Sultani Jamsheed hakukana kiti cha Usultani wa Zanzibar

*Prince Sayyid Ali bin Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Khalifa bin Jamshid Al-Said
*Princess Sayyida Matuqa bint Jamshid Al-Said (1957-)
*Prince Sayyid Abdullah bin Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Wasfi bin Jamshid Al-Said (1972-)
*Princess Sayyida Adla bint Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Gharib bin Jamshid Al-Said

[/QUOTE]
Hee kumbe watoto wa Sultan nao wanaitwa maPrince na maPrincess na je hiyo Sayyid inamaanisha nini?
 
Hapa sioni kwanini CCM wanaogopa kuongelea hili, Usultani unaweza rudi kama CCM hawakuwa makini kwani kama kuna kundi kubwa linalo utambua utawala wa kisultani mpaka kusabisa 50/50 kwenye uchaguzi dawa ni kuliongelea na kutafuta dawa ya kudumu badala ya vita ya chini kwa chini.

Kuna conspirancy mbili hapa, siku za nyuma niliamini kuwa CUF ndio wanaowezarejesha Usultani lakini kama kinachosemwa hapo juu kuhusu mtoto wa mjakazi ni kweli, then usultani tunaweza uzuia sisi wa bara tu otherwise utarudi muda si mrefu na CCM hawataweza zuia
 

Wasipotoa? Unasahau sasa 'wameungana'?
CCM (Zanzibar) na CUF (Zanzibar) misimamo yao hutoa Baraza la Wawakilishi. Humu tunaweza kueleza hamasa na chnagamoto tu. Na kwa hilo la Jamsheed halina umuhimu kwao (wakati huu), Na wala halihusiani na Yajayo
yanayotarajiwa.
 
Kwa kadiri ya kwamba Sultani Jamsheed Bin Abdallah anaendelea kujitambua kuwa ni Sultani wa Zanzibar na kwa kadiri ya kwamba uzao wake unakidai kiti hicho kama urithi wa haki yao; na kwa kadiri ya kwamba wapo Wazanzibari ambao wanamtambua Jamsheed kama Sultani wao na ya kwamba wako tayari kurejesha status quo ya 1963 (ambapo Sultani alikuwa ni mfalme wa heshima Kikatiba kama ilivyo Uingereza - japo tofauti kidogo) basi juhudi zote za maridhiano haziwezi kufanikiwa kwani Sultani na uzao wake watakuwa ni kama kivuli juu ya Zanzibar na watu wake.

Ningependa CCM na CUF watoe misimamo yao kwa maswali yangu hayo.

Nakufagilia mkuu MKJJ kwa kuweza kuliona hilio na kufikiria mambo magumu!
Kwa hali iliyopo sasa ndani ya CCM hamna strategic thinkers wa kuona hizo flash points.
Inavoelekea ndani ya top achelons za CCM hakuna wanao weza kufikiri hatima ya kisiasa ya nchi zaidi ya kulindana na kulinda nafasi zao.
Utabiri wangu ni machafuko zaidi yanaweza kutokea Zenj baada ya kutambua kuwa Maalim Sharrif amewateka kiakili viongozi wa Zenj hata wa Bara.
 
Ili kukata mzizi wa fitna, kwa nini wasiulizwe raia wote wa JMT? Ikiwa upande mmoja utaukataa Muungano basi uvunjwe. Hii imani kuwa watanganyika wanautaka Muungano inabidi ipimwe. Watu wanaweza kushangaa hapo wazanzibari wakautaka na watanganyika wakaukataa!

Amandla......
Mmmm....watu mmenogewa na harufu za karafuu :D
 
Kwa kadiri ya kwamba Sultani Jamsheed Bin Abdallah anaendelea kujitambua kuwa ni Sultani wa Zanzibar na kwa kadiri ya kwamba uzao wake unakidai kiti hicho kama urithi wa haki yao; na kwa kadiri ya kwamba wapo Wazanzibari ambao wanamtambua Jamsheed kama Sultani wao na ya kwamba wako tayari kurejesha status quo ya 1963 (ambapo Sultani alikuwa ni mfalme wa heshima Kikatiba kama ilivyo Uingereza - japo tofauti kidogo) basi juhudi zote za maridhiano haziwezi kufanikiwa kwani Sultani na uzao wake watakuwa ni kama kivuli juu ya Zanzibar na watu wake.

Ili kuleta mapatano ya kweli (kama anavyosema Lula) basi hatima ya Sultani na uzao wake ni lazima ijadiliwe.

a. Je, ni jinsi gani Bw. Jamsheed anaweza kurudi Zanzibar bila ya kuwa na mamlaka ya Usultani yeye na uzao wake milele?

b. Je, Bw. Jamsheed anaweza kuwa na nafasi yoyote ya heshima katika Zanzibar ukiondoa ya kutambuliwa kama Sultani?

c. Je, akikubali kukana kiti cha Usultani, yeye mwenyewe, wanawe na wale wote walio katika mnyonyoro wa urithi milele anaweza kurudi Zanzibar na sehemu ya upatanishi ni kumrudishia baadhi ya mali zake zilizochukuliwa baada ya mapinduzi ya 1964?

d. Je, aweza kurudi pasipo kuwa na nafasi yoyote ya kisiasa na kukatazwa yeye mwenyewe na warithi wake kushiriki katika uongozi wa chama chochote cha siasa?

e. Je, Bw. Jamsheed katika kuleta mapatano yuko tayari kutambua na kukubali uwepo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Uzao wa Jamsheed (allexperts):

*Prince Sayyid Ali bin Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Khalifa bin Jamshid Al-Said
*Princess Sayyida Matuqa bint Jamshid Al-Said (1957-)
*Prince Sayyid Abdullah bin Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Wasfi bin Jamshid Al-Said (1972-)
*Princess Sayyida Adla bint Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Gharib bin Jamshid Al-Said


Ningependa CCM na CUF watoe misimamo yao kwa maswali yangu hayo.

- Saafi sana mkuu, you nailed it! Nasikia toka siku nyingi sana yupo London, standby akisubiri tu mambo yaive ili arudi kushika himaya yake!

Respect.


FMEs!
 
Pasco!!Huyo mtoto humjui? Si Maalim seif. Waulize akina Natepe watakwambia. Kizazi chao kiko Oman kwa akina Sultan Qaboos
 
Mimi nasema kabla ya kuundwa serikali ya mseto au kupiga kura ya serikali ya mseto.. ipigwe kura kwanza kati ya wale wanaotaka status quo ya Usultani baada ya uhuru wa 1963 irejeshwe. Then.. tuzungumzie Mseto si ndivyo ilivyokuwa baada ya uhuru?
 
MM ninakuheshimu kwa maala zako zilizotulia, lakini hii umelikoroga.

huyo sultani wenu aliviumba vile visiwa? ni Mungu pekee ndiye anayeweza kusema zanzibar au nchi nyingne yoyote kuwa ni yake milele, sio upuuzi wa mkoloni wa mashariki. kama bado kuna watmwa huko zanziba hadi leo wanaomtaka bwana wao arudi kuwaswaga ndio waende, wahesabu wameumia.

nakwambia siku nikisikia ajenda ya sultani jamsheed imeingizwa kwenye majadiliano, nakuapia siku hiyohiyo najiunga rasmi na siasa na nitawatukana hao wapumbavu watakaoingiza hoja hiyo waziwazi na hadharani, hata mtikila mtamuona nafuu siku hiyo!

nakwambia nitakasirika mpaka basi.................
 
Abeid Karume aliliona hili. Akaharakisha kwelikweli Muungano. Kijana wake wa kuzaa, Amani, anadhani kuna maridhiano bila kumshirikisha Sultani Jamsheed na watu wake wengi tu mbali na hao walioko CUF. Haitawezekana.

kuna watu wana objection hapo mkuu.............
 
Mzee Mwanakijiji, haya mambo ya Sultan ni magumu, niliwahi pata mnong'ono Sultan Jamseed alimpa mimba mjakazi wa Kipemba, kwenye Kasri la kifalme, ili kufunika kombe, siri isivuje, yule mjakazi akaozeshwa kwa mtu, kwa ahadi atatunzwa maisha yake yote. Kwenye ndoa hiyo, kazaliwa mtoto wa kiume mwana Sultan Jamsid

Huyo mtoto mpaka sasa bado angalipo yupo hai, bukheri wa afya japo ni mtu mzima sasa, na bado anatunzwa na ukoo wa Kisultan, ili deal isishitukiwe, wafadhili wa ukoo huu wa Kisultani, wanafadhiliwa na Sultani wa Brunei ambaye ni nasaba na Jamsid. Kwa vile mtoto huyo mwenye damu ya Kisultan yupo, na ni siri, subirini baada ya kuanza serikali ya umoja wa kitaifa, siri zitaanza kufichuka.

Zanzibar kuna mambo, visa, na mikasa. Hii ni simulizi nyingine ya minong'ono. kuna ndugu wawili waligombea mkate, aliyewapa mkate, aliwapa kwa heshima ya baba yao, ndugu mmoja akapata, mwenzie akakosa, yule aliyekosa akasisitiza mkate mwingine ukitolewa, lazima sasa iwe zamu yake. Wajuzi wa mambo wakasema, haitapendeza huo mkate kile siku uonekane kama mnapokezana, wenyewe waweza fikiria ni kama usultani.

Huyu ndugu aliyekosa ameng'angania, lazima na yeye apate, kwani ndiye mwenye haki rasmi ya kupata ule mkate toka mwanzo, eti yeye ndiye mtoto halali wa wa yule baba, aliyepata kwanza, alikuwa ni wa kufikia, ila ni siri tuu!.Ni simulizi tuu. kama Alfu Lela U Lela, au siku Elfu na Moja.

punguzeni hekaya za abunuasi humu jamvini!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kuna watu walifikiria kuongoza nchi ni lelemama. Usione vinaelea ... ... ... ndiyo sababu wanatuingiza katika mikataba tata sana kuanzia kwenye madini na sasa huu wa EAC we ngoja tu mi nasubiri moto uwawakie mikononi mwao.
 
Lazima nikiri kuwa kwa hapa history yangu ilikuwa finyu kidogo, kumbe kuna haya mamabo yanaendelea? Thanks MMJ nimepata uelewa mpya na mimi
 
daah! Huyu jamaa mkorofi kweli, bado unaendele kuwachoche tu na mahistoria wsielewane. WaZENJ wamesema wanasahau yaliyopita wewe unawang'ang'aniza tu! Na mahistoria yako ya kichochezi, utakosa nini wewe WaZENJ wakielewana?, hakuna lisilo na mwisho, lazima usome alama nyakati halafu ukubali matokeo, la sivyo utaonekana wa ajabu. Hakuna Mzenj anaeongelea habari za sultani, wewe hayo umeyapata wapi, huo ndio uchochezi usio na faida. Kizazi kilichopo sasa zenj hakuna yoyote alie athiriwa na Usltani, ni kizazi kipya kinacho hitaji maendeleo kwa gharama yoyote, ni kizazi kinacho angalia mbele sio kurudi nyuma kama unavyo taka wewe, historia hiyo uliyo bebeshwa wewe Wa Zenj hawana haja nayo kwa hiyo usipoteze muda, kama wewe ni muungwana kweli andika yatakayo wasaidia Wazenj na sio huu uchochezi wako.

asante mkuu, kweli hata mimi huyu jamaa leo amenitia hasira na fikra kama za karumekenge!.....................
 
Vipi Mwanakijiji umzima kaka ?maskini mwezetu mtu hujafa hujaumbika.
 
wapo.. kina Prince William na wale wa Uswazi; vivyo hivyo yupo Jamsheed na uzao wake ambao walitawala Zanzibar kwa zaidi ya miaka 200!!

believe me, hayo mambo kama yapo basi ndo yanaishiaishia, we subiri uone in less tha half a century yatakuwa historia kamili .............

Mkuu masultani bado wapo wengi tu. Nilipokuwa Canada nilishangaa jamaa ananiambia kwamba hiyo hapo ni ardhi ya Queen Elizabeth II.

sasa mwambie huyo qeen aje kuchukua ardhi yake uone kama atapewa!!!!!!! wansema hivyo kama sehemu ya historia tu, kiuhalisi hakuna mtu anaweza kusema anamiliki ardhi ama watu...............time will tell!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom