Suluhisho la Machinga sio kufukuzwa, mji ubomolewe

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
14,840
31,583
Hello JF,
Suala la Machinga kufanya biashara mjini Kariakoo na sehemu nyinginezo limekua ni tatizo la miaka nenda rudi bila ufumbuzi wowote, imekua kero kwa wapita njia na wafanya biashara wengine,,,,,,,

Binafsi sidhani kama kuwafukuza waende sehemu nyingine ni suluhisho, wataenda kwa muda baada ya muda mfupi wanarudi tena,lazima tupate ufumbuzi wa hili tatizo litokomee for good,

In a way nawaelewa haileti maana kupelekwa sehemu ambazo ni ngumu kufanya biashara,,,,

Machinga wasifukuzwe bali napendekeza waachwe kufanya biashara hapo hapo mjini. Kwa vile Kariakoo ni ndogo kuwa accommodate both Machinga na wafanya biashara wengine, na since wote wana struggle for a space, THEN space itafutwe kwa kwenda juu. Namaanisha mji ubomolewe zijengwe ghorofa za biashara, na hii itatoa nafasi kwa wote. Chini/ underground,ama nyuma , juu,hizi ghorofa ziwe ndio sehemu maalumu ya hawa Machinga kufanya biashara zao, Nafasi kwa wote kufanya biashara,, hata nchi nyingine sio kwamba hakuna wafanya biashara ndogo ndogo ni wanatengewa sehemu zao hapo hapo mjini kwenye kitovu cha biashara,

Kufumua mji might seem costly at first lakini mimi ndio naona ndio suluhisho la kudumu,,,

Mnasemaje?

Becky
 
Tubomoe mji kisa machinga???? Duh. Hapa lazima unaposema tubomoe mji useme pia utawajengea sehemu gani na itabidi kujiuliza he wakakubali kukaa hapo.

Machinga ni tatizo kwa kila awamu since mzee Mwinyi alipofungua milango ya uchumi kuagiza bidhaa nje ya nchi. Machinga haagizi bidhaa nje labda ukijua machinga tunayemtarget ni yupi au machinga ni nani ndio unaweza kujua tatizo lipo wapi.

Machinga halisi ni yule aliyekuwa anachukua bidhaa kwa tajiri especially wahindi na kuuza kwa bei ndogo mitaani anazurura sababu halipi Kodi na mwenye mzigo anamchaji pesa ndogo akijua machinga atauza bila TRA kujua thamani halisi ya mzigo ulioingia kwenye godown na mzigo uliouzwa.

Machinga anauza kwa bei ya kunegotiate anaanza bei ya juu kabisa na anaweza kuuza hata bei ya chini kabisa sababu hana operation costs kubwa kama mwenye duka na kumbuka yeye hana mtaji mkubwa, mtaji alionao ni bidhaa alizonazo mkononi.

Kwa mfano, Machinga walijengewa pale machinga complex jiulize ilitokea nini? Tatizo sio kuwajengea Ila ukikaa bar au ukiwa kwenye foleni wao wanakusaidia wanakuletea bidhaa hapo ulipo na kwa bei nafuu wakati mwingine, au pia wanakupunguzia adha ya kwenda Kariakoo au kwingine kununua let's say just kofia au sandals, so haihitaji kwenda machinga complex na hii ndio ikawaumiza wale ambao waliamua kwenda machinga complex wakajikuta pale hawauzi kitu wakarudi mtaani na hakuna machinga anakubali kurudi pale.

Labda tutafute eneo liwe gulio Yani labda kama mnada fulani kila siku kadhaa kunakuwa na nyama, michezo nk kama Dodoma au kibaha walivyofanya although bado haitaondoa hawa street vendors wa kila siku ambao TRA wanatakiwa kuwakamata sababu hawalipi Kodi.

Dawa ni TRA kukamata kila anayeuza mkononi utaona kama watakuwepo sababu pesa nyingi sana inapotelea hapo.

Lakini, kumbuka napo tutakuwa na tatizo jipya la kukosa kazi. So ishu sio kuvunja mji tuandae mazingira mazuri tu mengine Ila hao watu ni ngumu kuwamaliza kwa nchi zetu hizi. Utavunja mji bila sababu.

Kimsingi machinga ni mtaji wa wanasiasa, just soma philosophy ya Plato kuhusu social classes utaelewa, we jitahidi kupambana kutoka kwenye class ya MEN OF ALL BASES METAL 😃😃😃 because the universe is a gang world my brother, there's no place for the innocent.
 
Sio kimya bado sijakuelewa, wamachinga hawataki kukodi fremu wanataka kuwa mbele ya maduka ya watu sasa ukisema ujenge kwenda juu usitegemee kama kuna chinga ataenda juu
Hapana mkuu nguvu Machinga wanaweka bidhaa zao mbele ya maduka ya watu sababu eneo liko strategic kibiashara, mbona hawapangi bidhaa zao huku kwingine kwenye maduka ya watu njoo Kisukulu huku hamna anayepanga bidhaa zake nje ya duka la mtu? Wanapanga kariakoo na huko posta?? eneo kwa kuwa liko strategic lazima tutafute mbinu ya ku utilise hio limited space hapo mjini. Binafsi kwa kuwa sehemu iko kibiashara Machinga wakiwa na uhakika wa kuuza bidhaa zao hawatajali wamewekwa ghorofa ya ngapi...
 
Hapana mkuu nguvu Machinga wanaweka bidhaa zao mbele ya maduka ya watu sababu eneo liko strategic kibiashara, mbona hawapangi bidhaa zao huku kwingine kwenye maduka ya watu njoo Kisukulu huku hamna anayepanga bidhaa zake nje ya duka la mtu? Wanapanga kariakoo na huko posta?? eneo kwa kuwa liko strategic lazima tutafute mbinu ya ku utilise hio limited space hapo mjini. Binafsi kwa kuwa sehemu iko kibiashara Machinga wakiwa na uhakika wa kuuza bidhaa zao hawatajali wamewekwa ghorofa ya ngapi,,,,binafsi nina uhakika sababu sehemu ni ya kibiashara, kila mtu ana uwezo wa kuuza then Machinga wakikatiwa sehemu hapo hapo watatii agizo la kukaa kwenye sehemu maalumu walizotengewa
Una wazo zuri Ila jiulize je does it work? Tuna machinga complex, kuna soko la magomeni usalama nenda soko jipya kisutu kaulize halafu uje uandike Tena please.
 
Sio kimya bado sijakuelewa, wamachinga hawataki kukodi fremu wanataka kuwa mbele ya maduka ya watu sasa ukisema ujenge kwenda juu usitegemee kama kuna chinga ataenda juu
Hawa machinga tunaowaongelea Leo ni walewale waliojengewa soko kubwa kama machinga complex na kisutu plus mengine makubwa hata Temeke limejengwa sasa sijui watu hawaoni tatizo sio jengo tatizo ni their way of doing business wao hawana huo mtaji wa kukodi eneo.

Angalia wale waliojaa kariakoo wanaouza bidhaa kwenye njia za wapita kwa miguu unakuta ni mtu ana mafungu kumi ya nyanya, vitunguu na bamia kadhaa mtaji hamalizi 20,000 analaza gunia chini kazi uendelee, hao wanawaumiza wale walioko kule shimoni ambako zamani ilikuwa ukitaka nyanya, mbogamboga lazima uende kule na wanalipa ushuru mkubwa kule.

Hii inawaumiza walioko chini kule na wanalazimika kutafuta watu wa kuwauzia ili nao wapate japo ushuru. This is crazy, hatuwezi kuwa na system ya biashara ya holela namna hii, tunaua macro business kwa kupromote micro business ambazo hazipo kwenye system rasmi ya kodi, no wonder serikali inaishia kuweka tozo za simu maana hawataki kukubali kwamba Kodi kubwa inapotea kwa machinga.

Actually wanaopiga kelele ni hao ambao hawalipi Kodi wanauza bidhaa na kujipatia kipato bila kulipa Kodi ya bidhaa wanazouza, hii ni kosa hata kisheria ni mfumo wa tax evasion which is punishable by law.

Kama mtu anataka kufanya biashara nadhani tukubali kwamba biashara sio lelemama kwamba unafanya kiholela tu wakati kuna gharama za kusafiaha mji, gharama za ujenzi wa miundombinu ambayo wao wameikuta na wanataka kuitumia ingali haikujengwa kwa ajili ya kuaccomodate hizo biashara zao.

Hata tukiwaruhusu kuna masuala ya kiusalama kama Moto, ajali nk pia masuala ya kiafya unakuta huduma kama vyoo hakuna hayo maeneo, mama ntilie wanauza chakula sababu ya wale wanaofanya biashara hizo lakini kiafya ni sahihi?

Hebu tujiulize mbona wenye malori wanaambiwa hakina kupaki lorry kiholela otherwise inapigwa fine na hawabishi inabidi kila tajiri anunue yard ya kupaki lorry zake.

Lazima tufike wakati tuondokane na fikra za zamani, ni ngumu sana kukubali Ila with time wataondoka na itazoeleka tu.
 
Una wazo zuri Ila jiulize je does it work? Tuna machinga complex, kuna soko la magomeni usalama nenda soko jipya kisutu kaulize halafu uje uandike Tena please.
Nikaulize nini?? Ukishabomoa mji na kutenga eneo lao hapo hapo mjini unaintroduce fee ya kutumia hio sehemu ya kufanya biashara, japokua eneo litakua dogo fee yake inatakiwa kuwa kubwa sababu ni mjini. Hii itawatawanya, kwa wasiomudu kuuza mjini watatafuta maeneo mengine,ofcourse this won't work if maeneo mengine muundo mbinu yao haitatengenezwa. So pote panapoonekana Machinga wanasumbua sana ni kuwawekea sehemu hapo hapo ya kuuza kwa kuwajengea strategically hio limited space.

Mwisho ningependa pia kuwe na visheria vidogo vidogo vya kuwazuia wafanyabiashara kufanya biashara kiholela,,,
 
In fact unakubaliana nami kwamba haitakuwa feasible kubomoa na kujenga maeneo ya biashara ya machinga since wewe mwenyewe unasuggest iwepo ushuru mkubwa ambapo tayari machinga hataweza so tunarudi kulekule kwamba ni tatizo.

Kuhusu sheria ndogondogo zipo zinatungwa na Halmashauri za miji na ni kali ndio maana unaona kina Mahakama ya Jiji ambayo kazi yake ni kuenforce hizo kanuni. Ndio maana askari wa jiji wakiwakamata huwa wanawapeleka kwenye hiyo Mahakama na adhabu mara nyingi ni fine, hata kutupa takataka unapelekwa hapo.
 
Kiukweli hata tukibomoa wakapangwa wachache bado watakuwepo watakaouza nje ya maeneo hayo tu. Ukitaka kudeal na sheria inayolenga kuondoa tatizo dawa ni kuweka katazo moja kwa moja hakuna kufanya biashara maeneo hayo ukikutwa ni mahakamani period.
 
In fact unakubaliana nami kwamba haitakuwa feasible kubomoa na kujenga maeneo ya biashara ya machinga since wewe mwenyewe unasuggest iwepo ushuru mkubwa ambapo tayari machinga hataweza so tunarudi kulekule kwamba ni tatizo.

Kuhusu sheria ndogondogo zipo zinatungwa na Halmashauri za miji na ni kali ndio maana unaona kina Mahakama ya Jiji ambayo kazi yake ni kuenforce hizo kanuni. Ndio maana askari wa jiji wakiwakamata huwa wanawapeleka kwenye hiyo Mahakama na adhabu mara nyingi ni fine, hata kutupa takataka unapelekwa hapo.
Mkuu vitu vitatu, bomoa mji, Tenga sehemu zao,weka fees,this will only work kama kubomoa kunaendana na ku develop sehemu nyingine zinazoonekana kuwa centres za biashara.

High fees nilikua namaanisha Mmachinga anayeuza Kariakoo asiwe sawa na wa Buguruni, sijasema walipe high fees mpaka washindwe kumudu. Ofcourse, Mmachinga fees zao hazitakuwa sawa na wafanyabiasha wa kawaida
 
Mkuu maghorofa kwa saikolojia ya machinga hayalipi na hayafai.

Ukiwa ghorofani hauna uwezo wa kukimbia kimbia kushawishi ama kutapeli mteja.

Unakuwa kama mwanamke wa kiswahili, kuolewa hadi atafutwe na aanze kutongozwa yeye, haruhusiwi kupenda ama kutamani mwanaume kwa hisia zake (kuusemea moyo), ataitwa kicheche.
 
Wamachinga wamemaliza barabara zote za waenda kwa miguu, kuanzia mataa ya uhuru hadi karume upande wa TBL raia wanatumia barabara moja na magari, eneo la watembea kwa miguu lote limejaa vibanda hadi fensi ya tbl haionekani na mamlaka zipo wala hazijali
 
Hapana mkuu nguvu Machinga wanaweka bidhaa zao mbele ya maduka ya watu sababu eneo liko strategic kibiashara, mbona hawapangi bidhaa zao huku kwingine kwenye maduka ya watu njoo Kisukulu huku hamna anayepanga bidhaa zake nje ya duka la mtu? Wanapanga kariakoo na huko posta?? eneo kwa kuwa liko strategic lazima tutafute mbinu ya ku utilise hio limited space hapo mjini. Binafsi kwa kuwa sehemu iko kibiashara Machinga wakiwa na uhakika wa kuuza bidhaa zao hawatajali wamewekwa ghorofa ya ngapi...
Una uhakika mkuu? Machinga umuweke ghorofani kweli? Labda hujaelewa mentality za wafanyabiashara wadogo na wachuuzi, lakini pia mentality za wanunuzi wa kitanzania.

Kwangu hapa ndio mzizi wa tatizo ulipo, purchasing power ya mtanzania ndio inamuweka machinga alipo, kama mtanzania angekuwa na uwezo wa kununua bidhaa kwa kupanga(shopping), kama mtanzania angekuwa na mfuko uliojaa hivyo kuwa na uwezo wa kwenda kufanya manunuzi ya wiki, usingeona kushamiri kwa wachuuzi. Kwangu tatizo lipo hapo.

Ila machinga hatokaa ghorofani, that's for sure, machinga hatokaa mbali na njia za watu, machinga anataka kukaa wanapopita watu, coz sisi tunanunua bila hata kupanga, anajua 2k-5k atazipata kirahisi.

Shida ya mtanzania, anatoka asubuhi na 10k-20k, hana wazo la kununua shati la mtumba, anakuja machinga na shati kali za 5k, akiiona tu ile shati, "oya njoo tuone", mwisho wa siku ananunua hata bila kupanga, hakuwa na mpango huo...ndio maana machinga hawataisha.

Tutafute suluhu, Ila kumuweka machinga mbali na watu hujatatua tatizo bado.
 
Hello JF,
Suala la Machinga kufanya biashara mjini Kariakoo na sehemu nyinginezo limekua ni tatizo la miaka nenda rudi bila ufumbuzi wowote, imekua kero kwa wapita njia na wafanya biashara wengine,,,,,,,

Binafsi sidhani kama kuwafukuza waende sehemu nyingine ni suluhisho, wataenda kwa muda baada ya muda mfupi wanarudi tena,lazima tupate ufumbuzi wa hili tatizo litokomee for good,

In a way nawaelewa haileti maana kupelekwa sehemu ambazo ni ngumu kufanya biashara,,,,

Machinga wasifukuzwe bali napendekeza waachwe kufanya biashara hapo hapo mjini. Kwa vile Kariakoo ni ndogo kuwa accommodate both Machinga na wafanya biashara wengine, na since wote wana struggle for a space, THEN space itafutwe kwa kwenda juu. Namaanisha mji ubomolewe zijengwe ghorofa za biashara, na hii itatoa nafasi kwa wote. Chini/ underground,ama nyuma , juu,hizi ghorofa ziwe ndio sehemu maalumu ya hawa Machinga kufanya biashara zao, Nafasi kwa wote kufanya biashara,, hata nchi nyingine sio kwamba hakuna wafanya biashara ndogo ndogo ni wanatengewa sehemu zao hapo hapo mjini kwenye kitovu cha biashara,

Kufumua mji might seem costly at first lakini mimi ndio naona ndio suluhisho la kudumu,,,

Mnasemaje?

Becky
Yani watu wavunjiwe nyumba zao kwa sababu ya machinga? Ukumbuke machinga yupo barabarani kama eneo rahisi la kuwapata wateja hasa wapita njia. Sasa machinga awe floor ya 8 nani atamfata huko juu ikiwa
 
yaani ujenge magorofa kisa machinga? Muuza pafyumu kwa meza apange gorofani? muuza chupi nae akae gorofani juu? Gharama za ujenzi nani anagaramia kama ni serikali hiyo hela itarudije? Hao machinga wanataka weweke meza zao sehemu ya wazi na vibanda vyao na wala sio flem hizo unazo sema wewe!

Kwani si mfano ni hapo Karume serikali ilikula hasara kwa kujenga soko la Machinga complex na machinga kwa lengo la wamachinga wote kwamba watoke maeneo ya chini au wazi na kupewa vizimba juu gorofani huku wakichangia hela kidogo, nani alienda kule sasa? wote walihama na kuendelea kuuza chini tu jumba likaheuka ghofu mpaka leo vijana wanavutia bange tu pale.

Hawa wafukuzwe kwa haraka mno hata hivyo tulichelewa mno kuwaondoa hawa wameharibu mji anzeni na machinga halafu wafate boda boda nao wapangiwe maeneo ya kuweka vituo vyao sio kila sehemu ni vituo nao ni kero nyingine inayokuja kwa kasi mno.
 
Mji kubomolewa hapo tunazungumzia uwepo wa bajeti tena, kwa hii bajeti yetu inayomtegemea mzungu ili miradi itekelezeke naona bora tutulie tu tupambane na hali yetu.

Machinga vyema waondoke mjini, wanende nje ya miji, wahitaji wa bidhaa wakijua wanapopatikana watawafuata, hili sio suala la kusema wakiondolewa mjini hawatapata wateja, provided wao kodi hawalipi basi na bidhaa zao zitakuwa bei rahisi, naamini watafuatwa popote watakapokwenda.
 
Back
Top Bottom