Sukari ya Uganda sawa, korosho zetu vipi? Kwahiyo jibu la waziri lilikuwa nonsense!

Tatizo ni mzimu wa Magu unawatesa, wanajaribu kila namna kumaliza kila kitu kilichokuwa na uhusiano wowote ule na Magu, ndo maana hakuna logic yoyote kwenye maamuzi yao, siajabu sababu hasa ni kutaka kumfurahisha Museveni ambaye alikuwa karibu na Magu sasa wamuweke upande wao.

Hawa watu hawana mapenzi yoyote wala hawajali chochote kuhusu Tanzania isipokuwa wao wenyewe .

Fikiria Bwawa la Nyerere lingetuingizia Megawatt zaidi ya 2000 hii ingepunguza bei ya umeme/ kWh kwa kaisi kikubwa sana na kupunguza gharama ya uzalishaji na mwishowe bei ya bidhaa madukani pamoja na sukari yenyewe au mafuta ya kula lkn hawalitaki na wana- sabotage, kwa nini ?
Nasikia hakuna kitu kinachoendelea huko bwawani mpaka muda huu. Ni bonge la hujuma kwa Nchi. Na ndiyo maana aliwekwa marope maana anaaminika kwa fitna. Tutakutana nao 2025.
 
Sukari ya Uganda ilishaleta tatizo la kisiasa Kenya. Ni Sukari inayotokana na viwanda vya wahindi waliowekeza Uganda. Sasa naona imehamia Tanzania

Haina shida ni kawaida kwa kila nchi kuwasaidia wazalishaji wake lakini, hata sisi Korosho zetu vipi? Mbaazi hazina soko, Pamba haina soko, Mazao kama kahawa ni shida tu! Hatujasikia Rais akihangaika kiasi hiki hadi kutukana waziri wake mbele ya Rais wa Uganda.

Yaonekana kila anayemtembelea rais, anapewa ahadi nzito. This is to be easy-going! Na kutaka sifa za kizembe Fulani hivi!
Muunde task force ya kulazimisha watu wanunue hizo bidhaa. Mnafikiria kuwa na task force za kufilisi watu tu kwa kuwadai wasichodaiwa? Hii kazi ni ya kwenu. Ile nyingine mliojipa ni dhulumati.
Mama akaipiga chini, tunaendeleza maisha
 
Duuh 🤣

Sawa kwa kuwa sukari si bidhaa ya umuhimu kwako.....
Ongeza ufahamu. UMewahi sikia njaa nchini kwa sababu ya ukosefu wa sukari TZ hii? Ulaya inatokea maana ni walaji mikate. Wewe pambana na ugali na magimbi.
 
Ongeza ufahamu. UMewahi sikia njaa nchini kwa sababu ya ukosefu wa sukari TZ hii? Ulaya inatokea maana ni walaji mikate. Wewe pambana na ugali na magimbi.
Kwa hiyo ufahamu wako ni kuwa Tanzania hatuli mikate?!!!

Ya kwamba BEKARI za kisasa na BUBU si biashara yenye kuingiza kipato ?!!!

Ya kwamba mijini hatuli maandazi ,kalimati na keki?!!!

Acha ufinyu wa fikra.....
 
Back
Top Bottom