Suluhisho la matatizo ya ndoa/mahusiano...... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Suluhisho la matatizo ya ndoa/mahusiano......

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by sakapal, Oct 8, 2012.

 1. sakapal

  sakapal JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,824
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Habari zenu wana MMU, jana nimelala usingizi wa mang'amung'amu baada ya kusimuliwa mkasa mmoja wa kwenye ndoa na kuniacha na maswali meengi bila majibu. Mkasa wenyewe uko hivi:-
  dada yangu (mtoto wa baba mkubwa) alinialika jana na watoto kulikuwa na hafla fupi tuu, kutokana na majukumu ya hapa na pale nilifika jioni na watoto. Baada ya kusabahiana maongezi yalianza na ndo hapo akaanza kunieleza yanayomsibu yeye na mumewe. (wana watoto 2, mmoja wa kike mwingine wa kiume). Baada ya ndoa yao walifanikiwa kimaisha na kutoka kwenye hali ya chini hadi maisha ya kifahari, baada ya yote haya mumewe akaanza vizaa zaa vya kusoma CPA, CPA ndo ikawa CPAAAA lol haina katikati ya wiki wala week end. Mume akiondoka asubuhi kwenda kazini kurudi saa tano usiku kila siku, haya jumamosi na jumapili nayo akitoka saa mbili asubuhi hurudi saa tano usiku. Na akirudi hamna kupeana mchezo mume anasema amechoka. Siku za week end atajaribu kujishikashika atapiga kimoja na akimaliza hapo kachoka. Hii hali ilikuwa inamkera sana dada yangu na akilalamika na kuongea nae mumewe wala hamjali na anamuona hana jipya.
  Sasa dada yangu jana alikuwa mechukia na akaniambia mdogo wangu nakwambia hili ila nimeshaamua narudia vidum vyangu na amemwambia live mume wake kuwa asimtafute wala asimfatilie na yeye anaenda kutafuta wake huko nje wa kumridhisha kiunyumba. Jana hiyohiyo mume wake aliniambia kiutaniutani '' shemeji naomba usiondoke leo endelea kuwepo angalau naiona tabasamu ya mke wangu, yaani ukiondoka tuu hali itarudi ileile, dada yako kaninunia na hali ni mbaya''. Nilicheka tuu sikumjibu kitu na muda ulifika nikaondoka kwani nami ninamji wangu.
  Ndoa yao imefika pagumu watoto bado wadogo mkubwa anamiaka 5 na mdogo 2 ilhali dada yangu amesema nimechoka mdogo wangu, kuliko niletewe ukimwi ndani bora na mimi niende nikautafute huko nje nikiupata nijue nami nilitoka. Daah! hapo nilichoka kabisa na akathubutu kusema najuta kuolewa na mume wa jinsi yake ambaye tulianzia from scratch, bora ningeolewa na mtu ambaye wa mjini alishashika hela na amezizoea kuliko hivi nilivoolewa na mtu ambaye hakuwa na hela hivi sasa kazipata basi anajiona dunia yote yake. Mume hatulii nyumbani hii CPA nimeshaichoka.

  Baada ya maelezo hayo nilijiuliza:-
  Hela imelaaniwana wanaozishika wanapata laana hiyo?
  Hivi suluhisho la ndoa ni nini?
  Lini matatizo ya ndoa yataisha?
  Matatizo ya ndoa yanasababishwa na nini?
  Je ni mapepo ndo yanavamia ndoa na kuzivuruga hasa mafanikio yanapokuja?
  Je ili ndoa isiwe na matatizo haya bora kubaki na hali ya chini kiuchumi?
  Je wanandoa wasitafute hela na kuinuka kiuchumi ili wasiwe na matatizo?
  Je mafanikio na maendeleo kwenye ndoa yanaleta matatizo kwenye ndoa?
  Naomba mchango wenu wa mawazo wana MMU woote ili niweze kumsihi dada yangu anusuru ndoa yake.
  NB: hii habari ni ya kweli naomba mawazo yako tafadhali.
   
 2. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  my unmarried, uneducated, poor man's response in blue
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Pesa hutumika kuuweka hadharani 'upu.mbavu' wa mtu au kuihubiri 'hekima' yake.

  Pesa ni kifaa tu kama kalamu, sitaki kuamini kama kalamu aghali inabadili maarifa yako kichwani.
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Ha ha ha ha, una mambo siku hizi

   
 5. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  jamani ndio ukweli huo. nasumbuka na gf, elimu yangu ni ku-type document kazini na bado nataabika kuweka petroli kwenye ka-corolla kangu. yaani we.. acha tuu ngoja nioe. sina pesa so ndoa yangu itakuwa na amani na raha tupu bila mapepo lol
   
 6. sakapal

  sakapal JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,824
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  asante kwa mchango wako ntauchambua na kuuwakilisha, lol.
   
 7. sakapal

  sakapal JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,824
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  unachosema ni kweli Kongosho, mtu akiwa na pesa sijui zinakuwa zinamuwasha miguuni, yaani hawezi kukaa mahali pamoja, na anaweza kufanya chochote bila kuwa na woga wala kujali, daah! ukichanganya na pombe ndo balaa
   
 8. kbm

  kbm JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 4,963
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mpe pole. Lakini hujatueleza kinagaubaga kuhusu wanandoa wako na CPA yao, yawezekana kati yao kuna mmoja ameshindwa kutimiza wajibu wake kama mwanandoa na kumfanya mwenzake apoteze mwelekeo na kukosa hamu kwa mwenzie, hii mara nyingi inatokea, nani hatari sana katika familia mambo haya yakianza kujitokeza. Jana jumapili kuna mjadala ulikuwa unaendelea hapa JF kuhusu mahusiano (jinsi ya kumteka mwenzio kimapenzi) Topic ilivyoanza kawaida lakini mbele ya safari watu wengi tulifaidika namichango ya wadau. Kuna dada Grace & Madame inaoneka ni wanaJF waliobobea ktk maswala ya mahusiano ukiwasiliana nao waweza saidia (BIG UP! Grace & Madame) ingawaje kunabaadhi yetu wanaJF tulianza kuharibu hari ya hewa kwa kuweka picha za utupu, lakini ili kuwa topic nzuri kwa wanandoa.
   
 9. sakapal

  sakapal JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,824
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  heheheheeeee, sio formula Blaine, sinadata kamili ila wengi kama sio wote walionza from scratch kwenye ndoa walipofanikiwa mambo yaliharibika, hakukuwa na ndoa tena bali maudhi na karaha tuu...........
   
 10. sakapal

  sakapal JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,824
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  pole zako ntazifikisha kwa dada, kweli inawezekana kuna mmoja wao aidha dada yangu au mume wake ameshindwa kutimiza wajibu wake wa ndoa, sina uhakika nani alianza kuharibu na aliyeanza alianza kwa sababu zipi, nitaufatilia huop mjadala uliosema, thanx kbm
   
 11. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  mh!pesa !pesa pesa
  pesa zinavunja mapenzi ,pesa zinajenga mapenzi
  pesa zinaleta furaha pesa zinaleta maumivu
  pesa zinaleta mambo kibao! sakapal naweza kuimagine viatu vya dada yako!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. sakapal

  sakapal JF-Expert Member

  #12
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,824
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  yaani anauchungu na maumivu na ameshaikatia tamaa ndoa yake.
   
 13. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  ngoja nifanye kazi moja hivi halafu nakuja kama nusu saa hivi,tujaribu kuweka mambo sawa!manake mi huwa naumia sana ndoa kitu ndoa kinapofika hatua hii!naumia sana kwa kweli!
   
 14. d

  destiny1 JF-Expert Member

  #14
  Oct 8, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 250
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sijaona tatizo lolote kubwa la kutisha hapo, ni tatizo la kawaida sana kuchokana sometimes, mwambie mwanadada asithubutu vidumu ni sumu, wanawake hatuwezi hayo mambo atalowea huko maana wanawake tumeumbwa kupenda na sio kutimiza haja za mwili tu, aongeze manjonjo, akunjue sura mumewe kashasema anaogopa hiyo sura yake aliyoikunja jamani. Atabasamu, asamehe, amwambie mume wake I love you so much darling kwa maneno na matendo, aone miujiza ikitendeka ndani ya ndoa yake.
   
 15. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #15
  Oct 8, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  how is this related to my post?? sikusema chochote kuhusu vidumu au tamaa za kiwili wala sikumshauri afanye hivyo
   
 16. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #16
  Oct 8, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  usikatae wanaume na pesa wachana nao kabisa wakifanikiwa aiseee hutawaona kabisa nakwambia ikiisha atarudi kama digidigi jmosi nimekutana na rafiki yangu akawa ananieleza the same thing wanaume na pesa ni hatari sana nakiri hili
   
 17. Fyong'oxi

  Fyong'oxi JF-Expert Member

  #17
  Oct 8, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  HAPO FURAHA HAIWEZI KUWA NA AFYA, STORI KAMA HIZI ZITAOGOPESHA VIJANA KUOA/LEWA! au ndio changamoto ?
   
 18. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #18
  Oct 8, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  walaaahiiiiiiiiiiiiii nimekosa cha kusema
   
 19. d

  destiny1 JF-Expert Member

  #19
  Oct 8, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 250
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  oppps! sorry oooh, I meant kumquote mleta mada, haraka haraka unajua tena naogopa kukutwa na bosi :eyebrows:
   
 20. piper

  piper JF-Expert Member

  #20
  Oct 8, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ama kweli ndoa ndoano
   
Loading...