Sultani Jamsheed hakukana kiti cha Usultani wa Zanzibar

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
i1658_sultan.jpg

Kwa kadiri ya kwamba Sultani Jamsheed Bin Abdallah anaendelea kujitambua kuwa ni Sultani wa Zanzibar na kwa kadiri ya kwamba uzao wake unakidai kiti hicho kama urithi wa haki yao; na kwa kadiri ya kwamba wapo Wazanzibari ambao wanamtambua Jamsheed kama Sultani wao na ya kwamba wako tayari kurejesha status quo ya 1963 (ambapo Sultani alikuwa ni mfalme wa heshima Kikatiba kama ilivyo Uingereza - japo tofauti kidogo) basi juhudi zote za maridhiano haziwezi kufanikiwa kwani Sultani na uzao wake watakuwa ni kama kivuli juu ya Zanzibar na watu wake.

Ili kuleta mapatano ya kweli (kama anavyosema Lula) basi hatima ya Sultani na uzao wake ni lazima ijadiliwe.

a. Je, ni jinsi gani Bw. Jamsheed anaweza kurudi Zanzibar bila ya kuwa na mamlaka ya Usultani yeye na uzao wake milele?

b. Je, Bw. Jamsheed anaweza kuwa na nafasi yoyote ya heshima katika Zanzibar ukiondoa ya kutambuliwa kama Sultani?

c. Je, akikubali kukana kiti cha Usultani, yeye mwenyewe, wanawe na wale wote walio katika mnyonyoro wa urithi milele anaweza kurudi Zanzibar na sehemu ya upatanishi ni kumrudishia baadhi ya mali zake zilizochukuliwa baada ya mapinduzi ya 1964?

d. Je, aweza kurudi pasipo kuwa na nafasi yoyote ya kisiasa na kukatazwa yeye mwenyewe na warithi wake kushiriki katika uongozi wa chama chochote cha siasa?

e. Je, Bw. Jamsheed katika kuleta mapatano yuko tayari kutambua na kukubali uwepo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Uzao wa Jamsheed (allexperts):

*Prince Sayyid Ali bin Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Khalifa bin Jamshid Al-Said
*Princess Sayyida Matuqa bint Jamshid Al-Said (1957-)
*Prince Sayyid Abdullah bin Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Wasfi bin Jamshid Al-Said (1972-)
*Princess Sayyida Adla bint Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Gharib bin Jamshid Al-Said

Ningependa CCM na CUF watoe misimamo yao kwa maswali yangu hayo.

Kwa habari zaidi ya line of succession ya Masultani wa Zanzibar BONYEZA HAPA
 
Mzee elimu unayoitoa ni kitu muhimu sana. I just wish hawa viongozi wetu wangelikuwa na muda wa kwenda into details na kutoacha any stone unturned. Vinginevyo wananchi watakujastukia wamerudishwa kwenye enzi ya usultani bila kujijua.
 
Kama hamuamini maneno yangu waambieni kina Seif na Karume watoe wito kwa Jamsheed kukana kiti cha Usultani wa Zanzibar muone kama kule kugawanyikwa kwa karibu 50:50 kutaishia wapi!
 
Well put Mwanakijiji. Kuna sehemu nilisema Mapatano ya UKWELI hayatatokea Zanzibar milele.

Hii yao ni kama Israel na Palestine
 
Kwani asili ya usultani wake ni wa visiwani zanzibar au nje ya zanzibar??????
kama asili ya usultani wake ni wa zanzibar si mpaka huo umma wake umtake jee kama haumtaki inakuwaje??? [kuna nchi nyingi ambazo zilikuwa na falme hizi lakini leo hazi [[russia,france,bulgaria,greece,egypt,syria etc etc]
Na kama usultani wake asili yake ni kutoka nje [kuvamia nchi] haki hizo atazipata wapi??????
 
Abeid Karume aliliona hili. Akaharakisha kwelikweli Muungano. Kijana wake wa kuzaa, Amani, anadhani kuna maridhiano bila kumshirikisha Sultani Jamsheed na watu wake wengi tu mbali na hao walioko CUF. Haitawezekana.
 
Kwa kadiri ya kwamba Sultani Jamsheed Bin Abdallah anaendelea kujitambua kuwa ni Sultani wa Zanzibar na kwa kadiri ya kwamba uzao wake unakidai kiti hicho kama urithi wa haki yao; na kwa kadiri ya kwamba wapo Wazanzibari ambao wanamtambua Jamsheed kama Sultani wao na ya kwamba wako tayari kurejesha status quo ya 1963 (ambapo Sultani alikuwa ni mfalme wa heshima Kikatiba kama ilivyo Uingereza - japo tofauti kidogo) basi juhudi zote za maridhiano haziwezi kufanikiwa kwani Sultani na uzao wake watakuwa ni kama kivuli juu ya Zanzibar na watu wake.

Ili kuleta mapatano ya kweli (kama anavyosema Lula) basi hatima ya Sultani na uzao wake ni lazima ijadiliwe.

a. Je, ni jinsi gani Bw. Jamsheed anaweza kurudi Zanzibar bila ya kuwa na mamlaka ya Usultani yeye na uzao wake milele?

b. Je, Bw. Jamsheed anaweza kuwa na nafasi yoyote ya heshima katika Zanzibar ukiondoa ya kutambuliwa kama Sultani?

c. Je, akikubali kukana kiti cha Usultani, yeye mwenyewe, wanawe na wale wote walio katika mnyonyoro wa urithi milele anaweza kurudi Zanzibar na sehemu ya upatanishi ni kumrudishia baadhi ya mali zake zilizochukuliwa baada ya mapinduzi ya 1964?

d. Je, aweza kurudi pasipo kuwa na nafasi yoyote ya kisiasa na kukatazwa yeye mwenyewe na warithi wake kushiriki katika uongozi wa chama chochote cha siasa?

e. Je, Bw. Jamsheed katika kuleta mapatano yuko tayari kutambua na kukubali uwepo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Uzao wa Jamsheed (allexperts):

*Prince Sayyid Ali bin Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Khalifa bin Jamshid Al-Said
*Princess Sayyida Matuqa bint Jamshid Al-Said (1957-)
*Prince Sayyid Abdullah bin Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Wasfi bin Jamshid Al-Said (1972-)
*Princess Sayyida Adla bint Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Gharib bin Jamshid Al-Said

Ningependa CCM na CUF watoe misimamo yao kwa maswali yangu hayo.

Once again another Conspiracy mie naomba utupe source za reference zako na data kama zipo kama huna tafadhali usiyazungumze haya!!!!

Pia zanzibar kweli yanakuja mapinduzi kama hamjui but this time ni kutoka kwa vijana kwani akina shamhuna na wenzie wanazeeka na wanapungua idadi tunabakia sie tusiyajua mapinduzi wala kuyapigania, wamechoka na hii bullshit propaganda ya ugozi lazima pawepo na level playing field na sie eti sisi waafrika, wale waarabu etc. hii haijengi nchi na imeshakaa nayo vya kutosha (miaka zaidi ya 40 nadhani inatosha!!!!). Sasa yanahitajika maendeleo na sio blah blah!!!!
 
Sio kwa WAZANZIBARI na MAPINDUZI DAIMA.

Yap na sasa ni mapinduzi ya maendeleo Uungwana wa maneno na propaganda za ugozi hazifai kubezwa wakati wanakufa na njaa zanzibar. Biashara ya madawa kulevya imetapakaa zanzibar. Maadili ndio usiseme yameporomoka kabisa!!!!
 
Kwa kadiri ya kwamba Sultani Jamsheed Bin Abdallah anaendelea kujitambua kuwa ni Sultani wa Zanzibar na kwa kadiri ya kwamba uzao wake unakidai kiti hicho kama urithi wa haki yao; na kwa kadiri ya kwamba wapo Wazanzibari ambao wanamtambua Jamsheed kama Sultani wao na ya kwamba wako tayari kurejesha status quo ya 1963 (ambapo Sultani alikuwa ni mfalme wa heshima Kikatiba kama ilivyo Uingereza - japo tofauti kidogo) basi juhudi zote za maridhiano haziwezi kufanikiwa kwani Sultani na uzao wake watakuwa ni kama kivuli juu ya Zanzibar na watu wake.

Ili kuleta mapatano ya kweli (kama anavyosema Lula) basi hatima ya Sultani na uzao wake ni lazima ijadiliwe.
Mzee Mwanakijiji, haya mambo ya Sultan ni magumu, niliwahi pata mnong'ono Sultan Jamseed alimpa mimba mjakazi wa Kipemba, kwenye Kasri la kifalme, ili kufunika kombe, siri isivuje, yule mjakazi akaozeshwa kwa mtu, kwa ahadi atatunzwa maisha yake yote. Kwenye ndoa hiyo, kazaliwa mtoto wa kiume mwana Sultan Jamsid

Huyo mtoto mpaka sasa bado angalipo yupo hai, bukheri wa afya japo ni mtu mzima sasa, na bado anatunzwa na ukoo wa Kisultan, ili deal isishitukiwe, wafadhili wa ukoo huu wa Kisultani, wanafadhiliwa na Sultani wa Brunei ambaye ni nasaba na Jamsid. Kwa vile mtoto huyo mwenye damu ya Kisultan yupo, na ni siri, subirini baada ya kuanza serikali ya umoja wa kitaifa, siri zitaanza kufichuka.

Zanzibar kuna mambo, visa, na mikasa. Hii ni simulizi nyingine ya minong'ono. kuna ndugu wawili waligombea mkate, aliyewapa mkate, aliwapa kwa heshima ya baba yao, ndugu mmoja akapata, mwenzie akakosa, yule aliyekosa akasisitiza mkate mwingine ukitolewa, lazima sasa iwe zamu yake. Wajuzi wa mambo wakasema, haitapendeza huo mkate kile siku uonekane kama mnapokezana, wenyewe waweza fikiria ni kama usultani.

Huyu ndugu aliyekosa ameng'angania, lazima na yeye apate, kwani ndiye mwenye haki rasmi ya kupata ule mkate toka mwanzo, eti yeye ndiye mtoto halali wa wa yule baba, aliyepata kwanza, alikuwa ni wa kufikia, ila ni siri tuu!.Ni simulizi tuu. kama Alfu Lela U Lela, au siku Elfu na Moja.
 
Baraza la wawakilishi linasisitiza kwamba serikali hiyo ya umoja wa kitaifa itakayoundwa itaendelea kuheshimu na kuthamini misingi mikuu ya mapinduzi ya tarehe 12.1.1964.
Hiyo ni moja ya hoja iliyowasilishwa na CUF barazani, kwa hiyo kikatiba hata CUF akiingia madarakani hakuna nafasi ya Sultani.

Someni katiba ya Zanzibar kabla hamjakurupuka na kudai usultani utarudishwa pindipo CUF itaingia madarakani.Zanzibar ni nchi inayoendeshwa kikatiba na kanuni za utawala bora.
 
Mzee Mwanakijiji, haya mambo ya Sultan ni magumu, niliwahi pata mnong'ono Sultan Jamseed alimpa mimba mjakazi wa Kipemba, kwenye Kasri la kifalme, ili kufunika kombe, siri isivuje, yule mjakazi akaozeshwa kwa mtu, kwa ahadi atatunzwa maisha yake yote. Kwenye ndoa hiyo, kazaliwa mtoto wa kiume mwana Sultan Jamsid

Huyo mtoto mpaka sasa bado angalipo yupo hai, bukheri wa afya japo ni mtu mzima sasa, na bado anatunzwa na ukoo wa Kisultan, ili deal isishitukiwe, wafadhili wa ukoo huu wa Kisultani, wanafadhiliwa na Sultani wa Brunei ambaye ni nasaba na Jamsid. Kwa vile mtoto huyo mwenye damu ya Kisultan yupo, na ni siri, subirini baada ya kuanza serikali ya umoja wa kitaifa, siri zitaanza kufichuka.

Zanzibar kuna mambo, visa, na mikasa. Hii ni simulizi nyingine ya minong'ono. kuna ndugu wawili waligombea mkate, aliyewapa mkate, aliwapa kwa heshima ya baba yao, ndugu mmoja akapata, mwenzie akakosa, yule aliyekosa akasisitiza mkate mwingine ukitolewa, lazima sasa iwe zamu yake. Wajuzi wa mambo wakasema, haitapendeza huo mkate kile siku uonekane kama mnapokezana, wenyewe waweza fikiria ni kama usultani.

Huyu ndugu aliyekosa ameng'angania, lazima na yeye apate, kwani ndiye mwenye haki rasmi ya kupata ule mkate toka mwanzo, eti yeye ndiye mtoto halali wa wa yule baba, aliyepata kwanza, alikuwa ni wa kufikia, ila ni siri tuu!.Ni simulizi tuu. kama Alfu Lela U Lela, au siku Elfu na Moja.
Kazi ipo mwaka huu.Inaelekea siasa za kisiwani zimejaa kina Leonard Da Vinchi kibao maana hapa hata sielewi kunani
 
e. Je, Bw. Jamsheed katika kuleta mapatano yuko tayari kutambua na kukubali uwepo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Sio sultani tuu, wazanzibari wenyewe hawajakubali bado kuwepo kwa muungano.

Bora tuanze na hao walio ndani ya visiwa kwanza, halafu ndio tutizame kama muungano utakuwepo...then tumuulize na Sultani
 
Yap na sasa ni mapinduzi ya maendeleo Uungwana wa maneno na propaganda za ugozi hazifai kubezwa wakati wanakufa na njaa zanzibar. Biashara ya madawa kulevya imetapakaa zanzibar. Maadili ndio usiseme yameporomoka kabisa!!!!
Ndugu yangu haya ni maneno mazito. Tumejikita sana kupiga domo tunajisahau sisi ni kina nani. This life has a meaning and we cant know that meaning if we spend alot of our time on issues that don't add any value to us as individuals. Naogopa sana kuhisi hivyo, lakini mara nyingi wanasiasa wanatutumia kuhitimisha agenda zao za kupata madaraka, pengine bila kutoa msaada wowote kwetu baada ya kuyakwaa madaraka hayo. Hii ya Zanzibar hii haijakaa katika kutafuta mwelekeo mzuri tu wa siku za usoni, ila pia imebeba ajenda nzito ya baadhi ya watu kutaka kupata hayo madaraka kwa gharama yoyote ile. Ndiyo maana naona nguvu imeelekezwa kuufukia chini muungano ambao naona baadhi wanataka kusema ndiyo chanzo cha matatizo ya kisiasa ya Zanzibar.Mimi sitaki kuamini hivyo maana yale mapinduzi yalikuja kwasababu kulikuwa na matatizo ya kisiasa. Je nayo yaliletw na muungano?
 
Sio sultani tuu, wazanzibari wenyewe hawajakubali bado kuwepo kwa muungano.

Bora tuanze na hao walio ndani ya visiwa kwanza, halafu ndio tutizame kama muungano utakuwepo...then tumuulize na Sultani

Ili kukata mzizi wa fitna, kwa nini wasiulizwe raia wote wa JMT? Ikiwa upande mmoja utaukataa Muungano basi uvunjwe. Hii imani kuwa watanganyika wanautaka Muungano inabidi ipimwe. Watu wanaweza kushangaa hapo wazanzibari wakautaka na watanganyika wakaukataa!

Amandla......
 
Kwa kadiri ya kwamba Sultani Jamsheed Bin Abdallah anaendelea kujitambua kuwa ni Sultani wa Zanzibar na kwa kadiri ya kwamba uzao wake unakidai kiti hicho kama urithi wa haki yao; na kwa kadiri ya kwamba wapo Wazanzibari ambao wanamtambua Jamsheed kama Sultani wao na ya kwamba wako tayari kurejesha status quo ya 1963 (ambapo Sultani alikuwa ni mfalme wa heshima Kikatiba kama ilivyo Uingereza - japo tofauti kidogo) basi juhudi zote za maridhiano haziwezi kufanikiwa kwani Sultani na uzao wake watakuwa ni kama kivuli juu ya Zanzibar na watu wake.

Ili kuleta mapatano ya kweli (kama anavyosema Lula) basi hatima ya Sultani na uzao wake ni lazima ijadiliwe.

a. Je, ni jinsi gani Bw. Jamsheed anaweza kurudi Zanzibar bila ya kuwa na mamlaka ya Usultani yeye na uzao wake milele?

b. Je, Bw. Jamsheed anaweza kuwa na nafasi yoyote ya heshima katika Zanzibar ukiondoa ya kutambuliwa kama Sultani?

c. Je, akikubali kukana kiti cha Usultani, yeye mwenyewe, wanawe na wale wote walio katika mnyonyoro wa urithi milele anaweza kurudi Zanzibar na sehemu ya upatanishi ni kumrudishia baadhi ya mali zake zilizochukuliwa baada ya mapinduzi ya 1964?

d. Je, aweza kurudi pasipo kuwa na nafasi yoyote ya kisiasa na kukatazwa yeye mwenyewe na warithi wake kushiriki katika uongozi wa chama chochote cha siasa?

e. Je, Bw. Jamsheed katika kuleta mapatano yuko tayari kutambua na kukubali uwepo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Uzao wa Jamsheed (allexperts):

*Prince Sayyid Ali bin Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Khalifa bin Jamshid Al-Said
*Princess Sayyida Matuqa bint Jamshid Al-Said (1957-)
*Prince Sayyid Abdullah bin Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Wasfi bin Jamshid Al-Said (1972-)
*Princess Sayyida Adla bint Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Gharib bin Jamshid Al-Said

Ningependa CCM na CUF watoe misimamo yao kwa maswali yangu hayo.

daah! Huyu jamaa mkorofi kweli, bado unaendele kuwachoche tu na mahistoria wsielewane. WaZENJ wamesema wanasahau yaliyopita wewe unawang'ang'aniza tu! Na mahistoria yako ya kichochezi, utakosa nini wewe WaZENJ wakielewana?, hakuna lisilo na mwisho, lazima usome alama nyakati halafu ukubali matokeo, la sivyo utaonekana wa ajabu. Hakuna Mzenj anaeongelea habari za sultani, wewe hayo umeyapata wapi, huo ndio uchochezi usio na faida. Kizazi kilichopo sasa zenj hakuna yoyote alie athiriwa na Usltani, ni kizazi kipya kinacho hitaji maendeleo kwa gharama yoyote, ni kizazi kinacho angalia mbele sio kurudi nyuma kama unavyo taka wewe, historia hiyo uliyo bebeshwa wewe Wa Zenj hawana haja nayo kwa hiyo usipoteze muda, kama wewe ni muungwana kweli andika yatakayo wasaidia Wazenj na sio huu uchochezi wako.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom