Sultan Qaboos wa Oman afariki dunia. Sultan Haitham Bin Tariq Al Said achaguliwa kuwa mrithi wake

Tindikali

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2010
Messages
1,370
Points
2,000

Tindikali

JF-Expert Member
Joined Mar 26, 2010
1,370 2,000
Tindikali

...sifahamu kuhusu siasa za ndani ila wametupita
Well, siasa za ndani huwa hakuna, Oman ya Sultani Kwabuzi.

He was a ruthless omnipotent ruler who brooked no political processes.

2014 alipotezwa mwandishi mkosoaji na mtetezi wa haki za binadamu Mohammed Alfazari, aliyewekwa kizuizini kituo cha polisi na kuondoka mazima.

Hakuna bunge, sheria za Oman zinapitishwa kwa tangazo la mfalme, royal decree. Anachoota usiku asubuhi kinatangazwa, mchana sheria!

Sultani Kwabuzi amekufa akiwa Gavana wa Benki Kuu ya Oman, Mkuu wa Majeshi ya Oman, Waziri wa Mambo ya Nje, Waziri wa Ulinzi na Sultani wa Oman, vyote kwa mpigo.

Dikteta Jean Bedel Bokassa, Seseseko Kuku Ngebendu, Dada Iddi Amini Nduli, walijilimbikizia mavyeo ya kijeshi na kiraia lakini uroho wao wa madaraka haukufikia wa kujiweka Ugavana wa Benki Kuu ili uwe mmiliki binafsi wa akaunti kuu ya nchi kama alivyofanya Sultani Kwabuzi.
 

Ivonovsky da White

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2012
Messages
829
Points
1,000

Ivonovsky da White

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2012
829 1,000
Inna li Llahi wa inna ilayhi rajiun.

Ni msiba mzito kwa Oman na dunia kwa ujumla.

Qaboos ni kiongozi wa kupigiwa mfano duniani. Sijawahi kusikia nchi ya Oman ikiwa na maadui.

Nijuavyo, Oman wakati wote wa Qaboos haikuingilia siasa za ndani au za nje za nchi yoyote duniani. Na kuingilia kwake nchi ya nje ni aidha kutoa misaada au kupatanisha tu.

Oman ni nchi pekee ya Kiarabu yenye raia wenye nidhamu ya hali ya juu katikanmaisha yao ya kila siku. Reflection ya uongozi wa Qaboos ulionekana kwa kila raia wa Oman.

Sijakutana na raia wa Oman ambae hakumpenda Qaboos. Sijakutana na raia wa nje ya Oman ambae amewahi kumponda Qabois au utawala wake.

Tanzania na Oman zina historia ya undugu wa karne na karne na hakuna ajuae ulianzia wapi exactly. Record za uhusiano na muingiliano baina ya Tanzania na Oman zipo za zaidi ya miaka elfu moja nyuma na ni dahari.

Allah amlaze pema peponi amsamehe yeye aliyetutangulia atusamehe nasi tunaoelekea huko kwenye makazi ya milele. Amin.
Kweli Waafrika tunasahau kabisa . Hawa hatuna undugu nao walituuza kama kuku hawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2011
Messages
68,421
Points
2,000

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2011
68,421 2,000
Kweli Waafrika tunasahau kabisa . Hawa hatuna undugu nao walituuza kama kuku hawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Si kweli, walio kuuza wazungu na babu zako, hao waliuondoa utumwa.

Wazungu mpaka leo hii wanawanunua na kuwauza, huelewi hilo?

Unaelewa meli ya kwanza kupeleka Waafrika America iliitwa Jesus, yes Yesu?
 

mr chopa

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2016
Messages
660
Points
1,000

mr chopa

JF-Expert Member
Joined Aug 26, 2016
660 1,000

Ivonovsky da White

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2012
Messages
829
Points
1,000

Ivonovsky da White

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2012
829 1,000
Sio kweli wazungu ndio walituuza na kutuweka kwenye zoo Kama nyani na ngedere mpaka leo wanaitwa black Americans nchi kibao za ulaya zimejaa kizazi Cha watumwa ila mzungu noma

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni waarabu ndo wamefanya yote hayo. Mbaya zaidi walikuwa wanawaasi ili wasizaliane. Huko America wanazaliana sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ivonovsky da White

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2012
Messages
829
Points
1,000

Ivonovsky da White

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2012
829 1,000
Si kweli, walio kuuza wazungu na babu zako, hao waliuondoa utumwa.

Wazungu mpaka leo hii wanawanunua na kuwauza, huelewi hilo?

Unaelewa meli ya kwanza kupeleka Waafrika America iliitwa Jesus, yes Yesu?
Unaelewa biashara ya utumwa ilianza mwaka gani? Sultan Said alikuwa kinara kwenda kuwachukua watumwa kigoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Messages
7,588
Points
2,000

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined Jan 14, 2010
7,588 2,000
January 13, 2020
Zanzibar, Tanzania

Khitma kwa ajili ya Sultan Qaboos yasomwa Zanzibar
Kufuatia kifo cha Sultan Qaboos bin Said wa Oman tarehe 10 Januari 2020, wakaazi wa Mji Mkongwe wa Zanzibar wamekusanyika kumuombea dua kiongozi huyo mashuhuri duniani.

Source: Weyani TV
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Messages
7,588
Points
2,000

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined Jan 14, 2010
7,588 2,000
January 13, 2020
Zanzibar, Tanzania
Makamu wa Kwanza mstaafu Maalim Seif awapa mkono wa pole WaOmani
Kufuatia kifo cha kiongozi wa Oman, Sultan Qaboos bin Said, kilichotokea juzi, Makamu wa Kwanza Mstaafu wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mshauri Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, amekwenda kwenye Ubalozi Mdogo wa Oman uliopo Mjini Unguja kwa kuwapa pole raia wa Oman kutokana na msiba huo.

Source: Weyani TV
 

zinj

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2013
Messages
949
Points
500

zinj

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2013
949 500
Afu watu wanashindwa elewa wa Oman kwa East Africa wapo wengi tu zaidi ya Zanzibar/Mombasa na wengi wapo ‘hinterland’ kuliko sehemu hizo za pwani kwa idadi (japokuwa machotara wa ki Oman ndo wengi zaidi)

Nashangaa hata wa Oman wengi wanajua ukisema umetoka Africa wanachukulia ni Zanzibar tu

Njoo Tanga, Mtwara,Lindi, baadhi ya sehemu Morogoro na nyumbani kwao sasa Tabora/Shinyanga (Shelui, Igunga, Nzega, Choma, Tinde, Itobo, Bukene, Nata, Mwangohe, Isaka, Kagongwa,Didia, Urambo, Sikonge, Mabama, Kaliua Sangilwa , Maganzo,Malampaka,Shagihilu nk) kuna jamii kubwa ya wa Oman sehemu hizo achia mbali Karagwe mpaka Rwanda na Burundi

Kwahiyo kwa baadhi ya jamaa zetu leo ni msiba mzito kwao ni WaTanzania kweli lkn pia historia yao inafungamana na Oman na ndo maana hakuna nchi nje ya Afrika na duniani kwa mtanzania yoyote huwezi kupata shida ya lugha ya Kiswahili zaidi ya Oman (Nina ushahidi kwa hili na mpaka vijijini kabisa nimefika Oman) kati ya watu wanne hauwezi kosa mmoja anaejua kiswahili na kuna wengine wanajua Kiswahili hata hawajafika huku wamejulia nyumban sababu wazazi wao wanaongea kiswahili labda kizazi hiki kiishe ndo kiswahili kwao kitaanza kupotea
Mkuu:
Kigoma Ujiji kuna msikiti uliojengwa na hawa wa Oman mwaka 1840.
 

zinj

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2013
Messages
949
Points
500

zinj

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2013
949 500
Ukweli ni kwamba Historia ya Oman ni sawa na ya Korea ya Kaskazini na Kusini.

Historia za Nchi hizo 3 zinafichwa na wala haziruhusiwi kuandikwa popote pale ndiyomana hazitoki nje ya Nchi isipokuwa zinabaki Ndani ya Vichwa vya Raia wao wanaozishuhidia tu.

Unajuwa sababu ni nini?

Raia yoyote wa Nchi hizo akitoa Historia au Jambo baya lolote la Nchi hizo basi anahukumia kifo kwa uhaini (Treason).

Hivi Unadhani Mapinduzi aliyoyafanya Qaboos dhidi ya babayake hayakumwaga damu?

Ukweli ambao hauruhusiwi kuzungumzwa na Raia yeyote wa Oman ni kuhusu Mapinduzi haya.

Mimi ni Mzanzibar na Nina Familia ambayo ni Raia wa Oman na Wanaishi Mascut Oman. Miongoni mwa wanayoyajua lakini hayawezi kuandikwa popote ni kuwa!

Qaboos baada ya kusoma Oman ni Waingereza ndiyo waliomuwezesha kumpindua babayake ili kuitoa Nchi katika Siasa za Mashariki (Communism) za Russia na China na kuingiza Oman katika siasa za Magharibi (Capitalism).

Bila ya Waingereza Qaboos hakuwa na uwezo wa Kumpindua babayake.

Na katika Harakati za Mapinduzi hayo Babayake Qaboos alijeruhiwa kwa kupigwa Risasi ya Mguu na Kukimbilia Uengereza ambako alitibiwa na Kufa kwa Jeraha.

Baada ya Kifo chake Historia ya Mapinduzi hayo ikawa Banned, Na kumbukumbu zote kuhusu Babayeke, Qaboos akazifuta na Raia wakawa forced kusahau Legacy ya Babayake Qaboos.

Hadi sasa hakuna historia ya Babayeke Qaboos iliyochapishwa.

Ni huyu Qaboos Mtoto ndiye aliyezuiwa kutajwa babayake na kuhakikisha anasahaulika kama aliishi Duniani.

Kwanini Hajaowa?
Baada ya Mapinduzi kabla ya Babayake Kufa alimtumia ujumbe Mwanawe na kumwambia "Kama Ulivyonipindua Mimi, na Wewe Atatokea Mtoto wako Akupindue".

Hapo ndipo akayachukua hayo Maneno kwa uzito na Kuachana na Habari za Kuowa au Kuzaa Mtoto wa Kwenye Ndoa kwa kuhofia kuja kupinduliwa na Mtoto wake.

Ndiyo hapo akawa anaishi kwa Kuletewa Wanawake anaowahitaji ndani ya Palace yake anagonga wanaishi kwa kipindi anachotaka yeye mwenyewe Qaboos then wanalipwa na kuondoka.

But nisawa na kutekwa na Wasiojuilikana yaani ukiingia kwenye Qasri ya Qaboos ukitoka katu hitosema ulichofanywa.

In Short Jamaa inawezekana anaowatoto ambao kawazaa illegally kwa Mila za Kiislam na hawahesabiki kuwa ni Wanae.

Hata Hivyo ukweli usiofichika ni kwamba Kafanya Mageuzi Makubwa ya Kiuchumi ndani ya Oman.
Mkuu:
Ahsante kwa ufafanuzi huu mzuri.
Hivi ni kweli kuna uhusiano wa kindugu kati ya Masultani walio tawala Zanzibar na hawa wa Sultanate of Oman?
 

chilubi

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Messages
6,247
Points
2,000

chilubi

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2011
6,247 2,000
Hata Trump alienda North Korea

Ki video kinachoonyesha Kikwete kaenda Oman hakifanyi Oman na Tanganyika kuwa na historical ties...

Zanzibar, Mombasa, regions along slave caravan routes across East Africa may care about Sultan Kwabuz.

Masses of Tanganyikans in the hinterland couldn't care less about an Oman sultan.
Upumbavu umekutawala kiasi icho kumbe :D
 

King Ngwaba

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2016
Messages
13,868
Points
2,000

King Ngwaba

JF-Expert Member
Joined May 15, 2016
13,868 2,000
Mkuu:
Ahsante kwa ufafanuzi huu mzuri.
Hivi ni kweli kuna uhusiano wa kindugu kati ya Masultani walio tawala Zanzibar na hawa wa Sultanate of Oman?
Ni kweli Masultan wa Oman na Wazanzibar walikuwa ni Watu wa Ukoo mmoja ambapo wote ni Kizazi cha Mfalme wa Oman aliyekuwa akiishi Zanzibar Sayyid Saeed Bin Sultan.

Kumbuka kuwa Makao Makuu ya Serikali ya Oman yalikuwa Zanzibar na Mfalme wa Oman alikuwa akiishi Zanzibar.

Ila katika Watoto wake wakatofautiana wakaamua kugawana Mmoja akarudi Oman kuwa Mfalme wa Oman pekee, na Mwengine akabaki Zanzibar kuwa Mfalme wa Zanzibar pekee.

Lakini Baada ya Uengereza kuitawala Oman na Zanzibar ikawa chini ya Muengereza.

Kwahiyo Zanzibar mpaka inapata Uhuru ilikuwa chini ya Uengereza huku Mfalme wa Zanzibar akiwa ni Puppet wa Uengereza na wala si Oman kama Watu wanavyodanganywa na kuaminishwa.

Oman yenye ilikuwa ni Koloni la Muengereza, Sasa Koloni litawezaje kutawala Zanzibar.

Na ukisoma harakati za kudai Uhuru za Kina Karume zote utaziona kuwa Walikiwa wakienda Uengereza kuzidai na wala Hawakuwahi kwenda Oman kidai Uhuru.

Na December mwaka 1963 (tarehe nimeisahau lakini unaweza kigoogle) utakutia kuwa Zanzibar ilikabidhiwa Uhuru wake kamili kitoka kwa Uengereza na wala si Oman.

Na Waziri Mkuu aliyekabidhiwa alikuwa ni Mswahili Muhamedi Shamte (Hakuna Muarabu anaitwa Shamte).

Bali kitokana na Chuki tu za baadhi ya Watu wa Ndani na Nje ya Zanzibar ndiyo zikapangwa njama za Kuipindua Serikali iliyokabidhiwa Uhuru ambayo Wazanzibari waliwapindua Wazanzibari wenzao.

Hakuna Muarabu aliyepinduliwa kwani Serikali na Viongozi wake walikuwa ni Waswahili.
 

Forum statistics

Threads 1,379,784
Members 525,565
Posts 33,756,474
Top