Suluhisho la Kudumu la Muungano Bora wa Tanganyika na Zanzibar Hili Hapa

1. Watu wa Tanganyika wenye makazi ya kudumu Zanzibar na Wazanzibar wenye makazi ya kudumu Tanganyika, wapewe uhiari, haki na uraia wa kuendelea kuishi Zanzibar au Tanganyika mtawalia.

2. Endapo Tanganyika na Zanzibar zitaendelea kuwa na uraia wa nchi moja, basi nchi hizi mbili ziwe na makubaliano maalum ya uraia maalum wa nchi mbili (Duo Exclusive Treaty on Special Dual Citizenship) kwa Watanganyika na Wazanzibar ambao watahiari kuwa na uraia wa nchi mbili baina ya Tanganyika na Zanzibar pekee.

3. Tanganyika na Zanzibar ziwe madola huru kama ilivyokuwa kabla ya muungano na zijiunge katika jumuiya au taasisi mbalimbali za kikanda au kimataifa ikiwa pamoja na Umoja wa Mataifa (UN), FIFA, nk.

4. Pasiwepo viza ya kusafiria kati ya Tanganyika na Zanzibar isipokuwa vitambulisho vya uraia au hati za kusafiria (passports) zitumike kumtambua Mtanganyika au Mzanzibar.

5. Iundwe Tume ya Mahusiano na Ujirani Mwema baina ya Tanganyika na Zanzibar (Commission for Relations and Good Neighbourhood). Tume hii pamoja na mambo yatakayojitokeza, ifanye yafuatayo:

(a) Kuweka utaratibu wa kuimarisha uhusiano na ulinzi wa pamoja wa Majeshi ya Ulinzi ya Watu wa Zanzibar (Zanzibar People’s Defence Forces - ZPDF) na Majeshi ya Ulinzi ya Watu wa Tanganyika (Tanganyika People’s Defence Forces -TPDF). Wanajeshi wa Tanganyika na Zanzibar wataendelea kutumika kwa pamoja kulinda watu na mipaka ya Tanganyika na Zanzibar.

(b) Kugawanya madeni ya nje kulingana na uwiano halisi wa jinsi yalivyotumika kusaidia nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar.

(c) Kuratibu balozi za nje ili ziendelee kutumiwa pamoja kiofisi (shared consulates) kwa Tanganyika na Zanzibar hadi wakati ambapo uwezo wa kila nchi utaruhusu kuwa na ubalozi wake.

(d) Kuratibu fedha na/au sarafu za aina moja ili ziendelee kutumika kihalali kati ya Tanganyika na Zanzibar ili kudumisha uhusiano na utambulisho wa kihistoria.

Hitimisho

Nikiwa mwanafunzi wa Mwalimu Nyerere nihitimishe kwa kusema alichokataza ni kufukuzana baina ya Watanganyika na Wazanzibar. Akaita dhambi kubwa sawa na kula nyama ya mtu. Hakukataza maelewano na makubaliano ya amani. Na sitegemei watu wanaokubaliana kwa amani watapigana. Wala si sahihi kulinganisha hilo na Sudan ambao walipigana miongo kadhaa wagawane nchi.

Wakati vita vya Uganda na Tanzania vikielekea ukingoni kabisa Mwalimu Nyerere alilaumiwa kuwa anataka kuimeza Uganda, wengine wakadiriki kusema kama alivyoimeza Zanzibar. Yeye alijibu kuwa lililo la msingi ni kudumisha amani na nchi jirani na kuwa na uhusiano mwema - si kuunganisha nchi. Tubakie majirani wema kama ilivyo kwa Zambia, Msumbiji, Rwanda, Kenya na kwingineko. Kuwa na mahusiano mema na jirani ni jambo la msingi na si lazima muunganishe nchi.

Kuna nchi nyingi tunahusiana nazo vizuri sana na kwa ukaribu japo haziko jirani, sembuse Zanzibar na Tanganyika! Undugu ni mahusiano mema si kuunganisha nchi. Na ujirani na udugu wa kihistoria upo kwa nchi zote tunazopakana nazo na si Tanganyika na Zanzibar pekee.

Muungano usilindwe kwa vitisho na kulazimishana, bali kujenga na kuimarisha mahusiano na ushirikiano mwema wa viongozi na wananchi wa hizi nchi mbili.

Kuna faida nyingi za kitaifa na kimataifa kwetu sisi Watanganyika kuwa nchi kamili, na vivyo hivyo kwa Zanzibar. Tusizibiane fursa na kuendelea kukerana au kulalamikiana!
Hakuna haja ya kuzunguka huku na huko. Nchi moja kuwa na serikali mbili au tatu ni urasimu na garama zisizokuwa lazima. NCHI MOJA SERIKALI MOJA. Basi.

Tupige kura ya maoni- waZanzibari na waTanganyika kwa pamoja wanataka muungaano, sawa, tuwe nchi moja yenye serikali moja. Upande mmoja hautaki, au pande zote mbili hazitaki, tuachane na huu muungano ambao mpaka sasa wananchi wa hizi nchi mbili hawajapata nafasi ya kuutolea maoni kwa njia ya kura.

Kufikia hapa tunachojua kwa uhakika ni wanasiasa wachache tuu wa ccm ndio wanautaka muungaano kwa maslahi yao binafsi. na ndio wanaapa kila siku kulinda muungano huu. Waulize faida za muungano huu, kwa ulinganisho wa mathalani, kutokuwepo muungano baina ya Tanganyika na Rwanda auZambis na Malawi kama wanazo.

Sababu zilizo pelekea muungano mwaka 1964 leo hazina mashiko kabisa, hatupaswi kuung'ang'ania. Tunatumia gharama kubwa bila faida yoyote, kama tulivyotumia gharama kubwa kuhamia Dodoma, kwa kufuata sababu za miaka ya 1970, na mawazo ya Nyerere, bila kuzingayia kuwa sasa tuko karne ya 21 yenye maendeleo makubwa ya teknolojia ambapo njia za mawasiliano na usafiri hazitulazimu mji mkuu kuwa katikati. Yale mawazo kwamba ni rahisi adui kupiga Dar es salaam kwa vile ni pembezoni na imepakana na bahari yamepitwa na wakati. Hatuna haja ya kuwa na maadui, na tukiwa nao wanaweza kutupiga hata kutokea bahari ya Atlantic.
 
Wazenji wengi wapewe ajira bara na wabara wengi wapewe ajira Zenji halafu wazaliane mchanganyiko hadi washindwe kubaguana.
Kama tu tunavyoheshimiana uislam na ukristo ,,maana kuna ndoa nyingi tu ambazo zimechanganya dini hizi mbili na uzao mwingi uliotokana na familia za aina hiyo na hivyo kufanikiwa kuondoa ubaguzi.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
nimeipenda hii kwa minajiri labda itatufikisha nipatakapo mimi kuwa na nchi moja na serkali moja. mana hii mipaka ni ya kikolon tu. asili yetu ni wamoja. na sijui kwanini hii serkali moja haipigiwi debe na wachangiaj wengi! tunasahau aina nyingine za muungano nje ya serkali moja ni kwa faida ya wapenda madaraka hasa!
 
Wazo murua kabisa!

Naungana na hoja zako kwa mikono miwili na miguu miwili pia. Hatuwezi kuendelea kujifanya tunatatua kero zisizoisha na kuwatisha wanaozihoji kero hizo.
Hakuna haja ya kuzunguka huku na huko. Nchi moja kuwa na serikali mbili au tatu ni urasimu na garama zisizokuwa lazima. NCHI MOJA SERIKALI MOJA. Basi.

Tupige kura ya maoni- waZanzibari na waTanganyika kwa pamoja wanataka muungaano, sawa, tuwe nchi moja yenye serikali moja. Upande mmoja hautaki, au pande zote mbili hazitaki, tuachane na huu muungano ambao mpaka sasa wananchi wa hizi nchi mbili hawajapata nafasi ya kuutolea maoni kwa njia ya kura.

Kufikia hapa tunachojua kwa uhakika ni wanasiasa wachache tuu wa ccm ndio wanautaka muungaano kwa maslahi yao binafsi. na ndio wanaapa kila siku kulinda muungano huu. Waulize faida za muungano huu, kwa ulinganisho wa mathalani, kutokuwepo muungano baina ya Tanganyika na Rwanda auZambis na Malawi kama wanazo.

Sababu zilizo pelekea muungano mwaka 1964 leo hazina mashiko kabisa, hatupaswi kuung'ang'ania. Tunatumia gharama kubwa bila faida yoyote, kama tulivyotumia gharama kubwa kuhamia Dodoma, kwa kufuata sababu za miaka ya 1970, na mawazo ya Nyerere, bila kuzingayia kuwa sasa tuko karne ya 21 yenye maendeleo makubwa ya teknolojia ambapo njia za mawasiliano na usafiri hazitulazimu mji mkuu kuwa katikati. Yale mawazo kwamba ni rahisi adui kupiga Dar es salaam kwa vile ni pembezoni na imepakana na bahari yamepitwa na wakati. Hatuna haja ya kuwa na maadui, na tukiwa nao wanaweza kutupiga hata kutokea bahari ya Atlantic.
 
Niliwahi kupendekeza hilo la serikali moja kama ilivyo sasa kwa Wajerumani. Awali walikuwa na nchi mbili tofauti, Ujerumani Magharibi na Ujerumani Mashariki. 1989 zikaungana na kuwa na Ujerumani moja ya sasa.

Kwetu Wazanzibari walikataa katakata kwa madai kwamba Zanzibar itakuwa imemezwa na Tanganyika! Kama unakumbuka, hata ripoti ya Warioba ilibainisha hofu yao hiyo na kuja na serikali tatu. Kwa anayetaka nina makala yangu inayojadili kwa kina hilo suluhisho. Anayetaka anipe email au nimpe inbox
nimeipenda hii kwa minajiri labda itatufikisha nipatakapo mimi kuwa na nchi moja na serkali moja. mana hii mipaka ni ya kikolon tu. asili yetu ni wamoja. na sijui kwanini hii serkali moja haipigiwi debe na wachangiaj wengi! tunasahau aina nyingine za muungano nje ya serkali moja ni kwa faida ya wapenda madaraka hasa!
 
dhana ya kumezwa sijui inatoa wapi mashiko endapo kila eneo la kiutawala linakuwa na uwakilishi kama ilivyo tanzania na wabunge! kinachotakiwa ni uwepo wa POLITICAL WILL. nionavyo mimi ni uchu wa madaraka na ubinafs ndo hofu kubwa ya wachache wanufaika. wananch wengi kinachoeleweka ni muunganiko wa mazima yan serkali moja. rais mmoja. bunge moja. sheria moja. mahakama moja. jeshi moja. uchumi mmoja. watu wamoja. sub zake ni mikoa na majimbo. mbona hawana au hatuna hofu ya rais au waziri kutokea ukanda flan kuwa atawabagua ukanda mwingine! bas tu njia ilobaki ya mda mrefu ni kuingiliana kijamii, kikazi, kindoa, kibiashara, kiardhi,kidini, mbelen labda atapatikana kiongoz wa maono, bila uchu, waungane. UMOJA NI NGUVU!
 
Kwanza hakuna raia wa Zaznibar na Tanganyika wote wanaitwa watanzania Ila wakazi wa......

Pili hakuna passport ya Tanzania na Zanzibar passport ni moja tu ya Tanzania inatumika na pande zote.

Pia hajuna visa kuingia ama kutoka Zanzibar na wapo watanganyika wengi Zanzibar wenye ukazi kule na huku pia.

Kuna baadhi ya hoja zako Zina msingi nyingine sijui umezipata wapi niliona niweke sawa hilo
 
Tofauti na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania isemayo Zanzibar ni sehemu ya JMT, Wazanzibar wengi huona Zanzibar ni nchi, ni taifa na ni dola. Aidha, katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010 inatamka wazi kuwa Zanzibar ni nchi.

Ieleweke kuwa muungano haupaswi kuwa jumuiko la viongozi la kupeana vyeo na kuwatisha wanaohoji utata na kero za muungano zisizoisha.

Muungano mzuri huunganisha mioyo ya watu kwa kushirikiana na kuhusiana kwa hiari, kwa usawa na kwa faida ya pande zote mbili. Sivyo ilivyo kwa Tanganyika na Zanzibar na watu wao. Hakuna urari wowote ule!

Wazanzibari wengi hujiona wana nchi yao na taifa lao, na hujitambulisha hivyo kimataifa. Hawajitambulishi kama Watanzania toka Tanzania! Soma shairi hili la Mzanzibari Mohammed K. Ghassani katika diwani yake ya N'na Kwetu (Sauti ya Mgeni Ugenini):

"Mapenzi nikupendayo, nchi yangu Zinjibari
Sitampenda mwenzio, na wala siko tayari

Mapenzi nikupendayo, nchi yangu ya uzawa
Kwa mwengine siwi nayo, na wala haitakuwa

Mapenzi nikupendayo, ewe taifa tukufu
Hatazuka mfanowo, wala sitakukhalifu

Mapenzi nikupendayo, dola yangu Zanzibar
Yang'ara kama kioo, wala hayatachakaa

Mapendo nikupendayo, watwani wangu watwani (nchi)
Twaa yote nilonayo, na wala sitakukhini (sitakufanyia khiyana)

Mapenzi nikupendayo, biladi yangu biladi (mji)
Takupenda kila leo, na daima yatazidi"

Je, hapo kuna muungano wa kweli toka katika mioyo ya Wazanzibari wengi? Hakuna! Je, Watanganyika tuna mapenzi kama hayo kwa Tanganyika??!!
 
Tuwe na states mbili zinazofanya Jamuhuri moja
Tanzania haiwezi kukwepa historia! Miungano yote ya kulazimisha inapata kifo cha asili. Iangalie USSR Kuanzia vita vikuu vya 2 Hadi 1990 au Yugoslavia chink ya Tito iliyogeuka kuwa nchi Saba za eneo la Baltic. Kwa hapa Africa angalia iliyokuwa Senegambia sasa hivi kuna Senegal na Gambia. Mambo ya muungano hayapaswi kulazimishwa bali watu waingie kwa hiari baada ya referandum.

USA ina muungano wa tofauti ambapo zile states ziliunganishwa kwenye umoja kwa civil wars zilizodumu kuanzia 1776 mpaka mwanzoni mwa karne ya 18. Lakini zile states Zina autonomy kubwa kisiasa na kiuchumi. Status ya Gavana wa California Schwazznegger yaweza kuwa ilikuwa kubwa kuliko hata PM wa Uingereza Tony Blair kwa wakati ule
 
Dawa ya huu Muungano ni kuvunjwa tu tukaishi kama majirani wema kuliko kulazimisha udugu wa damu usiokuepo.

Tuwe na makubaliano ya muingiliano wa kijamii tu, kama kutembealeana bila ya visa, Pamoja na kuwa na ruhusa ya mtu kufanya makaazi popote ndani ya nchi zetu, uruhusiwa ajira bila ya kuhitaji vibali vya kazi, na mazingira rahisi ya uwekezaji baina yetu pamoja na muingiliano wa kibiashara. Sharing baadhi ya Balozi pia litakua ni jambo jema.

Nilichogundua matatizo yetu ni ya kiutawala na si ya kijamii. Kwhaiyo suluhisho na serekali kutengenishwa tu kila mmoja awe nayake na maingiliano ya kijamii yaendelee kukuwepo.
 
Serikali moja au kila mtu ale kwa urefu wa kamba zake..

Kwenye huu muungano nyerere sijui aliwaza vitu gani..muungano gani hauna balance.

Yani upo kama host and parasite mode of life.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom