Suluhisho la Mgogoro wa Msitu wa Ngezi Zanzibar ni kuonesha ramani ya 1997

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,661
2,000
SULUHISHO LA MGOGORO WA MSITU WA NGEZI NA MASHAMBA YA WANANCHI NI KUONYESHWA RAMANI HALISI YA MSITU ULIOPIMWA NA SERIKALI JUL 1997 NA KUPEWA KIWANJA NO.14 MAKANGALE.

Imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya watendaji wa Serikali kutumia mamlaka yao vibaya kupora haki za wanachi kinyemela kwa kisingizio cha uamuzi wa Serikali.

Jana nilimsikiliza mwakilishi wa Welezo Nd. Hassan Khamis (Mkwezi na Mkulima) akizungumza kwa ukali sana, alipokuwa akichangia hotuba ya bajeti Wizara ya ardhi kuhusu msitu wa hifadhi wa Ngezi kuwa umekatwa viwanja. Ikumbukwe kwamba vita hii ilianzia kwenye mijadala ya redio baadae magazati na sasa Baraza la wawakilishi.

Ni wazi kwamba mwakilishi huyu na wenzake walifatwa na kundi hilo kwa lengo la kuzuwia haki za watu zisipatikane kama walivyo kusudia. Kama kwamba haitoshi wawakilishi hao walipewa vielelezo na watu hao mpaka vya wakati wa mzee Hassan Nassor Moyo alipokuwa waziri wa kilimo vinavyo thibitisha kuwa eneo la Ngezi ni eneo la msitu wa hifadhi

Mnamo mwezi wa July mwaka 1997 wizara ya kilimo iliomba kupimiwa eneo la msitu baada ugomvi na wanachi wenye mashamba yaliyo pakana na msitu upimaji huo ulifanyika na msitu huo ukapewa kiwanja No: 14 Makangale, hilo sio siri linajulikana kila mahala na beacon zake zipo. Sasa huko kwenye mashamba ya watu wamekwenda kufanya nini? Mbona walipo pima mwaka 1997 hawakufika kwenye mashamba ya watu wanakodai kwamba hivi sasa ni eneo lao? Au mzee moyo alikuwa waziri mwaka 1998?

Ukweli ni kwamba Baada ya kiongozi mmoja (jina kapuni) kuteuliwa akapewa nafasi ya misitu wizara ya kilimo, baada ya kuona mashamba ya wananchi yaliyopo karibu kilomita moja na beacon za msitu halisi uliopimwa na Serikali, alivutiwa na mashamba hayo kwa matamanio ya nafsi yake, na akafanya dhulma ya kutaka kuyaingiza mashamba hayo katika msitu wa hifadhi kinyume na sheria. Aliamua kujitengenezea ramani mpya ya msitu ambayo ndio aliyo wakabidhi wawakilishi kwa lengo la kupotosha umma. Lakini pamoja na kutengeneza ramani hiyo bado mipaka halisi ya msitu huo inaonekana. Nimeweka ramani aliyo jitengenezea lakini pamoja nahayo alishindwa kuondosha mpaka baina ya msitu na mashamba ya wananchi, picha halisi inajieleza.

Hii inaonyesha wazi kwamba ukweli anaujuwa ila analo alilolikusudia kwa wananchi hao lakini ukweli hausemi. Tunaiomba Serikali itende haki kwa hili.

Tunataka wizara ya kilimo ieleze walipimiwa na nani kwenye yale mashamba ya watu baada ya ule upimaji halali ulio fanyika July 1997? Pia waeleze wameyapatapataje mashamba hayo? Jee! wamelipa fidia kwa wananchi hao? Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 toleo la mwaka 1995 kifungu 17/C imeweka wazi kuhusiana na sheria za uchukuwaji wa mali ya mtu. Kifungu 17 Hakuna mali ya mtu yeyote itakayo chukuliwa kwa nguvu na hakuna maslahi au haki yoyote inayo tokana na mali hiyo iliyo chukuliwa kwa nguvu isipokuwa pale ambapo masharti yafuatayo yametimizwa. Miongono mwa Masharti hayo ni kifungu 17/C Sheria imewekwa kuhusiana na umilikaji au uchukuaji huo kwa kutoa fidia inayo lingana. Jee! Wizara ya kilimo ilikamilisha taratibu hizo au imepora tu? Naomba kuwasilisha by Ally Rashid.

Chanzo: Mzalendo
 

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
6,689
2,000
Nimeuelewa sana uchambuzi wako mkuu,popote ulipo agiza soda nitalipa.Safi sana
 

Chapa Nalo Jr

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
7,116
2,000
Kibaraza chenyewe kina mafi siem watupu wala hakinogi hata kujua yaliyoongelewa. Yaani hata wakiamua kuuza ZNZ leo hii wala wananchi hawatajua
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom