Makala Jr
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 3,395
- 1,110
Kamanda wa jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam,Suleiman Kova ameonya juu ya maandamano yanayoratibiwa na jumuiya ya madaktari pamoja na yale ya baraza la kiislamu.Kamanda Kova ameamuru kutofanyika kwa maandamano hayo kwani ni ishara ya uvunjifu wa amani kwani masuala yanayowafanya waandamane yapo chini ya mahakama.Kamanda Kova amesisitiza kwamba kama wanataka wafikishe ujumbe kuhusu kulaani kitendo alichofanyiwa Dr.Ulimboka basi wakae kwenye hall,wawaite waandishi wa habari kisha wauwasilishe ujumbe kwa njia hivyo kwani hata yeye ndivyo anavyofanya huwa haandamani.Pia Kova amedokeza juu ya kukamatwa kwa mtuhumiwa wa Genge la Gangster linalomilikiwa na mtu mmoja maarufu kwa jina la SILENCER. Ameongezeka kuwa mtuhumiwa yupo chini ya ulinzi na anahojiwa na polisi. source-Cloudz(taarifa ya habari,jioni ya leo) My Take:Nini jukumu la jeshi la polisi kuhusu maandamano na sheria inasemaje?