Suluhisho la Kudumu la Muungano Bora wa Tanganyika na Zanzibar Hili Hapa

Gwappo Mwakatobe

JF-Expert Member
Nov 22, 2019
1,494
1,874
1. Watu wa Tanganyika wenye makazi ya kudumu Zanzibar na Wazanzibar wenye makazi ya kudumu Tanganyika, wapewe uhiari, haki na uraia wa kuendelea kuishi Zanzibar au Tanganyika mtawalia.

2. Endapo Tanganyika na Zanzibar zitaendelea kuwa na uraia wa nchi moja, basi nchi hizi mbili ziwe na makubaliano maalum ya uraia maalum wa nchi mbili (Duo Exclusive Treaty on Special Dual Citizenship) kwa Watanganyika na Wazanzibar ambao watahiari kuwa na uraia wa nchi mbili baina ya Tanganyika na Zanzibar pekee.

3. Tanganyika na Zanzibar ziwe madola huru kama ilivyokuwa kabla ya muungano na zijiunge katika jumuiya au taasisi mbalimbali za kikanda au kimataifa ikiwa pamoja na Umoja wa Mataifa (UN), FIFA, nk.

4. Pasiwepo viza ya kusafiria kati ya Tanganyika na Zanzibar isipokuwa vitambulisho vya uraia au hati za kusafiria (passports) zitumike kumtambua Mtanganyika au Mzanzibar.

5. Iundwe Tume ya Mahusiano na Ujirani Mwema baina ya Tanganyika na Zanzibar (Commission for Relations and Good Neighbourhood). Tume hii pamoja na mambo yatakayojitokeza, ifanye yafuatayo:

(a) Kuweka utaratibu wa kuimarisha uhusiano na ulinzi wa pamoja wa Majeshi ya Ulinzi ya Watu wa Zanzibar (Zanzibar People’s Defence Forces - ZPDF) na Majeshi ya Ulinzi ya Watu wa Tanganyika (Tanganyika People’s Defence Forces -TPDF). Wanajeshi wa Tanganyika na Zanzibar wataendelea kutumika kwa pamoja kulinda watu na mipaka ya Tanganyika na Zanzibar.

(b) Kugawanya madeni ya nje kulingana na uwiano halisi wa jinsi yalivyotumika kusaidia nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar.

(c) Kuratibu balozi za nje ili ziendelee kutumiwa pamoja kiofisi (shared consulates) kwa Tanganyika na Zanzibar hadi wakati ambapo uwezo wa kila nchi utaruhusu kuwa na ubalozi wake.

(d) Kuratibu fedha na/au sarafu za aina moja ili ziendelee kutumika kihalali kati ya Tanganyika na Zanzibar ili kudumisha uhusiano na utambulisho wa kihistoria.

Hitimisho

Nikiwa mwanafunzi wa Mwalimu Nyerere nihitimishe kwa kusema alichokataza ni kufukuzana baina ya Watanganyika na Wazanzibar. Akaita dhambi kubwa sawa na kula nyama ya mtu. Hakukataza maelewano na makubaliano ya amani. Na sitegemei watu wanaokubaliana kwa amani watapigana. Wala si sahihi kulinganisha hilo na Sudan ambao walipigana miongo kadhaa wagawane nchi.

Wakati vita vya Uganda na Tanzania vikielekea ukingoni kabisa Mwalimu Nyerere alilaumiwa kuwa anataka kuimeza Uganda, wengine wakadiriki kusema kama alivyoimeza Zanzibar. Yeye alijibu kuwa lililo la msingi ni kudumisha amani na nchi jirani na kuwa na uhusiano mwema - si kuunganisha nchi. Tubakie majirani wema kama ilivyo kwa Zambia, Msumbiji, Rwanda, Kenya na kwingineko. Kuwa na mahusiano mema na jirani ni jambo la msingi na si lazima muunganishe nchi.

Kuna nchi nyingi tunahusiana nazo vizuri sana na kwa ukaribu japo haziko jirani, sembuse Zanzibar na Tanganyika! Undugu ni mahusiano mema si kuunganisha nchi. Na ujirani na udugu wa kihistoria upo kwa nchi zote tunazopakana nazo na si Tanganyika na Zanzibar pekee.

Muungano usilindwe kwa vitisho na kulazimishana, bali kujenga na kuimarisha mahusiano na ushirikiano mwema wa viongozi na wananchi wa hizi nchi mbili.

Kuna faida nyingi za kitaifa na kimataifa kwetu sisi Watanganyika kuwa nchi kamili, na vivyo hivyo kwa Zanzibar. Tusizibiane fursa na kuendelea kukerana au kulalamikiana!
 
Angalizo lako zuri sana na lenye hoja ya msingi sana!
Mimi naona suluhu ni aidha kukubali uwepo wa Muungano wa Serikali Tatu au hizi Nchi mbili zijitenge tu. Haiwezekani Wazanzibari watuone Watanganyika kama mizigo vile!

Na wakati huo huo na sisi Watanganyika tunaamini kabisa Wazanzibari ni chawa!! Yaani wanatunyonya tu damu!
 
Mtoa mada umejieleza vizuri, suluhisho hapa ni kila nchi kujijengea na kujivunia upande wake na kuishi kama majirani wema tu,kila upande utapata ari ya uzalendo na kujiletea maendeleo ya haraka na pia tutaondokana na siasa mivutano isiyokwisha.

Hizi ni nchi za kiafrika tunahitaji kuishi kwa urafiki na sio kuishi kwa miaka 50 mingine kutatua changamoto, muungano ambao msingi wake ni changamoto,hatutaweza kufika popote na tunapotezea wananchi wetu wakati wao wa maisha mazuri tu.
 
Tanzania haiwezi kukwepa historia! Miungano yote ya kulazimisha inapata kifo cha asili. Iangalie USSR Kuanzia vita vikuu vya 2 Hadi 1990 au Yugoslavia chink ya Tito iliyogeuka kuwa nchi Saba za eneo la Baltic. Kwa hapa Africa angalia iliyokuwa Senegambia sasa hivi kuna Senegal na Gambia. Mambo ya muungano hayapaswi kulazimishwa bali watu waingie kwa hiari baada ya referandum.

USA ina muungano wa tofauti ambapo zile states ziliunganishwa kwenye umoja kwa civil wars zilizodumu kuanzia 1776 mpaka mwanzoni mwa karne ya 18. Lakini zile states Zina autonomy kubwa kisiasa na kiuchumi. Status ya Gavana wa California Schwazznegger yaweza kuwa ilikuwa kubwa kuliko hata PM wa Uingereza Tony Blair kwa wakati ule
 
Ni kweli kabisa. La sivyo kero hazitaisha kamwe!

Ninachojifunza kwenye mijadala hii ni kuwa kila mzanzibari akiongoza JMT hoja za Muungano huibuka kwa nguvu sana upande wa TZ Bara lakini akiongoza mtanzania bara hoja hazipo kulikoni? Mfano kipindi cha Alhaji Ally Hassan Mwinyi ilitokea G55 na sasa kuna move hiyo!
 
Sioni suluhisho hasa ikizingatiwa kuwa hutambui kuwa kile unachokiita Tanganyika na Zanzibar ni creature of colonial demarcation of Africa. Kama ni kukubali huu ukoloni basi talakianeni kila mtu achukue chake na watu wake.

Raia wa nchi hizi za kikoloni wanaoishi kwenye nchi husika waishi kama wageni kuondoa udhia au warejee makwao. Tumechoka na chokochoko zisizo na kichwa wala miguu.
 
Mtoa mada umejieleza vizuri, suluhisho hapa ni kila nchi kujijengea na kujivunia upande wake na kuishi kama majirani wema tu,kila upande utapata ari ya uzalendo na kujiletea maendeleo ya haraka na pia tutaondokana na siasa mivutano isiyokwisha.
Hizi ni nchi za kiafrika tunahitaji kuishi kwa urafiki na sio kuishi kwa miaka 50 mingine kutatua changamoto, muungano ambao msingi wake ni changamoto,hatutaweza kufika popote na tunapotezea wananchi wetu wakati wao wa maisha mazuri tu.
Akina kabudi wanasema hakuna ndoa isiyo na misuguano. Bora kuwepo umahiri katika utatuzi wa hizo changamoto!
 
Ninachojifunza kwenye mijadala hii ni kuwa kila mzanzibari akiongoza JMT hoja za Muungano huibuka kwa nguvu sana upande wa TZ Bara lakini akiongoza mtanzania bara hoja hazipo kulikoni? Mfano kipindi cha Alhaji Ally Hassan Mwinyi ilitokea G55 na sasa kuna move hiyo!
Ni ubinafsi tu. Kama waliungana kinafiki itakula kwao!

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna anaetaka huu Muungano uwepo zaidi ya CCM ,maana wanajua fika Muungano ukiondoka na wao ndio mwisho wao wa ukiritimba,ndio kila mmoja wao utamsikia akipiga makelele nitaulinda muungano weee nitaulinda muungano akiongezea kwa hali na mali ,utazania wanapigania dini.
CCM mashee watoweni,msijibabaishe ,kama hamkuwatoa tunapeleka tena dua kwa ALLAH,mwengine wadondoke .
 
1. Watu wa Tanganyika wenye makazi ya kudumu Zanzibar na Wazanzibar wenye makazi ya kudumu Tanganyika, wapewe uhiari, haki na uraia wa kuendelea kuishi Zanzibar au Tanganyika mtawalia.

2. Endapo Tanganyika na Zanzibar zitaendelea kuwa na uraia wa nchi moja, basi nchi hizi mbili ziwe na makubaliano maalum ya uraia maalum wa nchi mbili (Duo Exclusive Treaty on Special Dual Citizenship) kwa Watanganyika na Wazanzibar ambao watahiari kuwa na uraia wa nchi mbili baina ya Tanganyika na Zanzibar pekee.

3. Tanganyika na Zanzibar ziwe madola huru kama ilivyokuwa kabla ya muungano na zijiunge katika jumuiya au taasisi mbalimbali za kikanda au kimataifa ikiwa pamoja na Umoja wa Mataifa (UN), FIFA, nk.

4. Pasiwepo viza ya kusafiria kati ya Tanganyika na Zanzibar isipokuwa vitambulisho vya uraia au hati za kusafiria (passports) zitumike kumtambua Mtanganyika au Mzanzibar.

5. Iundwe Tume ya Mahusiano na Ujirani Mwema baina ya Tanganyika na Zanzibar (Commission for Relations and Good Neighbourhood). Tume hii pamoja na mambo yatakayojitokeza, ifanye yafuatayo:

(a) Kuweka utaratibu wa kuimarisha uhusiano na ulinzi wa pamoja wa Majeshi ya Ulinzi ya Watu wa Zanzibar (Zanzibar People’s Defence Forces - ZPDF) na Majeshi ya Ulinzi ya Watu wa Tanganyika (Tanganyika People’s Defence Forces -TPDF). Wanajeshi wa Tanganyika na Zanzibar wataendelea kutumika kwa pamoja kulinda watu na mipaka ya Tanganyika na Zanzibar.

(b) Kugawanya madeni ya nje kulingana na uwiano halisi wa jinsi yalivyotumika kusaidia nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar.

(c) Kuratibu balozi za nje ili ziendelee kutumiwa pamoja kiofisi (shared consulates) kwa Tanganyika na Zanzibar hadi wakati ambapo uwezo wa kila nchi utaruhusu kuwa na ubalozi wake.

(d) Kuratibu fedha na/au sarafu za aina moja ili ziendelee kutumika kihalali kati ya Tanganyika na Zanzibar ili kudumisha uhusiano na utambulisho wa kihistoria.

Hitimisho

Nikiwa mwanafunzi wa Mwalimu Nyerere nihitimishe kwa kusema alichokataza ni kufukuzana baina ya Watanganyika na Wazanzibar. Akaita dhambi kubwa sawa na kula nyama ya mtu. Hakukataza maelewano na makubaliano ya amani. Na sitegemei watu wanaokubaliana kwa amani watapigana. Wala si sahihi kulinganisha hilo na Sudan ambao walipigana miongo kadhaa wagawane nchi.

Wakati vita vya Uganda na Tanzania vikielekea ukingoni kabisa Mwalimu Nyerere alilaumiwa kuwa anataka kuimeza Uganda, wengine wakadiriki kusema kama alivyoimeza Zanzibar. Yeye alijibu kuwa lililo la msingi ni kudumisha amani na nchi jirani na kuwa na uhusiano mwema - si kuunganisha nchi. Tubakie majirani wema kama ilivyo kwa Zambia, Msumbiji, Rwanda, Kenya na kwingineko. Kuwa na mahusiano mema na jirani ni jambo la msingi na si lazima muunganishe nchi.

Kuna nchi nyingi tunahusiana nazo vizuri sana na kwa ukaribu japo haziko jirani, sembuse Zanzibar na Tanganyika! Undugu ni mahusiano mema si kuunganisha nchi. Na ujirani na udugu wa kihistoria upo kwa nchi zote tunazopakana nazo na si Tanganyika na Zanzibar pekee.

Muungano usilindwe kwa vitisho na kulazimishana, bali kujenga na kuimarisha mahusiano na ushirikiano mwema wa viongozi na wananchi wa hizi nchi mbili.

Kuna faida nyingi za kitaifa na kimataifa kwetu sisi Watanganyika kuwa nchi kamili, na vivyo hivyo kwa Zanzibar. Tusizibiane fursa na kuendelea kukerana au kulalamikiana!
Tuunde serkali moja tu lakini makao makuu ya serikali yaweko Pemba tena katika kisiwa cha Kojani.
 
Hakuna anaetaka huu Muungano uwepo zaidi ya CCM ,maana wanajua fika Muungano ukiondoka na wao ndio mwisho wao wa ukiritimba,ndio kila mmoja wao utamsikia akipiga makelele nitaulinda muungano weee nitaulinda muungano akiongezea kwa hali na mali ,utazania wanapigania dini.
CCM mashee watoweni,msijibabaishe ,kama hamkuwatoa tunapeleka tena dua kwa ALLAH,mwengine wadondoke .
Well saida hakuna anayetaka huu muungano fake
 
Mtoa mada umejieleza vizuri, suluhisho hapa ni kila nchi kujijengea na kujivunia upande wake na kuishi kama majirani wema tu,kila upande utapata ari ya uzalendo na kujiletea maendeleo ya haraka na pia tutaondokana na siasa mivutano isiyokwisha.
Hizi ni nchi za kiafrika tunahitaji kuishi kwa urafiki na sio kuishi kwa miaka 50 mingine kutatua changamoto, muungano ambao msingi wake ni changamoto,hatutaweza kufika popote na tunapotezea wananchi wetu wakati wao wa maisha mazuri tu.
Kwanini viongozi wanatulazimisha kwenye muungano wao huu?
 
Wazenji wengi wapewe ajira bara na wabara wengi wapewe ajira Zenji halafu wazaliane mchanganyiko hadi washindwe kubaguana.
Kama tu tunavyoheshimiana uislam na ukristo ,,maana kuna ndoa nyingi tu ambazo zimechanganya dini hizi mbili na uzao mwingi uliotokana na familia za aina hiyo na hivyo kufanikiwa kuondoa ubaguzi.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom