SoC02 Suluhisho la ukosefu wa ajira Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

Dr maduka

New Member
Sep 11, 2021
2
4
Suluhisho la ukosefu wa ajira Tanzania.

Utangulizi;

Ukosefu wa ajira imekuwa tatizo kubwa Sana kwa nchi zinazoendelea na nchi yetu Tanzania ikiwa miongoni. Tatizo linaanzia kwa mfumo wa elimu unaowaandaa vijana wasomi namna ya kuja kukabili hii hali ya ukosefu wa ajira imekuwa haina tiba yoyote. Maana kwa Sasa tuko na wasomi wengi walioko mtaani wamekaa bila kuzalisha chochote ili hali Taifa limepoteza na linaendelea kupoteza rasilimali nyingine kuandaa wasomi watakaokuja kukaa mtaani bila kuingiza chochote, kwa kuwa mfumo wetu wa elimu unaowaandaa wasomi kuja kuwa tegemezi wa ajira pekee na serikali haina uwezo wa kuwaajiri wote.

Juhudi nyingi zinafanyika kupunguza wimbi hili la wasomi wasio na ajira lakini hazijafua dafu Wala kiwa mwarobaini sahihi wa kitatua matatizo haya. Mfano Kuna viongoz wa serikali wakiulizwa kuhusu ukosefu wa ajira watasema ajira kweli hazipo ila vijana wakajiajiri wenyewe. Hapo maswali mengi yanakuja "watawezaje kujiajiri bila kuwa na mitaji?"

Kwa sababu mtu anatumia miaka 16-18 akiwa shuleni na hii inamaanisha anatoa pesa tu bila kuingiza halafu mwisho wa siku unamwambia akajiajiri kweli?

Kwa kiasi kikubwa serikali inataka kuachia kampuni za michezo ya kubashiri jukumu la kuajiri vijana maana kunauwiano wa vijana Saba Kati ya kumi wanategemea michezo ya kubashiri Kama chanzo kikuu Cha kujitengenezea kipato. Kwa staili hii tunaenda kutengeneza taifa la watu tegemezi na wasioiishia kesho yao.

Kwanza matabaka huanza kutengenezwa kuanzia kidato Cha nne, pale wanaofeli mitihani kuonekana hawafai na waliofaulu wanaonekana Ni Bora zaidi. Lakin hata kwenye familia huwezi kuta watoti wote watakuwa vizuri darasani ila huwezi kuwatenga na kwanyanyapaa. Tabaka la pili kidato Cha sita wale wanaofeli pia huonekana siyo kitu, na nafasi yao katika jamii hupotea kabisa.

Ukiunganisha wanafunzi wanaofeli kidato Cha nne na Cha sita unakuta Ni zaidi ya asilimia 60 ya wanafunzi wote, hii idadi yote inaenda kukaa Mitaani bila ajira, asilimia 40 itaenda vyuoni ila hata wakimaliza wote Ni chini ya asilimia 10 tu ndo wanaopata ajira.

Hivo tunakuwa tumetengeneza zaidi ya asilimia 90 ya darasa lote kuwa mitaan bila ajira pamoja na wale waliopambana kufikia juu ila bado wanakuwa hawana tofauti na waliokomea chini. Hi Nicole kwa mwaka mmoja na Kila mwaka tunazalisha aina hi ya watu, hapo utatuzi wa suala la ukosefu wa ajira haliwezi kuwa rahisi.

Dhima;
Baada ya kufanya uchunguzi na kuangalia vijana wengi walioko mtaani ambao wameweza kuhimili maisha bila kuajiriwa , nligundua wengi wako na ujuzi mbalimbali, na ujuzi huu wengi wameupatia katika vyuo vya VETA. kutokana na hali hiyo ilipalekea Mimi kuja na suluhisho litakalosaidia kutatua ukosefu wa ajira, kupunguza mzigo serikalini na kuongeza mapato kwa taifa.

Njia hii Ni kupitia utoaji wa mafunzo mbali mbali kulingana na hitaji la mtu kupitia vyuo vya VETA baada ya mafunzo wahitimu wapewe mitaji (hata kwa njia ya mikopo) wanaingia kwenye uzalishaji, ila siyo kumwambia mtu aliyesomea utabibu akajiajiri hiyo inakuwa ngumu zaidi.

Namna ya utoaji mafunzo nnavyoshauri iwe;
1. Wanafunzi wote wanaomaliza darasa la saba na wasiweze kuendelea na masomo ya kidato Cha kwanza, wote waende katika vyuo vya VETA wakajifunze ujuzi mbalimbali kulingana na vipaji na uwezo wa Kila mmoja. Katika kundi la watu huwezi kukuta wote wanaweza kusoma na kufaulu mitihani tu, Kuna wengine kusoma na kufaulu masomo ya kuandika hawawezi Ila kwenye masomo ya ujuzi na vitendo Ni wazuri zaidi ya wanaojua kufaulu kwa kuandika. Mafunzo hayo yafanyike kwa mwaka mmoja na yasiwe ya gharama yoyote(serikali igharamie mafunzo hayo) ili mwitikio uwe mkubwa, gharama za matumizi binafsi mwanafunzi mwenyewe atagharamia. Baada ya kumaliza mafunzo hayo wale watakaoendelea na vyuo mbalimbali wanaenda, Wale ambao hawatoendelea na vyuo, wanatengeneza vikundi kulingana na fani zao, wanapatiwa mikopo ya mitaji na serikali, wanaanza kuzalisha. Hapo serikali itakuwa imepunguza asilimia kubwa ya vijana ambao wangeingia Mitaani bila uwezo wa kupata ajira yoyote, kwa sababu mtu aliyemaliza kidato Cha nne na akafeli hana nafasi ya kugombania ajira sehemu yoyote. Pia kupitia uzalishaji wa vikundi hivo watapata mapato na kupunguza mzigo wa utegemezi.

2. Kundi la pili Ni vijana wanaomaliza kidato Cha nne wasipate nafasi ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano, moja kwa moja wanajiunga na kufanya masomo ya ujuzi kwa mwaka Mmoja, kama itakavokuwa kwa darasa la saba, serikali itahusika kugharamia masomo na upatikanaji wa mitaji wamalizapo mafunzo.

3. Kundi la tatu ni vijana wanaomaliza kidato cha sita badala ya kwenda kukiunga na jeshi la kujenga taifa na kuendelea na vyuo vikuu kwa watakaofaulu, wote wanaenda kujiunga na vyuo vya VETA kwa mwaka mmoja pia, katika fani mbali mbalimbali, hii itawapatia msingi mzuri hata Kama watakapokuwa vyuoni kuwa na uwezo wa kujitengenezea kipato baadala ya kuwa tegemezi kwa serikali na wazazi pindi wakiwa chuoni. Hata baada ya kumaliza vyuo namba kidogo Sana ya vijana watakuwa na nia ya kuajiriwa Ila wengi watakuwa na uwezo wa kuingia Mitaani na kupambana na maisha kwa kujiajiri maana wanaujuzi wa kutosha. Kw Sasa vijana wengi wanaomaliza vyuo vikuu Ila hajui hata aanzie wapi bila ajira, mm nikiwa mmoja wapo baada ya kuhitimu katika chuo kikuu muhimbili sikuwa hata na ABC ya kupambana na maisha tofauti na kutafuta ajira katika fani niliyosomea.

Maana mpaka namaliza chuo nlikuwa Sina ujuziwala uzoefu wowote na maisha ya kujiajiri na Ni kipi nitafanya katika kujiajiri huko, siyo Mimi pekeangu Ila vijana wengi Sana nlikuwa napokea malalamiko, maana kila mmoja alikuwa mgeni mtaani, kwa kuwa maisha yote tulikuwa tunapambana kuqeza kufaulu masomo ya darasani na siyo kuwaza maisha baada ya masomo hayo.

4. Kwa wale ambao hawatofanikiwa kuendelea na masomo ya vyuo vikuu nao pia wanatengeneza vikundi kulingana na fani zao watapewa mikopo ya mitaji na serikali na wataingia kuzalisha. Hivo maisha yatakuwa nafuu maana serikali itapunguza mzigo wa vijana wasiona ajira pia itapata mapato na watu watakuwa na maisha mazuri.

Hitimisho;

Kwa njia hii wimbi la vijana wasio na ajira na wasio na uwezo wa kujiajiri utapungua kwa kiasi kikubwa sana. Pia pato la mtu mmoja mmoja litakua na kupunguza hali ya umasikini katika nchi yetu.

Kuhusu kuwa na vyuo vya VETA vya kutosha, Kama serikali imeweza kupata mikopo na kujenga vyumba vya madarasa kila shule nchini, haiwezi kukosa pesa za kuweza kujenga vyuo hivo.

Hivo natoa rai kwa viongozi wa serikali na wizara husika Kama watapata kusoma ujumbe huu waweze kutafakari na kufanyia kazi. Nchi nyingi zilizofanikiwa ambazo zilipata Uhuru pamoja na sisi, wameweza kwa sababu ya kuwa na namba kubwa ya wazalishaji katika nchi zao. Hivo na sisi tutafanikiwa Kama kila mtu atashiriki katika uzalishaji na tutakuwa tumeitendea haki rasilimali watu tuliyonayo katika nchi yetu.
 

Attachments

  • suluhisho la ukosefu wa ajira Tanzania.docx
    44.6 KB · Views: 5
Back
Top Bottom