Suluhisho la kudumu la Machinga ni kuifumua dhana nzima ya Ujasiriamali na Kujiajiri

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,397
3,884
Moja ya kosa kubwa ambalo limefanyika kwa muda mrefu toka dhana ya Ujasiriamali ianze kupigiwa chapuo, ni kusahau na kushindwa kuambatanisha dhana hiyo na elimu ya uwajibikaji kwa jamii, sera madhubuti za uwezeshaji kwa wafanyabiashara wa kati na elimu ya maadili ya biashara (business ethics).

Ukiacha yale yanayoonekana mema yaliyokuja na Ujasiriamali, lakini kuna mengi mabaya ambayo yameletwa pia na hiyo dhana. Tumekuwa jamii ya watu wasio na nidhamu kazini, tumejenga imani kuwa waajiri wanatunyonya kwa hiyo ni sahihi kudokoa na kuiba ili tukafanye biashara zetu wenyewe.

Huwa nashangaa sana ninaposikia mtu anaposisitiza kuwa kuajiriwa ni utumwa, najiulizaga huyu anayesema hivi atakapoenda kuanzisha biashara yake, hao atakaowaajiri watakuwa ni watumwa wake? Sikatai unyonywaji upo kwa baadhi ya waajiri ila hii imani ya kuwa kuajiriwa ni utumwa imeleta chuki na tamaa kwa wengi.

Kwa kuwa wengi wanaofanya biashara sasa hivi katika level zote hawana elimu ya kutosha ya maadili ya biashara, imepelekea bidhaa feki kuuzwa, bei zisizozingatia gharama kwa muuzaji, huduma mbovu kwa wateja, ufisadi na utapeli mwingine.

Nini mapendekezo yangu?

Kwanza, tuifumue dhana nzima ya Ujasiriamali. Tutoke kwenye kusisitiza watu wajiajiri, twende kwenye kusisitiza watu 'wajiajiri na waajiri wengine'. Hatuna uchumi ambao kila mtu anaweza kuwa mfanyabiashara. Matokeo yake kila mtu anafanya biashara zile zile tu halafu zote ni kama za uchuuzi tu.

Pili, tufumue mfumo wetu wa kodi, utoaji leseni na usimamizi wa biashara nchini. Hili limeshaongelewa sana na wadau mbalimbali kwa muda mrefu kwa hiyo sitalielezea sana. Ila lengo kuu liwe kuwezesha watu wenye nia ya kufanya biashara waweze kuwa na mitaji mikubwa ya kufanya biashara na nafasi ya kuajiri wengine. Mfanyabiashara mmoja akiweza kuwatoa machinga watano wakaajiriwa kwenye duka moja, umepunguza vibanda vitano ambavyo vingejengwa barabarani au vijana watano kutembeza bidhaa katikati ya barabara.

Tatu, tukazie kutoa na kusambaza elimu ya maadili ya biashara katika ngazi zote. Kwa kiasi kikubwa sheria za nchi, ikiwemo watu wanaojenga hovyo vibanda vya biashara katika maeneo wasiyoruhusiwa ni kwa sababu hawana elimu hii. Naomba nieleweke, kutokuwa na elimu ya maadili ya biashara haimaanishi mtu anakuwa hajui kuwa wanatenda kosa. Elimu inamsaidia mtu kujizuia kutenda kosa hata pale anapopata vishawishi au msukumo wa kufanya hivyo.
 
Picha linaanza umachinga sio ujasiriamali ni biashara ndogo ndogo hivi ni vitu viwili tofauti sana.

Tatizo machinga wwmegeuka chanzo cha madaraka, naweza sema ndio kundi linalopendelewa zaidi kwa sasa wamewapiga chini watumishi (rafiki mkuu wa serikali (zama zile))
 
Back
Top Bottom