Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Kwa kadiri ya kwamba Sultani Jamsheed Bin Abdallah anaendelea kujitambua kuwa ni Sultani wa Zanzibar na kwa kadiri ya kwamba uzao wake unakidai kiti hicho kama urithi wa haki yao; na kwa kadiri ya kwamba wapo Wazanzibari ambao wanamtambua Jamsheed kama Sultani wao na ya kwamba wako tayari kurejesha status quo ya 1963 (ambapo Sultani alikuwa ni mfalme wa heshima Kikatiba kama ilivyo Uingereza - japo tofauti kidogo) basi juhudi zote za maridhiano haziwezi kufanikiwa kwani Sultani na uzao wake watakuwa ni kama kivuli juu ya Zanzibar na watu wake.
Ili kuleta mapatano ya kweli (kama anavyosema Lula) basi hatima ya Sultani na uzao wake ni lazima ijadiliwe.
a. Je, ni jinsi gani Bw. Jamsheed anaweza kurudi Zanzibar bila ya kuwa na mamlaka ya Usultani yeye na uzao wake milele?
b. Je, Bw. Jamsheed anaweza kuwa na nafasi yoyote ya heshima katika Zanzibar ukiondoa ya kutambuliwa kama Sultani?
c. Je, akikubali kukana kiti cha Usultani, yeye mwenyewe, wanawe na wale wote walio katika mnyonyoro wa urithi milele anaweza kurudi Zanzibar na sehemu ya upatanishi ni kumrudishia baadhi ya mali zake zilizochukuliwa baada ya mapinduzi ya 1964?
d. Je, aweza kurudi pasipo kuwa na nafasi yoyote ya kisiasa na kukatazwa yeye mwenyewe na warithi wake kushiriki katika uongozi wa chama chochote cha siasa?
e. Je, Bw. Jamsheed katika kuleta mapatano yuko tayari kutambua na kukubali uwepo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Uzao wa Jamsheed (allexperts):
*Prince Sayyid Ali bin Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Khalifa bin Jamshid Al-Said
*Princess Sayyida Matuqa bint Jamshid Al-Said (1957-)
*Prince Sayyid Abdullah bin Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Wasfi bin Jamshid Al-Said (1972-)
*Princess Sayyida Adla bint Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Gharib bin Jamshid Al-Said
Ningependa CCM na CUF watoe misimamo yao kwa maswali yangu hayo.
Kwa habari zaidi ya line of succession ya Masultani wa Zanzibar BONYEZA HAPA