Sukari sasa Tsh 6,000/- kwa kilo. Waziri Mkuu, zile tani ulizoagiza ziko wapi?

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Sukari imefikia tsh 6000/, nakumbuka waziri Mkuu alisema kuna sukari imeshaingia na nyingine ilikuwa inafika siku chance zijazo,najua kwa jinsi serikali hii inavyopenda vyombo vya habari lazima tungeoneshwa hiyo meli,binafsi sijaiona

Kwanini sukari inaendele kupanda?

Ni kweli iliagizwa kutoka wapi?

Nikipiga hesabu rahisi ni kwamba taifa limeingia hasara kubwa hasa wananchi kwa ujumla,kutoka kununua sukari 2000 mpaka 6000/ maana yake mwananchi anatumia 4000/ zaidi,kama watanzania milioni kumi-wakinunua sukari,hasara kwao itakuwa 4000*10,000,000/ sawa na bilioni arobaini kwa siku.

Sakata hili linakaribia mwezi sasa,sisi tupige hesabu ya siku kumi tu,40,000,000,000/zidisha Mara kumi,sawa na bilioni mia nne,kwa hiyo kama ni mwezi basi pesa zilizopotea kwenye uchumi ni nyingi sana.

Screenshot from 2016-05-19 07:55:33.png


Chanzo: Mtanzania
 
Hii wala siiti kuwa ni vita, huu udhaifu wa watu kutaka kuonekana kila waamuacho wao ndio sahihi, hapa ni busara kidogo tu, hata kijiko cha chai hakijai..........dakika mbili ni nyingi hili saga linaisha na maisha yanasonga kama kawaida.
Tatizo yupi wa kutoa hizo busara, kila mtu mbabe.
 
Wananchu tuliahidiwa kuwa neema inakuja baada ya tambo ya bei elekezi ya sukari kuwa sasa itakuwa Tshs.1,800 kwa kilo. Leo hii sukari hapa Mwanza ni Tshs.6,000 kwa kilo. Sisi wananchi tunajiuliza zile tambo za Serikali kuwa kilo ya sukari itakuwa Tshs.1,800 zimefikia wapi?.
 
HII NI SERIKALI YA KUKURUPUKA HUWEZI UKAMPANGIA BEI YA KUUZA MFANYABIASHARA IKIWA ANAONA HAPATI FAIDA KABISA BORA AIWEKE NDANI
NB:SULUHISHO NI SERIKALI KUAGIZA SUKARI YAO NJE YA NCHI NDO WAUZE KWA BEI WAITAKAYO AMA SIVYO MGOGORO HAUTAISHA NA WAFANYABIASHARA
Mkuu umeongea jambo zito,mfanyabiashara anunue sukari kilo 1850,unamwambia auze 1800
 
Back
Top Bottom