SoC01 Suluhisho kupunguza utapeli unaofanywa na madalali

Stories of Change - 2021 Competition

JOHNGERVAS

JF-Expert Member
Mar 22, 2016
470
597
Salaam Wakuu.

Kwanza kabisa kila mmoja anafahamu
Watu wengi katika kupata ardhi zao au nyumba za kupangisha wametumia watu wanaoitwa madalali. Tunafahamu kwa uchache juu ya shughuli zao wanazofanya kila siku.

NAMNA WANAVYOFANYA KAZI

Mara nyingi kazi za madali hawa hazina formula maalum lakini mfumo wanaotumia Mara nyingi hasa hawa wa Kupangisha vyumba au nyumba wanachukua posho yao Kiasi cha Kodi utakayolipa kwa mwezi mmoja. Mfano kama kodi yako ni laki kwa mwezi wewe utalazimika kumpa laki moja.

Pia hutoza Posho kati ya 5000-25000 kama posho ya huduma ya kwenda kukuonyesha Chumba,nyumba au kiwanja.

UTAPELI,NAMNA WANAVYOLIZA WATU.

pamoja na kuwa Msaada mkubwa hawa madalali,wengi wao wameharibu na kuchafua kabisa tasnia hii kwa kujihusisha na utapeli. Mfano unaweza kumtafuta dalali kwamba unahitaji chumba mbezi,kimara,ubungo n.k na unamtajia sifa zote za nyumba au chumba unachohitaji dalali kwasababu anajua utampa service charge anakuambia vipo njoo ucheki. Anakuambia uje uangalie ilihali akijua kabisa kwamba hana chumba ila anajua atakachokifanya.

Ukifika atakupeleka kwenye nyumba ambayo haina sifa ulizomtajia atakuambia hapa ukishalipia tu mwenye nyumba atarekebisha,ukishalipia tu umeliwa. Ama anatakuzungusha mitaa tofauti tofauti atakuonyesha nyumba au vyumba ambavyo havina sifa ulizomtajia afuu baadae anakuambia umlipe chake kama hutaki.

Utapeli mwingine ni Kushirikiana na wenye nyumba kupangisha nyumba Mara Mbili. Dalali atakupeleka kwenye nyumba ataongea na mwenye nyumba atamuuliza kama vyumba vipo,mwenye nyumba atamuambia vilikuwepo ila vimejaa japo waliolipia wengine hawajahamia. Watafanya mipango ya kukutapeli utapelekwa utaona vyumba ukiridhika unalipia atakupa mkataba "MAGUMASHI" utampa na dalali chake. Siku ukitaka kuja kuhamia utakuta tayari kuna MTU mwingine. Ukimuuliza dalali atakuambia mwambie mwenye nyumba,ukimtafuta mwenye nyumba atakuambia Mimi sipo mtafute dalali. Ukimsumbua sana atakuambia ni kweli kuna MTU alikuja subiri nitakulipa hela yako,atakupa kidogo kidogo na hatamalizia yote.

Utapeli mwingine unaofanyika wakishirikiana na wenye nyumba. Labda mwenye nyumba anaweza kuwa nyumba yake anapangisha 150k Dalali anamwambia kwa sifa za nyumba yako nitakuletea wateja wa laki mbili kwasababu ya tamaa zao ili apate cha juu atanwambia hii ya udalali (cha juu) iliyoongeka mm nitachukua elf 25 kila mwezi. Watu wanaumizwa sana na hawa madalali wameibiwa,wametapeliwa n.k

Upo wizi na utapeli Mkubwa unaofanywa na madali wanaweza hata kukusainisha mkataba feki wakakupangishia nyumba ya mtu.

Sasa ili kuepukana na utapeli unaofanywa na madalali tunaweza kufanya yafuatayo.

KUSHIRIKISHA SERIKALI ZA MITAA/VIJIJI
Tungeweza kushirikisha viongozi wa serikali za mitaa tukaepukana na usumbufu na utapeli wa madali kwa kufanya yafuatayo

Mwenye kuuza,kupangisha,nyumba au kiwanja apelekee taarifa zote pamoja na sifa ya kitu husika aache na namba zake. Ili kama atatokea MTU anayehitaji nyumba au kiwanja Mbezi mtaa wa msigani anaenda moja kwa moja serikali za mitaa anaulizia anapewa sifa za nyumba zilizopo anachagua na serikali za mitaa wachukue hata 10% ya kodi yake. Hii itasaidia kuongeza mapato kwenye serikali za mitaa na kupunguza wimbi la matapeli lakini pia mikataba itafanyika kisheria.

Hii ndio njia pekee ya kuondokana na matapeli.
 
Back
Top Bottom