakikisha kuwa tatizo husika limekoma au kufanyiwa kazi?.je, ni mtendaji wa chini(mtekelezaji) peke yake au pamoja na mwananchi(mpokea huduma)

Kumeshuhudiwa kuwa maelekezo mengi au kauli za viongozi katika ngazi ya juu juu ya kurekebisha au kuondoa mapungufu hupoteza nguvu baada tu ya kusikika au hufanyiwa kazi ndani ya muda mfupi baada ya kutolewa.Mara nyingi hali hurejea tena kama mwanzo na kufanya matatizo na changamoto katika ustawishaji wa huduma za kijamii kuwa sugu.

Suluhisho hapa ni kuwepo kwa mfumo wa mawasiliano ya moja kwa moja kati ya viongozi wa juu na wananchi ambao watakuwa wanatoa mrejesho wa moja kwa moja bila kuwahusisha watendaji wa chini ambao mara nyingi ndio chanzo cha changamoto, utendaji mbovu, kero , ukiukwaji wa maelekezo pamoja na kukosa weledi na ufanisi.

Watendaji hawa wa chini wanaweza kudanganya kwa namna moja au nyingine katika ripoti zao kuelekea kwa wakuu wa idara ili kukwepa kuwajibishwa baada ya kushndwa kuyafanyia kazi maelezo kutoka kwa wakuu wao.Sababu za kushindwa huku kunaweza kuwa kuwa na maslahi binafsi katika mfumo wa sasa au utegeaji wa majukukmu yao ya msingi.

Kunaweza kubuniwa namba za simu, tovuti au applications mbalimbali ili kuwawezesha wananchi kupeleka malalamiko au kueleza matatizo,kero na changamoto kwenda kwenye ngazi za juu moja kwa moja.Suala la msingi ni uongozi wa juu kufanya uchunguzi kwanza kabla ya maamuzi juu ya mrejesho uliotoka kwa umma au tarifa kuhusiana na tatizo husika.
 
Back
Top Bottom